Ileje
JF-Expert Member
- Dec 20, 2011
- 8,796
- 12,239
Jana katika ziara ya Makamba alipotembelea mabwawa ya kuzalisha umeme alitoa taarifa akitaka kuaminisha umma kuwa tatizo la upungufu wa umeme nchini na kwa sababu ya ukame! Hii si kweli hata kidogo.
Kwa macho yake mwenyewe ameona bwawa la Mtera lina maji ya kutosha, na kwa kuthibitisha hilo meneja wa bwawa amemwambia maji yaliyopo yanatosha kuzalisha umeme kwa full capacity ya megawatt 80 kwa miezi 7 hata kama hakuna hata tone moja la mvua litanyesha.
Kama bwawa la Mtera limejaa maji, iweje bwawa la Kidatu likose maji? Kwa sababu moja ya sababu ya kujenga bwawa la Mtera ilikuwa kuhifadhi maji kwa ajili ya bwawa la Kidatu.
Aidha kwa taarifa zilizopo bwawa la Kihansi linatapika maji. Kwa maana hiyo mabwawa yote ya Mtera, Kidatu na Kihansi yana maji ya kutosha kuzalisha umeme kwa full capacity yao.
Kuhusu mvua ni kuwa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini ina msimu mmoja wa mvua kuanzia Novemba/Disemba hadi April/Mei. Kwa hiyo huu ndiyo mwanzo wa msimu wa mvua, sasa huo ukame ni wa lini?
Hivyo namuomba Makamba afanye homework yake atafute nini chanzo cha upungufu wa umeme na siyo kusingizia maji. Maji yapo!