Makamba usipotoshe Nyanda za Juu Kusini hakuna ukame

Uongo we upo Tukuyu gani? Kuna mradi wa Barabara huko Tukuyu umesimama kwa ajili ya nvua,wewe upo Tukuyu gani nakuuliza?
Acha kuwa mvivu. Mito Chumala na Kimani ndo chanzo cha Mto Ruaha Mkuu ikiwa ni pamoja na Mto Ndembera toka mafinga. Mito hii ndo inayotegemewa pia kwa shughuli za Umwagiliaji hapa Mbarali. Hadi muda huu vibali vya kufungua maji havipo kutokana na udogo wa maji mitoni. Acheni kushabikia uwongo. Hiyo mvua ya Tukuyu unayoisema haijaweza kuleta hata maji mitoni. Nenda Ruaha National Park uone jinsi wanyama wanavyohangaika kupata maji. Nenda Ruaha Mbuyuni uone kiasi cha maji kinachopita ndani ya Mto Ruaha. Msiwe mnashiba maharage jana na kuja kujamba jamba huku.
 
Msimu wa mvua ndiyo kwanza unataka kuanza, ni ukame upi unaosema?
Msimu umechelewa katika mikoa ya kusini. Hata kaskazini kuliko Mto Pangani mvua za vuli hazipo na kusababisha maji kupungua ndani ya mto pangani ambao unategemewa kuzalisha umeme pale Hale na Pangani
 
Msimu umechelewa katika mikoa ya kusini. Hata kaskazini kuliko Mto Pangani mvua za vuli hazipo na kusababisha maji kupungua ndani ya mto pangani ambao unategemewa kuzalisha umeme pale Hale na Pangani
Meneja wa bwawa la Mtera amesema bwawa la Mtera lina maji ya kutosha kuzalisha umeme kwa miezi 7 hata kama hakuna hata tone moja la mvua, sasa kwa nini kuna upungufu wa umeme? Kupungua kwa umeme wa Hale hakuwezi kuathiri upatikanaji wake kwa nchi nzima kwani ni mdogo sana takribani megawatts 20.
 
Mtera capacity yake ni kuzalisha Megawatt 80. Huo upungufu wa Megawatt 350 umechangiwa na Hale/Pangani, Kidatu na Kihansi. hata Mtera ni suala la muda tu. Jua likiendelea kukamua hivi ilivyo hata hiyo miezi 7 nakuhakikishia hawatafika maana yale maji yana watumiaji zaidi ya TANESCO. Mtera pana mifugo, maatumizi ya majumbani, wanyama, wakulima wa mboga mboga n.k

Msisahau pia suala ya Evaporation.
 
Acha kukariri!

Uwezo wa Hale ni megawatts 21 na Pagani ni megawatts 68, kupungua kwa umeme kutoka vyanzo hivi hakuwezi kuleta taharuki nchini.

Mtera, Kidatu na Kihansi hakuna upungufu wa maji hivyo vyanzo hivi vinapaswa ku-operate katika full capacity. Aidha umeme mwingi zaidi tunapata kutoka vyanzo vya gesi ambavyo vinazalisha 60% ya umeme wote wa nchi. Vyanzo vya maji vinazalisha 40% ya umeme wote.

Kwa hiyo tusisingizie maji badala yake tutafute nini chanzo cha tatizo!
 
Mkuu sasa tukuamini wewe ama tumwamini Waziri - na kama anaendelea kuwa ofisini hadi muda huu maana yake Mamlaka yake ya uteuzi (Rais) imeridhika na utendaji wake wa kazi.
 
Acha kukariri!

Uwezo wa Hale ni megawatts 21 na Pagani ni megawatts 68, kupungua kwa umeme kutoka vyanzo hivi hakuwezi kuleta taharuki nchini.

Mtera, Kidatu na Kihansi hakuna upungufu wa maji hivyo vyanzo hivi vinapaswa ku-operate katika full capacity. Aidha umeme mwingi zaidi tunapata kutoka vyanzo vya gesi ambavyo vinazalisha 60% ya umeme wote wa nchi. Vyanzo vya maji vinazalisha 40% ya umeme wote.

Kwa hiyo tusisingizie maji badala yake tutafute nini chanzo cha tatizo!
Upo wakati uanongea huu upuuzi wako. Umewahi kufika Kidatu hivi karibuni? Umeona kile kiasi cha maji kilicho ndani ya Mto Ruaha? Kumbuka Kidatu halina bwawa kama la Nyumba ya Mungu na Mtera. Inategemea mtiririko wa maji mtoni. Pia Kihansi haina bwawa kama la Mtera. Ina reseivor dogo linalotegemea mtiririko wa maji mtoni.
 
Msimu wa mvua ndiyo kwanza unataka kuanza, ni ukame upi unaosema?
Kwa bahati mbaya ni nchi chache sana duniani ambazo nishati zake hutegemea chanjo kikuu kimoja tu ambacho ni mvua - isiponyesha tunauza mechi yaani tunaanza msako nyumba kwa nyumba nani mchawi.
 
Tumeona picha walizopiga kupitia chopa, sasa wewe unaleta maneno matupu hapa, weka na wewe picha zako tulinganishe vinginevyo ni majungu tuu.
 
Jana katika ziara ya Makamba alipotembelea mabwawa ya kuzalisha umeme alitoa taarifa akitaka kuaminisha umma kuwa tatizo la upungufu wa umeme nchini na kwa sababu ya ukame! Hii si kweli hata kidogo.

Kwa macho yake mwenyewe ameona bwawa la Mtera lina maji ya kutosha, na kwa kuthibitisha hilo meneja wa bwawa amemwambia maji yaliyopo yanatosha kuzalisha umeme kwa full capacity ya megawatt 80 kwa miezi 7 hata kama hakuna hata tone moja la mvua litanyesha.

Kama bwawa la Mtera limejaa maji, iweje bwawa la Kidatu likose maji? Kwa sababu moja ya sababu ya kujenga bwawa la Mtera ilikuwa kuhifadhi maji kwa ajili ya bwawa la Kidatu.

Aidha kwa taarifa zilizopo bwawa la Kihansi linatapika maji. Kwa maana hiyo mabwawa yote ya Mtera, Kidatu na Kihansi yana maji ya kutosha kuzalisha umeme kwa full capacity yao.

Kuhusu mvua ni kuwa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini ina msimu mmoja wa mvua kuanzia Novemba/Disemba hadi April/Mei. Kwa hiyo huu ndiyo mwanzo wa msimu wa mvua, sasa huo ukame ni wa lini?

Hivyo namuomba Makamba afanye homework yake atafute nini chanzo cha upungufu wa umeme na siyo kusingizia maji. Maji yapo!

Huyu mwamba naona ameamua zile wanaziita "Me against the world"
 
Back
Top Bottom