Makamba: Mnyika acha Unafiki, sote tumeshindwa Bungeni!

Makamba: Mnyika acha Unafiki, sote tumeshindwa Bungeni!

January kama unaona wabunge wa CCM hawapo kwa maslahi ya taifa, hama..hamia huku.....
 
Mnyika anapenda sifa za kizamani sana ndio maana alichemka chuo kijana mzima hana degree

Mgimwa na January wana degree mbona hazijawasaidia kugundua hii kodi ni fimbo kwa wanyonge?
 
Kwani hii namba ya Makamba ilikuwa ni siri? Kuna kipindi aliiweka mtandaoni kwa wana Bumbuli kumfikia kirahisi wanapokuwa na shida. Makamba na wizara yako, Chama chako na serikali ya CCM as whole, mmechemsha
 
anatuzidi wengi tu, wengine paragraph mbili lazima aweke na tusi, yaani kwake tusi ni kama chachandu kwenye mbuzi choma-- nafikiri mnamjua hakuna hata haja ya kumtaja hapa.

Unamaanisha yule economist akiyepigwa ban ya mwezi mzima....?
 
Unapokuwa na viongozi vijana kama Makamba ambao ni wasomi lakini wanafiki na wanaopewa vyeo kwa Kujikomba pamoja na kusaidiwa na wazazi wao, tunakosa amani moyoni kuhusu hatima ya nchi yetu. Vijana wanaochipukia walitakiwa wajifunze kwa wenzao kama J. Makamba vile. Hivi anashindwa kuomba msamaha Kwa niaba ya serikali kuhusu usumbufu kwa wananchi uliotokana na maamuzi yao mabaya (serikali ndio inapeleka mswaada Bungeni) mpaka atafute mtu wa kumlaumu wakati na yeye ni sehemu ya serikali, au siku hizi kwenye baraza la mawaziri hakuna kitu kinachoitwa "uwajibikaji wa pamoja?" (Collective responsibility).

Nadhani kuna Ombwe la uongozi hivyo vijana wamekosa kujua uongozi ni nini hivyo
kilichobaki ni kujikomba komba tu. Hivi huyu Makamba alitegemea Mnyika afanye nini zaidi ya kupaza sauti tu ya kutokubaliana hizo tozo. Tunavyojua wanaofanya Maamuzi bungeni ni ccm ambao kila kitu wanasema ndiyo (sijui huwa wanasoma miswaada hawa?). Nadhani hizi ndio siasa chafu kupindukia na kama viongozi tulionao ni aina hii, tunakoelekea ni kitendawili

CCM wajue kwamba, vitu vinavyofanya watu makini waichukie waziwazi au kimya kimya ni pamoja na mambo yao kujikombakomba ili upate cheo au unafiki walionao.
​
 
CCM mnalaumik kwa hili na mnastahili lawama...badala ya kukomaa kumlaumu MNYIKA ni bora urudi kuwalaumu wabinge woote wa chama chako.....
 
Mnyika amekomaa kuwa hawezi kuliachia jambo hilo. Sijaona kama ang'ang'ania ni SIASA. Ila kijana mnafki anajulikana tu hapo. Mtu uwe kwenye Wizara hiyohiyo yenye kuleta huo upuuzi alafu unajidai kutetea watu toka lini?
 
Binafsi niseme tu kuwa, ndugu yangu Januari Yusufu Makamba anamapungufu makubwa katika tafakuri ya mambo mazito,

Yeye ni Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia ambapo mamlaka ya mawasiliano ipo chini yake,

Yeye ni mbunge wa ccm, ambapo mswada wowote wa serikali kabla ya kupitishwa na Bunge ilikuwa sheria ni lazima WABUNGE wa chama chenye serikali wakutane na kuridhia upitishaji huo, kisha huingia bungeni na kupitisha kwa KAULI moja,

Sasa haiingii akili kijana tunaemtegemea kuwa injini ya maamuzi mema anakuwa na akili nyepesi kiasi hiki, anafanya siasa kwenye mambo yasiyohitaji siasa?

