Makampuni ya China yayazidi makampuni ya Marekani kwenye kandarasi za benki ya dunia

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,036
VCG111164344558.jpg

Katika siku za hivi karibuni Ofisi ya uwajibikaji ya serikali ya Marekani (GAO), ilitoa ripoti iliyohusu hali ya kandarasi za benki ya dunia kati ya China na Marekani, ikionesha kuwa China inaiacha Marekani kwa mbali, kwenye kunufaika na kwenye utekelezaji wa kandarasi hizo. Hali ambayo inaonesha kukubalika kwa makampuni ya China kimataifa, haijafurahiwa na Marekani na sasa inaanza kuchukuliwa kama ni moja ya maeneo ya kuishambulia China.

Wabunge wa chama cha Republican waliitaka Ofisi ya uwajibikaji ya serikali ya Marekani (GAO) kufanya utafiti kuhusu hali ya ushindani kati ya kampuni ya Marekani na China kwenye utekelezaji wa kandarasi za benki ya dunia, baada ya kuona Marekani inaachwa nyuma kwenye utekelezaji wa kandarasi nyingi kwenye nchi wakopaji kwa benki hiyo.

GAO ilitakiwa kutafiti mambo makuu mawili. Kwanza ni kujua kandarasi ngapi zilienda kwa Marekani, na pili ni kujua kama kati ya kandarasi hizo zilienda kwa kampuni yoyote ambayo imewekewa vikwazo na Marekani. Sababu ya kwanza inatokana na kuwa kwa sababu Marekani ni mchangiaji mkubwa wa benki ya dunia, inajiona kuwa yenyewe ndio inatakiwa kunufaika zaidi. Na sababu ya pili ni kuona inaweza kudhibiti vipi makampuni ya kigeni ambayo yameonesha uwezo wa kuyapiku makampuni ya Marekani.

Matokeo ya utafiti huyo yameonesha kuwa makampuni ya Marekani yalipata sehemu ndogo ya kandarasi na kuachwa nyuma kwa mbali, ikilinganishwa na makampuni ya China. Makampuni ya China yalipata 29.2% ya fedha za miradi katika kipindi cha kati ya mwaka 2013 na 2022, ambazo ni sawa na dola za kimarekani bilioni 21, wakati Marekani ilipata 2.4% ya fedha, sawa na dola za kimarekani bilioni 1.7.

Matokeo haya ambayo yametajwa na baadhi ya wabunge kuwa ni changamoto ya usalama dhidi ya Marekani, yamefichua udhaifu au kupuuza kwa Marekani kwenye utekelezaji wa kandarasi katika sehemu mbalimbali dunia, ambako kwake faida za kiuchumi na maslahi vinakuwa mbele kuliko kitu chochote.

Pamoja na kuwa faida za kiuchumi ni msingi wa mchakato wote kwenye kutafuta kandarasi kwenye zabuni, makampuni ya China yamekuwa yakiangalia mbali zaidi ya hapo. Ili mradi utekelezaji wa kandarasi hautasababisha hasara kwa pande mbili, makampuni ya China yanakuwa tayari kutekeleza zabuni katika eneo lolote duniani. Ndio maana ni hali ya kawaida kuona makampuni ya China yakishiriki kwenye zabuni katika nchi tajiri kabisa duniani na hata kwenye nchi maskini kabisa duniani.

Siku zote China imekuwa ikisema kuwa ushirikiano kati yake na nchi nyingine ni ushirikiano wa kunufaishana, na sio ushirikiano wa kunufaisha upande mmoja tu na kuufanya upande mwingine uendelee kuwa duni. Ndio maana faida sio nguvu pekee ya msukumo wakati makampuni ya China yanatafuta kandarasi. Kwa nchi zenye uwezo mdogo kifedha, makampuni ya China yamekuwa ni chaguo zuri kwao, na hizi ndio sababu zinazofanya makampuni ya China yapate kandarasi zaidi.
 
China anatafuta colonies duniani kupitia debt traps. Nendeni Sri Lanka, Djibouti na Zambia mukawaulize.
 
Wamarekani wanaona kufanya kazi Africa ni ujunga isipokuwa kwenye kuiba na kupora madini.

Wachina wataendelea kuwa ndugu zetu kwa kuwa hata huku kijijini nachingwea wapo wakitujengea barabara.
Wachina hawawajengi barabara bure, wanalipwa pesa nono na wakati mwingine wanatukopesha kwa benki zao kutujengea kwa hiyo wafaidikia mara mbili.
 
Katika siku za hivi karibuni Ofisi ya uwajibikaji ya serikali ya Marekani (GAO), ilitoa ripoti iliyohusu hali ya kandarasi za benki ya dunia kati ya China na Marekani, ikionesha kuwa China inaiacha Marekani kwa mbali, kwenye kunufaika na kwenye utekelezaji wa kandarasi hizo. Hali ambayo inaonesha kukubalika kwa makampuni ya China kimataifa, haijafurahiwa na Marekani na sasa inaanza kuchukuliwa kama ni moja ya maeneo ya kuishambulia China.

