Makanjanja wengi kwenye vyombo vya habari sababu ya kupoteza mvuto....

kasenene

JF-Expert Member
Jun 6, 2008
1,632
2,413
Nimejaribu kufuatilia vyombo vya habari karibia vyoote (vya Redio na TV) hasa kipindi hiki cha uchaguzi na kugundua kuwa asilimia kubwa ya vyombo vya habari vimepoteza weredi wa kutoa matangazo yenye tija na ubora kwa jamii tofauti na ilivyokuwa hapo siku za nyuma. Nimejaribu kufuatilia nyanja zoote za Siasa,michezo n.k zoote “bila bila” labda kidogo Muziki angalau wanajitahidi kwa kuwa hiyo tasnia hata ukimchukua leo mtoto wa darasa la saba anaweza kutangaza Diamond katoa “single” mpya n.k lakini je kwani muziki wa zamani hatutaki kuusikia tena siku hizi?.Tasnia nyingine zoote zilizobaki yaani ukisikiliza leo WASAFI, EFM,Clouds n.k utaishia kubadilistha “station” kila baada ya dk tano. Vipo baadhi vichache saana ambavyo vinajitahidi kama Redio one,redio tumaini, ITV,TBC (hawa wanaponzwa na siasa vingienvyo wako vizuri saana wakiacha siasa) n.k. lakini na wao wakati mwingine sijui wanaathriki na upepo wa mrundikano wa vyombo hivyo na kujiasahau.Nimejaribu kutafuta chanzo cha tatizo nikagundua yafuatayo:-

  • Elimu ndogo ya watangazaji wengi wa Redio an TV
  • Mamlaka (TCRA) kuachia olela utaratibu wa kaujiri wafanyakazi wa sekta hii bila kujari weredi…
  • Uvivu wa kufuatilia mambo na matukio ya msingi na yenye manufaa kwa jamii
  • Copy and paste (hii inapendeza ikabaki hivi hivi kwa kiswahili)
Wekeni sababu nyingine wakuu
 
Back
Top Bottom