Makamba chukua hatua, la sivyo hutaeleweka

Makamba chukua hatua, la sivyo hutaeleweka

Waziri anayeongoza kwa shutuma akiulizwa anasema tatizo ni uwaziri wake, kila siku shutuma mpya kwa mtu yule yule huku wajinga wakimtetea mnamuonea wivu!, utadhani waziri ni yeye pekee.

Kama hili taifa lingekuwa na vyombo vinavyoeleweka kuchunguza mienendo ya watu kabla ya kupewa vyeo naamini tusingefika hapa.

Tatizo vetting wanafanyiwa wasio na "connection", lakini wale wenye "connection" wanaingizwa serikalini bila kujali historia ya utendaji wao, na uadilifu wao.

Matokeo yake wanaenda kumchafua mpaka aliyewaweka kwa kujiegemeza kwake wakibanwa kwa udhaifu wao, japo naamini hayo ndio malipo ya wale wasioshughulisha akili zao, mzazi akiwa na mtoto mtukutu sifa mbaya ni zake pia.
Mtu anapoteuliwa na mwenye madaraka ya kuteua anavyo vigezo anavyovihitaji mteuzi kwa kazi anayotaka mteuliwa aitimize. Vigezo hivyo si lazima viwe vya uaminifu tu wa kufanya kazi, bali hata vya ubabaishaji kama mteuzi anataka mteuliwa akawe mbabaishaji.

Tukisema Makamba kapewa kazi maalum katika wizara hiyo aliyoteuliwa kwa vile anakidhi vigezo vya kufanya ufisadi kwa niaba ya mteuzi tutakuwa tunakosea?

Makamba hajajiteua awe kwenye wizara nyeti namna ile, sasa kwa nini tuendelee kuwa tunamwona Makamba ndiye mbaya, kumbe yeye yupo ili atimize matakwa ya mkubwa wake aliyemweka hapo.

Sijui ni kwa nini watu hupenda sana kulaumu hawa watu walio chini kwa kila jambo, hata wakati ambapo mharifu ni mtu aliye pembeni kabisa, ambaye sisi tunamwona kama malaika asiyeweza kufanya uharibifu.
 
Kelele zimekuwa nyingi Makamba fisadi, Makamba mwizi, ndio zake hizo lakini hakuna hata ushahidi kuwa siku fulani alikula shilingi kiasi flani kwa mishe flani
Kwanza ungejiuliza kwa nini inakuwa hivyo.
Kwa nini kelele nyingi zielekezwe kwake na siyo kwa waziri mwingine. Ukianzia hapo unaweza kujua kwa nini Makamba anahusishwa na hizi shutuma nyingi.

Usitake tu kufunga akili yako kwa mapenzi uliyonayo kwake, jaribu kujiuliza swali hilo 'critically' ukiwa na 'open mind'.
 
Kiongozi lazima uwajibike kwa unaowaongoza, kuwa transparency ili wasiwe na dukuduku kwako. We kalia pumba eti anamajukum ya kitaifa, nani alishapewa majukum kiasi cha kukosa muda wa kujenga hoja za wanaokukosoa.
Habari za chato?
 
Kwanza ungejiuliza kwa nini inakuwa hivyo.
Kwa nini kelele nyingi zielekezwe kwake na siyo kwa waziri mwingine. Ukianzia hapo unaweza kujua kwa nini Makamba anahusishwa na hizi shutuma nyingi.

Usitake tu kufunga akili yako kwa mapenzi uliyonayo kwake, jaribu kujiuliza swali hilo 'critically' ukiwa na 'open mind'.
Kwa nini usirahisishe kazi kwa kutupa ushahidi wa huo upigaji na wizi wa Makamba?
 
Watu wanapiga hela kujiandaa na Uchaguzi ujao maana uchaguzi unataka watu wale eti sasa watakula makopo?
Waambie mkuu, labda wataanza kukuelewa wewe.

Makamba yupo kufanya kazi maalum, sawa na ile aliyokabidhiwa wakati ule wa uchaguzi wa 2015, wa kuiba kura kimtandao.

Safari hii kapewa jukumu la kuhakikisha pesa ya kutosha inapatikana kabla ya 2025, na pengine ya ziada ya kuwekeza baada ya majukumu ya urais kufikia kikomo.
 
Makamba kwa mama ni sawa alivyokuwa bashite kwa jiwe
He is untouchable
 
Kwa nini usirahisishe kazi kwa kutupa ushahidi wa huo upigaji na wizi wa Makamba?
Wewe unahangaika sana kiasi kwamba huongezi thamani yoyote kwenye michango yako na haya unayoyashikia bango.
Shutuma hazihitaji zitolewe ushahidi, ila ni jukumu la anayeshutumiwa kujisafisha kuhusu shutuma zinazoelekezwa kwake.

Shutuma hazielekezwi kwa mtu yeyote bila kuwepo na viashiria au vitendo vinavyoonyesha uwepo wa shutuma hizo. Kwa hiyo ni kazi ya mshutumiwa kuonyesha vitendo anavyovifanya havihusiani na shutuma anazohusishwa nazo.
 
Kama unafuatilia habari za kisiasa. Hivi karibuni Makamba amekuwa akitajwa sana kwenye mitandao ya Jamii forums na Twitter kwa tuhuma mbalimbali.

Kuna wabunge pia wamemuattack directly kama wakina Luhanga Mpina na Msukuma.

