Makamba: Mnyika acha Unafiki, sote tumeshindwa Bungeni!

hakuna tofauti kati ya mnyika na wahuni wahuni wengine anaendesha siasa za kihuni za kudanganya watu na kuwahadaa watu sijaona cha maana kwake ila uongo ndiyo sili yake.
 
In fact nadhani hii thread badala ya kusomeka:

"Mnyika acha Unafiki, sote tumeshindwa Bungeni"


ilitakiwa kusomeka:
"Mnyika acha Unafiki, CHADEMA mmeshindwa Bungeni"


Kwa kweli katika hili CHADEMA wakubali walichemka kuwatetea wananchi; usiniulize kwa nini.
Kwa nini hutaki kuulizwa,au ndo hizo akili za kuambiwa?
Wabunge wametumwa na wananchi kuwawakilisha bungeni,pale wanapozidiwa nguvu na wapinzani wao kwa ushabiki wa vyama,ni muhimu kurudi kwa wananchi waliowatuma.
Binafsi nawapongeza wabunge wa CDM maana hawakuanza leo kurudi kwa wananchi kuelezea waliyoyasimamia bungeni wakashindwa kwa sababu ya uchache wao. Ongera sana J.Mnyika ,raia wema tuko pamoja nanyi kwa sala na maombi,hakika mtashinda.
HAKI HUINUA TAIFA BALI DHAMBI NI AIBU KWA WATU WOTE.
 
hakuna tofauti kati ya mnyika na wahuni wahuni wengine anaendesha siasa za kihuni za kudanganya watu na kuwahadaa watu sijaona cha maana kwake ila uongo ndiyo sili yake.
Malizia jina lako basi(mimi kuku),na kweli akili ya viumbe vyote iko kichwani,na kwa kuwa kichwa cha kuku ni kdogo bila shaka na akili yake ni ndogo.Na mwenye akili ndogo hawezi kuelewa akili kubwa inamaanisha nini.
 
Hivi Mnafiki ni nani kati ya hawa wawili? Makamba ambaye yuko serekalini na hoja ililetwa bungeni na serekali na ililetwa baada ya kubarikiwa na baraza la mawaziri ambaye yeye ni mjumbe au Mnyika ambaye yeye ni mbunge wa upinzani ambaye mara zote huwa hawakubali hoja za serekali lakini kwa sababu ya uchache wao wanazimwa?
Hivi Januari Makamba mpaka lini utagundua kuwa wananchi wa Tanzania wana uwezo wa kuchambua jema na baya? Makamba huna haja ya kuandika hapa, kawadanganye watu wa Bumbuli ambao hawajui chochote kuhusu jinsi mambo yanavyokwenda, sio watu wa kwenye mtandao. Nawewe Zitto, usijifanye una hekima kuliko wenzako. You were supposed call them and talk to them, usijitafutie cheap popularity.
Viva Mnyika

Mnafiki ni mnyika,yeye ni sehemu ya bunge lililopitisha hoja hii kama hakupenda wananchi tuumizwe mbona hakuipigia kelele kabla au baada ya wananchi kugundua kwamba wabunge wote wapo kwa maslai yao.
Siku zote anadandia hoja ili asikike lakini hiki kijamaa ni kijinga kweli,hadi sasa kero alizoahidi zitakwisha bado tunateseka na bei ya maji inazidi kupanda au kwa kuwa wanaotuuzia maji dumu 2000 ni ndugu zako

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Kwa nini hutaki kuulizwa,au ndo hizo akili za kuambiwa?
Wabunge wametumwa na wananchi kuwawakilisha bungeni,pale wanapozidiwa nguvu na wapinzani wao kwa ushabiki wa vyama,ni muhimu kurudi kwa wananchi waliowatuma.
Binafsi nawapongeza wabunge wa CDM maana hawakuanza leo kurudi kwa wananchi kuelezea waliyoyasimamia bungeni wakashindwa kwa sababu ya uchache wao. Ongera sana J.Mnyika ,raia wema tuko pamoja nanyi kwa sala na maombi,hakika mtashinda.
HAKI HUINUA TAIFA BALI DHAMBI NI AIBU KWA WATU WOTE.

Jifunze kusoma between the lines na tafakari kwa kina kama GT. Inaonekana hukuelewa nilichokiandika. Pole.
 