Sasa ndio anataka tuamini kuwa ana maslahi katika makampuni haya ya simu nchini?,

Wabunge wote CCM wamelipitisha hili suala la kodi ya simu kadi bila hata kusita, na kibaya zaidi limepitishwa kipindi kile cha mpito wa Mauaji ya BOMU yaliyofanywa na JESHI la polisi kule ARUSHA ambapo wabunge wote wa CHADEMA walikuwa huko na wale waliorejea hawakupata fursa ya kupitia jambo hili kwa utuvu,

Sasa Januari atueleze wazi kuwa yeye na tumu yake wameshindwa kusimamia wizara hii na wapishe watu wengune,

Watanzania ni werevu na wanatambua kuwa kulipa kodi ni lazima, lakini wanayo haki yakupinga kodi zenye sura ya unyanyasaji na za kifisadi!

Hivi mtanzania anaeishi chini ya mstari wa umasikini (under poverty line) wa shilingi 260 kwa siku, aliyejikakamua kwa miezi sita na kufanikiwa kumiliki simu ya 15,000/= leo umtake alipe 1000 kwa mwezi, gharama ya mda wa maongezi nayo imepanda, gharama ya chakula imepanda, gharama ya matibabu imepanda, gharama ya maji imepanda, nauli imepanda,

Lakini cha ajabu KIPATO cha Mtanzania huyu HAKIJAPANDA, je ataweza mzigo huu????

Januari mtoto wa Makamba fikiria kwanza kabla hujatoa maneno mkuu!

Takwimu za uchumi wa Tanzania kupitia GIN 2000-2010 zinasema kuwa, watanzania 60% wanaishi chini ya mstari wa umasikini, na watanzania 26% ni maikini wa wastani, wakati WATANZANIA 14% ni matajiri wanaoishi maisha ya anasa wakimiliki mahekalu ya kifahari na watoto wao kusoma shule za sifa ya kimataifa,

Sasa jiulize, je Bibi zetu akina Maseto, Mng'anzagala, Chabilibi, Muhuvila, walipe shilingi 1000 sawa na Reginand Mengi, Jakaya Kikwete, Ridhiwani Kikwete, Edward Lowasa, Freeman Mbowe, Yusufu Manji?????????

Kodi hii ni mzigo kwa Watanzania 60% wanaoishi chini ya mstari wa umasikini!

Serikali isitishe haraka sana kabla watanzania hatujaamua kuisitisha wenyewe!

Kumbe Polisi ndo walifanya Mauaji ya Arusha ??? kwa mjibu wa Maeleza yako???? ""Wabunge wote CCM wamelipitisha hili suala la simu kadi bila hata kusita, na kibaya zaidi limepitishwa kipindi kile cha mpito wa Mauaji yaliyofanywa na JESHI la polisi kule ARUSHA ambapo wabunge wote wa CHADEMA walikuwa huko na wale waliorejea hawakupata fursa ya kupitia jambo hili,""
 
big up zitto kabwe!nakukubali b'se huna akili za bavicha new generation ambao malumbano na matusi ndio jadi yao
 
Upuuzi tu wa kutaka madaraka... To is what is important kupiga soga kwenye simu au kupata umeme na maji? Full stop!!!
 
Siasa za akina mnyika haziwezi kutufikisha popote make ni unafiki mtupu .
 
ahaa wa@@@@@ wameacha kututete huko bungeni wanakuja huku mtandaon ili tujue nini watuchefue huyo mnyika pamo ja na makamba wote wako bungeni nawalikuwa na uwezo wotee kwa pamoja kutetea maslai ya wananch wao kutafuta sifa za kijinga

Uwe unatumia akili hata kidogooo tu,wakati wanapitisha bajeti yao ya mabwepande wabunge wote wa cdm walikuwa arusha kwenye mazishi ya mripukp wa polinyinyiemu. sasa kwakuwa kumbukumbu zako hazijulikani zimekalia wapi basi tena utafanye inabidi uje uje humu ndani tukupatie japo kidogo
 
Mnapokuwa bungeni wabunge wa CCm huwa mnajitoa roho linabaki kasha tu la mwili! aibu kabisa!!

Kila siku bunge lenu litakuwa la kupitisha sheria kiushaniki wa ndiyoooooo kwa vile mko wengi, wananchi akiwalaumu mnapeleka mswada wa marekebisho. Inakuwa kama mnampma mngonjwa homa kwa mkono, fike mahali ccm muwe na aibu na mtumie akili kuliko vitu mnavyotumia sasa hivi, hii ni aibu kwa wabunge wa ndio hata kwa mambo yasiyo na tija ka ananchi
 
156395_547413758655490_286445152_n.jpg
 
Back
Top Bottom