Busara mara nyingi huwa ni kunyamaza ukweli ujitenge na uongo. Lakini kuna wakati inabidi kutoka na kuchukua hatua za ziada kabla mambo hayajaaminika.

Uongo ukisemwa sana hugeuka kuwa ukweli. Ni muda sasa wa Makamba kutoka na kukanusha habari hizo, na ikiwezekana kuchukua hatua za kisheria kama walivyofanya Fatma Karume na Membe dhidi ya Musiba.

Lakini pia kama yasemwayo ni kweli hebu jitafakari sana, hata kama una ukaribu sana na Rais ni vizuri ujiuzulu.

Rais Mwinyi aliwahi kujiuzulu ukweli ukafahamika na baadae akaja kuwa Rais.

Haina maana kung'ang'ania kitu kama kinazidi kuharibika.
Ni wakati uchague kati ya mawili toka ujitetee au jiuzulu.

Kukaa kimya kwa nyakati kama hizi ni kuzidi kuharibu mambo.
Kumbuka BABA mtu mbelenya mkuu wa nchi na mbele ya kipazia sauti aliwaambia waTanzania " NI WAKATI WA KULAMBA ASALI".
Hivi haya maneno Rais, viongozi na waTanzania mliyachukuliaje?




Sent from my SM-A115AZ using JamiiForums mobile app
 
Kama unafuatilia habari za kisiasa. Hivi karibuni Makamba amekuwa akitajwa sana kwenye mitandao ya Jamii forums na Twitter kwa tuhuma mbalimbali.

Kuna wabunge pia wamemuattack directly kama wakina Luhanga Mpina na Msukuma.

Busara mara nyingi huwa ni kunyamaza ukweli ujitenge na uongo. Lakini kuna wakati inabidi kutoka na kuchukua hatua za ziada kabla mambo hayajaaminika.

Uongo ukisemwa sana hugeuka kuwa ukweli. Ni muda sasa wa Makamba kutoka na kukanusha habari hizo, na ikiwezekana kuchukua hatua za kisheria kama walivyofanya Fatma Karume na Membe dhidi ya Musiba.

Lakini pia kama yasemwayo ni kweli hebu jitafakari sana, hata kama una ukaribu sana na Rais ni vizuri ujiuzulu.

Rais Mwinyi aliwahi kujiuzulu ukweli ukafahamika na baadae akaja kuwa Rais.

Haina maana kung'ang'ania kitu kama kinazidi kuharibika.
Ni wakati uchague kati ya mawili toka ujitetee au jiuzulu.

Kukaa kimya kwa nyakati kama hizi ni kuzidi kuharibu mambo.
Yaani Makamba ajiuzulu sababu ya nyie takataka!??? Hivi nyie misukule Ya dikteta kichaa mmerogwa au??
 
Nani kakufundisha kuwa shutuma hazihitaji kutolewa ushahidi?

Elimu ya wapi hiyo?
Wewe unahangaika sana kiasi kwamba huongezi thamani yoyote kwenye michango yako na haya unayoyashikia bango.
Shutuma hazihitaji zitolewe ushahidi, ila ni jukumu la anayeshutumiwa kujisafisha kuhusu shutuma zinazoelekezwa kwake.

Shutuma hazielekezwi kwa mtu yeyote bila kuwepo na viashiria au vitendo vinavyoonyesha uwepo wa shutuma hizo. Kwa hiyo ni kazi ya mshutumiwa kuonyesha vitendo anavyovifanya havihusiani na shutuma anazohusishwa nazo.
 
Nani kakufundisha kuwa shutuma hazihitaji kutolewa ushahidi?

Elimu ya wapi hiyo?
Kwani wewe una elimu, hadi uhoji niliyonayo mimi. Nikiangalia michango yako mingi humu JFkila mara nakuona kama mchumia tumbo tu ambaye kichwani hana kitu chochote.
 
Kwenye utawala wa Jk kipindi cha maana Magu amengia mwishoni mwa 2015
Rais si alikuwa miaongoni mwa wapigaji cos Vodacom ilikuwa chini ya lowasa rafiki wa mtukufu Jk
Bunge si ndo lele tena lakupisha la kina wasila, ngeleja Makamba n.k

Kwahiyo alipiga shilingi ngapi na alipigaje?
 
Hii nchi mazezeta ni weng sana. Hivi wivu au chuki kwa mtendaji mzuri utauanikia wapi watu wakuelewe na kukujadili? Ukiona kiongoz anajadiliwa ujue kuna shida mahala

Tatizo wanaomjadili ni kakikundi flani kenye vinasaba flani vya ukabila.
 
Siyo vizuri kwa mustakabali mwema wa taifa kuruhusu watu watoe tuhuma hovyo hovyo kama zilizokuwa za musiba ili waziri au mtumishi mwingine wa uma achafuke.
Kama kuna ushahidi uwekwe hadharani na Makamba awajibike, ila kama hakuna, wanaoeneza uzushi washughulikiwe kwa mujibu wa sheria.
Siasa za kijinga zisipewe nafasi.
Ushahidi utolewe, kama hakuna wanaomtuhumu wakae kimya hadi wapate ushahidi, vinginevyo wanafanya makosa kisheria na kimaadili.

Kabisa mkuu sio tuhuma zina hang tu kila mtu anasema lake. Kama ni fisadi afungwe kama sio anayesambaza uongo afungwe
 
Back
Top Bottom