Makamu wa Rais, Samia Suluhu atuma salamu za pole kwa kifo cha Getrude Rwakatare. Amuombea upepo wa kisulisuli

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Makamu wa Rais wa Tanzania Samia Suluhu kwa kutumia ukurasa wa Twitter ametuma salamu za rambirambi kutokana na kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalumu, Mchungaji Dkt. Getrude Rwakatare.

Amesema "Kwa Masikitiko na mshtuko nimepokea taarifa ya kifo cha aliyekuwa Askofu na Mchungaji wa Kanisa la Mlima wa Moto (Mikocheni B Assemblies of God) na Mbunge wa Viti Maalum CCM Mhe. Dr. Gertrude P, Lwakatare kilichotokea leo April, 20, 2020".

Ameogezea na kusema "Namuomba Mwenyezi Mungu ailaze Roho ya Marehemu peponi na amjaalie Upepo wa Kisulisuli Amin."

Capture.PNG


photo_2020-04-20_12-06-53.jpg
 
Upepo wa kisulisuli naona kama umetumika mahala sipo hebu wataalam wa lugha mukuje
 
Ameogezea na kusema "Namuomba Mwenyezi Mungu ailaze Roho ya Marehemu peponi na amjaalie Upepo wa Kisulisuli Amin."
Marehemu ajaaliwe na mja wake upepo wa Kisulisuli.. Sijui umpeleke wapi?

Jr
 
Upepo wa kisulisuli naona kama umetumika mahala sipo hebu wataalam wa lugha mukuje
... ni kweli! Upepo wa kisulisuli angalau kwa mfano wa Nabii Elia ni gari lililomtwaa Elia duniani kumpeleka Mbinguni. So, upepo wa kisulisuli ni kwa walio hai sio waliokwisha fariki.
 
Baada ya watu kuanza kuuliza naye yuko wapi, naona kaibukia twitani. Hivi watanzania wangapi wana account twita?

Kingine nimeangalia video ya ibada yake ya mwisho, naona marehemu alisema corona imeletwa na Mungu huku akimnukuhu Bwana Yesu. Sasa najiuliza, aliyejiteua kama mkuu wa malaika si alisema huu ni ugonjwa wa shetani?

Mchungaji Lwakatare katika ibada yake ya mwisho
 
Masihara na msiba huu yatasababisha maafa. Watu wapigwe marufuku kwenda Kwa msiba huu.
 
Upepe wa kisuli suli.. Nginja Nginja mpaka Jehanamu.. DADEKI...!
Nimekuelewa SAMIA,
 
Influenza,
Kipindi tupo seminarini upepo wa kisulisuli ukitokea ulikuwa unaacha madhara mabaya kwa form one. Sijajua Mhe Vice amemaanisha nini kumtakia mwenzake upepo wa kisulisuli

Acha kukaa kihasara hasara
 
Back
Top Bottom