Kwa hiyo unamaanisha kuwa hiyo kodi ya laini ya simu ilipitisha na wabunge wa CCM...!! Hiyo ndio point ya msingi, kwa uelewa wangu wa bunge letu hata CDM wangepinga bado ingepita tu kwa nguvu ya wabunge wa CCm..!!

Exactly! Tena Spika akavuruga ratiba badala ya bajeti kupitishwa Jnne kama ilivyokuwa kwenye ratiba siku ambayo pia wabunge wa Chadema wangekuwa Bungeni, akalazimisha bajeti ipitishwe Jtatu kinyume na ratiba. Matokeo yake ndio hayo. I believe wabunge wa Chadema wasingekubaliana na huu ujinga.
 
Yaani mnaweza piga kelele na mwsho lisifanyike lolote na kodi tulipe oooh! Tanzania yangu mbona unatutesaa!!?

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
nyie midudu acheni umbururaaa wakati jamaa wanafanya uaramia wa ndiooo makamanda walikiwa msibani mbona mnajitoa akili mnajifanya hamjui kama wakati huo mliwatandika mabomu kule arusha?
Mburura ni wewe unaeshikiwa akili na wenzako....na utaendelea kushikiwa akili hivyo huku mwenyewe ukijidhani kwamba ndo muelewa kumbe ni sakala tu...
 
Mnyika anapenda sifa za kizamani sana ndio maana alichemka chuo kijana mzima hana degree

Hawa wana degree
Nchemba , JK , Pinda , Nape, na list ni ndefu ndani ya CCM akina Muhongo, Mgimwa nk Nchi iko wapi ?
 
HUYU January Makamba amepwaya sana, amshukuru sana Mh zitto kuingilia katilasivyo angeshushiwa nondo angeshindwa kuzijibu kabisa. yani mtu ni waziri lakini bado analalamika na akiambiwa anaita watu wanafiki.

Na kama unafiki umefanya mtetemeshwe kiasi hiki nakuanza kusema turudi kuifuta wakati wewe January ni mjumbe wa baraza la mawaziri na hii kodi uliijua kabla hata ya kuwasilishwa ni bora unafiki uendelee maana unaonekana kutusaidia sisi wananchi.

Nauliza tena hivi January nae huu uwaziri alibembelezwa kama Muhongo? anafanya nini? mbona kapwaya sana, mbona ana lilia tuu?
 
Wabunge watatu vijana wenye ari ya kusonga mbele kisasa. Wote watatu wakiwa na lengo moja la kuifuta kodi ya sim card.

Nadhani Mh. Makamba ndiye aliyeanza kumtupia Mh. Mnyika vijembe na hili ni kosa kubwa.

Ila Mh. Mnyika angetumia hekima katika hilo na si kuweka hadharani namba za mawaziri wawili bila idhini yao.

Na Mh. Zito angekuwa na dhamira ya dhati kuwarekebisha wenzie ange wa PM au kuwapigia simu na siyo kutafuta umaarufu juu ya malumbano yao kwa kutuonyesha kwamba yeye ana hekima zaidi yao.

Wote watatu naona wamekosea katika hili.
 
Kuwepo Dodoma, Arusha au Mwanza wakati wa vikao vya bunge ni maamuzi au matokeo ya vipaumbele vya mbunge binafsi. Hii si hoja msingi katika kujitetea juu ya maamuzi mabovu ya bunge.

Tukumbuke pia kwamba bunge ikifanya mema ni pongezi kwa Bunge lote. Na vile vile likiboronga ni lawama kwa bunge lote. "It is a collective decision system"

Binafsi naweza tu kumtoa mbunge mmoja au kundi la wabunge kwenye uamuzi fulani wa bunge endapo (wa)atapeleka hoja binafsi/mswada wa kupinga kisha ukagonga mwamba.
 
Tozo hiyo ilipendekezwa na Bunge lenyewe kupitia kamati ya bajeti inayoongozwa na Mbunge wa Bariadi mashariki na aliyekuwa mwanasheria mkuu wa serikali ya awamu ya tatu Mhe. Andrew Chenge. Na imeelezwa kwamba kamati hiyo ilipendekeza wananchi watozwe shs 1,450. Hivyo baada ya serikali kupokea mapendekezo hayo iliyachambua na kupunguza hadi shs 1,000 kwa line moja ya simu. Sasa suala la serikali kukusanya maoni ya wananchi litatoka wapi tena wakati suala lenyewe limependekezwa na wawakilishi au wasemaji wa wananchi. Wakulaumiwa zaidi ni hawa wabunge wetu (wasemaji kwa niaba ya wananchi). Hivyo huenda wabunge wa kamati hiyo walikusanya maoni ya wananchi ndio maana wakaja na mapendekezo hayo.