Wabunge wa chama cha Republican waliitaka Ofisi ya uwajibikaji ya serikali ya Marekani (GAO) kufanya utafiti kuhusu hali ya ushindani kati ya kampuni ya Marekani na China kwenye utekelezaji wa kandarasi za benki ya dunia, baada ya kuona Marekani inaachwa nyuma kwenye utekelezaji wa kandarasi nyingi kwenye nchi wakopaji kwa benki hiyo.

GAO ilitakiwa kutafiti mambo makuu mawili. Kwanza ni kujua kandarasi ngapi zilienda kwa Marekani, na pili ni kujua kama kati ya kandarasi hizo zilienda kwa kampuni yoyote ambayo imewekewa vikwazo na Marekani. Sababu ya kwanza inatokana na kuwa kwa sababu Marekani ni mchangiaji mkubwa wa benki ya dunia, inajiona kuwa yenyewe ndio inatakiwa kunufaika zaidi. Na sababu ya pili ni kuona inaweza kudhibiti vipi makampuni ya kigeni ambayo yameonesha uwezo wa kuyapiku makampuni ya Marekani.

Matokeo ya utafiti huyo yameonesha kuwa makampuni ya Marekani yalipata sehemu ndogo ya kandarasi na kuachwa nyuma kwa mbali, ikilinganishwa na makampuni ya China. Makampuni ya China yalipata 29.2% ya fedha za miradi katika kipindi cha kati ya mwaka 2013 na 2022, ambazo ni sawa na dola za kimarekani bilioni 21, wakati Marekani ilipata 2.4% ya fedha, sawa na dola za kimarekani bilioni 1.7.

Matokeo haya ambayo yametajwa na baadhi ya wabunge kuwa ni changamoto ya usalama dhidi ya Marekani, yamefichua udhaifu au kupuuza kwa Marekani kwenye utekelezaji wa kandarasi katika sehemu mbalimbali dunia, ambako kwake faida za kiuchumi na maslahi vinakuwa mbele kuliko kitu chochote.

Pamoja na kuwa faida za kiuchumi ni msingi wa mchakato wote kwenye kutafuta kandarasi kwenye zabuni, makampuni ya China yamekuwa yakiangalia mbali zaidi ya hapo. Ili mradi utekelezaji wa kandarasi hautasababisha hasara kwa pande mbili, makampuni ya China yanakuwa tayari kutekeleza zabuni katika eneo lolote duniani. Ndio maana ni hali ya kawaida kuona makampuni ya China yakishiriki kwenye zabuni katika nchi tajiri kabisa duniani na hata kwenye nchi maskini kabisa duniani.

Siku zote China imekuwa ikisema kuwa ushirikiano kati yake na nchi nyingine ni ushirikiano wa kunufaishana, na sio ushirikiano wa kunufaisha upande mmoja tu na kuufanya upande mwingine uendelee kuwa duni. Ndio maana faida sio nguvu pekee ya msukumo wakati makampuni ya China yanatafuta kandarasi. Kwa nchi zenye uwezo mdogo kifedha, makampuni ya China yamekuwa ni chaguo zuri kwao, na hizi ndio sababu zinazofanya makampuni ya China yapate kandarasi zaidi.
Hili sio jambo la kusherekea pesa za miradi ya benki ya dunia kwenda kwa wingi kwa China. Pesa za benki ya duni zinatakiwa zibaki ndani katika hayo mataifa masikini yanayopewa kwa ajili ya maendeleo
 
Bidhaa hafifu na za bei rahisi za China zitaua kabisa sekta ya viwanda muhimu Africa. Urusi hakuna kitu zaidi ya Ngano, Mbolea na AK 47.
Hilo halina upinzani, tutashtuka baadae na kuanza wakataa tumechelewa
 
Bidhaa hafifu na za bei rahisi za China zitaua kabisa sekta ya viwanda muhimu Africa. Urusi hakuna kitu zaidi ya Ngano, Mbolea na AK 47.
Ushakkulaa kkande umeshiba unakuja kujamba uku bidhaa za China zinauzwa hadi marekani uyo Russia uchumi wa ulaya umepungua ssababu yake nyie mna gesi, dhaabu, makaa ya mawe, misitu, bahari lkin mavi matupu
 
Sijui kama umesoma kwa umakini alichoandika!
tafakari pia hali halisi ilivyo duniani na ukweli kamili.
Usiwe na tabia ya kukurupuka kama uharo!
 
Hili sio jambo la kusherekea pesa za miradi ya benki ya dunia kwenda kwa wingi kwa China. Pesa za benki ya duni zinatakiwa zibaki ndani katika hayo mataifa masikini yanayopewa kwa ajili ya maendeleo
Afrika akili zipo kwenye ngono tu ni ngumu kuwa sawa na watu wenye akili nyingi hao wachina na wazungu dogo acha kuota ndoto za kipuuzi
 
Ushakkulaa kkande umeshiba unakuja kujamba uku bidhaa za China zinauzwa hadi marekani uyo Russia uchumi wa ulaya umepungua ssababu yake nyie mna gesi, dhaabu, makaa ya mawe, misitu, bahari lkin mavi matupu
Wamarekani wana viwanda vingi sana China kwa hiyo sehemu kubwa tu ya faida bado inarudi Marekani.
 
Back
Top Bottom