Makamba chukua hatua, la sivyo hutaeleweka

Makamba chukua hatua, la sivyo hutaeleweka

Mtu anapoteuliwa na mwenye madaraka ya kuteua anavyo vigezo anavyovihitaji mteuzi kwa kazi anayotaka mteuliwa aitimize. Vigezo hivyo si lazima viwe vya uaminifu tu wa kufanya kazi, bali hata vya ubabaishaji kama mteuzi anataka mteuliwa akawe mbabaishaji.

Tukisema Makamba kapewa kazi maalum katika wizara hiyo aliyoteuliwa kwa vile anakidhi vigezo vya kufanya ufisadi kwa niaba ya mteuzi tutakuwa tunakosea?

Makamba hajajiteua awe kwenye wizara nyeti namna ile, sasa kwa nini tuendelee kuwa tunamwona Makamba ndiye mbaya, kumbe yeye yupo ili atimize matakwa ya mkubwa wake aliyemweka hapo.

Sijui ni kwa nini watu hupenda sana kulaumu hawa watu walio chini kwa kila jambo, hata wakati ambapo mharifu ni mtu aliye pembeni kabisa, ambaye sisi tunamwona kama malaika asiyeweza kufanya uharibifu.

Ndio umekosea maana huna ushahidi wowote wa hayo uliyoyasema.
Acha porojo weka ushahidi
 
Kwanza ungejiuliza kwa nini inakuwa hivyo.
Kwa nini kelele nyingi zielekezwe kwake na siyo kwa waziri mwingine. Ukianzia hapo unaweza kujua kwa nini Makamba anahusishwa na hizi shutuma nyingi.

Usitake tu kufunga akili yako kwa mapenzi uliyonayo kwake, jaribu kujiuliza swali hilo 'critically' ukiwa na 'open mind'.

Kuna kundi flani la watu ndio muda wote wanapiga kelele juu yake sio watu wote.
Hatutaki maneno tupu tupe ushahidi tukuunge mkono kwenye kupiga kelele
 
Waambie mkuu, labda wataanza kukuelewa wewe.

Makamba yupo kufanya kazi maalum, sawa na ile aliyokabidhiwa wakati ule wa uchaguzi wa 2015, wa kuiba kura kimtandao.

Safari hii kapewa jukumu la kuhakikisha pesa ya kutosha inapatikana kabla ya 2025, na pengine ya ziada ya kuwekeza baada ya majukumu ya urais kufikia kikomo.

USHAHIDI uko wapi?
 
Kama unafuatilia habari za kisiasa. Hivi karibuni Makamba amekuwa akitajwa sana kwenye mitandao ya Jamii forums na Twitter kwa tuhuma mbalimbali.

Kuna wabunge pia wamemuattack directly kama wakina Luhanga Mpina na Msukuma.

Busara mara nyingi huwa ni kunyamaza ukweli ujitenge na uongo. Lakini kuna wakati inabidi kutoka na kuchukua hatua za ziada kabla mambo hayajaaminika.

Uongo ukisemwa sana hugeuka kuwa ukweli. Ni muda sasa wa Makamba kutoka na kukanusha habari hizo, na ikiwezekana kuchukua hatua za kisheria kama walivyofanya Fatma Karume na Membe dhidi ya Musiba.

Lakini pia kama yasemwayo ni kweli hebu jitafakari sana, hata kama una ukaribu sana na Rais ni vizuri ujiuzulu.

Rais Mwinyi aliwahi kujiuzulu ukweli ukafahamika na baadae akaja kuwa Rais.

Haina maana kung'ang'ania kitu kama kinazidi kuharibika.
Ni wakati uchague kati ya mawili toka ujitetee au jiuzulu.

Kukaa kimya kwa nyakati kama hizi ni kuzidi kuharibu mambo.
Wakati ambao serikali inapaswa kuchukua hatua ili kubana matumizi.

Mlamba asali Mwingine huku amechukua helikopta kuzunguka nchi nzima.

Eti anakagua maendeleo ya zoezi la uandikishwaji anuani za makazi rasmi ya wananchi.
Screenshot_20220411-165316_YouTube.jpg
Screenshot_20220411-165240_YouTube.jpg
 

Attachments

  • IMG-20220331-WA0020.jpg
    IMG-20220331-WA0020.jpg
    40.9 KB · Views: 8
  • IMG-20220331-WA0020.jpg
    IMG-20220331-WA0020.jpg
    40.9 KB · Views: 15
Waambie mkuu, labda wataanza kukuelewa wewe.

Makamba yupo kufanya kazi maalum, sawa na ile aliyokabidhiwa wakati ule wa uchaguzi wa 2015, wa kuiba kura kimtandao.

Safari hii kapewa jukumu la kuhakikisha pesa ya kutosha inapatikana kabla ya 2025, na pengine ya ziada ya kuwekeza baada ya majukumu ya urais kufikia kikomo.

Hilo liko wazi na utakuta mama anamwambia kaza hapo hapo na target yetu unaijua

Yaani kweli wamesema serikali haina dini sasa ukiingia na dini unaiacha kwenu uwe wa Dini yeyote

Mfungo huu ila bado haki Hakuna
Huyo ilikuwa atumbiliwe ila ni mission

Haya Houthi hawapigwi mwezi huu sijui na wao hawaibi mwezi huu
 
Mliambiwa kuwa ni kwaajili yake?
Naona sasa unataka ligi isiyo na maana, au unataka niseme mengine yasiyotakikana? Acha ligi ndugu yangu... hata michango ya kununua mitihani hiyo inajulikana nani alikuwa mwasisi wake, wengine tulikuwa waathirika tu kutokana na kadhia hiyo... weka ushahidi kama hutaki kuamini kwamba ni mmojawapo wa walioiba hiyo mitihihani ya Necta maana naona kama unataka kumtetea... au kama hutaki kukiri kwamba aliiba mitihani hiyo (na mimi nakuambia kwamba ni classmate wake na deal zima lilivyokuwa au lilivyosukwa nalijua pia- weka ushahidi kumsafisha) na sio yeye peke yake... na washirika wake pia...cha msingi hayo yamepita, sio haja ya kuyaendeleza, ila wizi ule ulituathiri sana (kisaikolojia pia ) wanafunzi wengi kwa kufutiwa matokeo yale... wengine ndio maana walikimbilia forest kumalizia, wengine tunajijua mbinu zetu...
 
Kuna kundi flani la watu ndio muda wote wanapiga kelele juu yake sio watu wote.
Hatutaki maneno tupu tupe ushahidi tukuunge mkono kwenye kupiga kelele
Sasa kama ni kundi fulani tu linapiga kelele, si waache tu watachoka kama ni kelele zisizokuwa na maana yoyote? Mbona wewe unashinda hapa ukirudia "ushahidi, ushahidi..." Ushahidi wa nini kama unajua ni kundi tu la watu!

Kuonyesha hofu kubwa uliyonayo juu ya huyo mtu wako, umepoteza hata uwezo wa kujenga hoja za kumtetea kwa hayo yanayosemwa juu yake, umebakia tu na hilo la "shahidi", unalorudiarudia kwenye kila bandiko unaloweka.
 
Back
Top Bottom