Sasa kama huenda walikusanya kama unavyodhani yaana "may be" unamaanisha..ni wananchi wepi hao mbona wanalalamika?? Amini ndugu yangu hata kama utajitahidi kuliona liko sawa jambo hili lakini WANANCHI WA NCHI HII hawashirikishwi katika miswada hii unayoisikia ikitoka tu ndio hulalamikiwa.. hayo yaliyoletwa na Mh. Chenge ni mwazo yake binafsi na si hata ya wale wa jimbo lake!! Na mawazo ya wananchi wa jimbo moja hayawakilishi mawazo ya watanzania wote.. Ujue tu mawzo ya Mbunge wa CCM hupokelewa kwa hisia za kuwabana wapinzani na mwisho kuwakomoa wananchi wala sio hao wapinzani. Hivyo maoni ya wananchi pia kueleweshwa juuu ya suala hili kabla kutengeza sheria zinazowaudhi ni muhimu. Otherwiswe unambie kama ulifuatwa na wahusika (wabunge/mbunge) ama hata kuona katika vyombo vya habari mitandao wananchi wakielimishwa na kupewa nafasi ya kutoa mawazo yao dhidi ya hii issue..
 
Wabunge watatu vijana wenye ari ya kusonga mbele kisasa. Wote watatu wakiwa na lengo moja la kuifuta kodi ya sim card.

Nadhani Mh. Makamba ndiye aliyeanza kumtupia Mh. Mnyika vijembe na hili ni kosa kubwa.

Ila Mh. Mnyika angetumia hekima katika hilo na si kuweka hadharani namba za mawaziri wawili bila idhini yao.

Na Mh. Zito angekuwa na dhamira ya dhati kuwarekebisha wenzie ange wa PM au kuwapigia simu na siyo kutafuta umaarufu juu ya malumbano yao kwa kutuonyesha kwamba yeye ana hekima zaidi yao.

Wote watatu naona wamekosea katika hili.

Sijaona kosa la zitto hapo na sijaona kosa la Mnyika hapo maana hata hiyo namaba ya January ukitaka utaipata kwenye website ya bunge na sio siri sema January hawezi kuhimiri Nondo za Mnyika imebidi Mh zitto amnusuru January maana angepewa Nondo nyingine ange hisi amevuliwa nguo. Kama uamini ninayo yasema muulize Nape anamjua vizuri Mnyika linapokuja swala la kujenga hoja na hapa Makamba ilibidi awe mpole na angeonekana muungwana kuliko kupanic wakati yeye ni mhusika mkuu kwenye kuweka hii kodi. hivi ujiulizi kwa nini ccm wamekuwa wapole kwenye hili?
 
Tukiacha ushabiki wa Kisiasa, January kasema ukweli, ingawa kwa hasira, kuwa alijaribu na akashindwa. jambo hili sidhani linafaa yeye kujiuzulu kama wengi wanavyomtaka. usisahau serikali nia yake ni kuongeza pato na kupunguza budget deficit ambayo ni aibu ya Tanzania bado, ingawa binafsi sikubaliani kama simu ni chanzo kizuri, ni ufinyu tu wa kufikiri mbali na kutaka majibu mepesi kwa matatizo makubwa.

Mnyika amechukua nafasi yake vizuri kama Mbunge wa chama cha Upinzani. hapa si ugomvi wa Makamba na Mnyika, hii ni shughuli ya serikali na upinzani. Upinzani wanapaswa kuweka pressure kama anavyoweka Mnyika ili ku-hold accountable serikali wawajibike kwa maamuzi yenye madhara kwa wananchi.

Ninamuona Makamba anavyoteswa na maamuzi haya ambayo kimsingi hayatokani na yeye binafsi, lakini naamini wananchi mnapaswa kuwaunga mkono hawa wawili na wengine wengi wanaopinga hili, na kuanza kulipigia kelele.
 
Back
Top Bottom