Makamba chukua hatua, la sivyo hutaeleweka

singojr

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2014
Posts
5,315
Reaction score
6,896
Kama unafuatilia habari za kisiasa. Hivi karibuni Makamba amekuwa akitajwa sana kwenye mitandao ya Jamii forums na Twitter kwa tuhuma mbalimbali.

Kuna wabunge pia wamemuattack directly kama wakina Luhanga Mpina na Msukuma.

Busara mara nyingi huwa ni kunyamaza ukweli ujitenge na uongo. Lakini kuna wakati inabidi kutoka na kuchukua hatua za ziada kabla mambo hayajaaminika.

Uongo ukisemwa sana hugeuka kuwa ukweli. Ni muda sasa wa Makamba kutoka na kukanusha habari hizo, na ikiwezekana kuchukua hatua za kisheria kama walivyofanya Fatma Karume na Membe dhidi ya Musiba.

Lakini pia kama yasemwayo ni kweli hebu jitafakari sana, hata kama una ukaribu sana na Rais ni vizuri ujiuzulu.

Rais Mwinyi aliwahi kujiuzulu ukweli ukafahamika na baadae akaja kuwa Rais.

Haina maana kung'ang'ania kitu kama kinazidi kuharibika.
Ni wakati uchague kati ya mawili toka ujitetee au jiuzulu.

Kukaa kimya kwa nyakati kama hizi ni kuzidi kuharibu mambo.
 
Waziri anayeongoza kwa shutuma akiulizwa anasema tatizo ni uwaziri wake, kila siku shutuma mpya kwa mtu yule yule huku wajinga wakimtetea mnamuonea wivu!, utadhani waziri ni yeye pekee.

Kama hili taifa lingekuwa na vyombo vinavyoeleweka kuchunguza mienendo ya watu kabla ya kupewa vyeo naamini tusingefika hapa.

Tatizo vetting wanafanyiwa wasio na "connection", lakini wale wenye "connection" wanaingizwa serikalini bila kujali historia ya utendaji wao, na uadilifu wao.

Matokeo yake wanaenda kumchafua mpaka aliyewaweka kwa kujiegemeza kwake wakibanwa kwa udhaifu wao, japo naamini hayo ndio malipo ya wale wasioshughulisha akili zao, mzazi akiwa na mtoto mtukutu sifa mbaya ni zake pia.
 
Mawaziri wa saivi wanaraha wanachakujitetea.

CORONA
VITA YA UKRAINE NA RUSSIA.

Wakiulizwa kuhusu mfumuko wa bei, umeme kukatika, taarifa kuhusu tozo kwenye mitandao ya simu, nk watapiga porojo mwisho utasikia sababu corona na vita.

Sasa najiuliza kale kamdudu na putin wana ujasiri wakukata kata umeme wetu, bila kuogopa shoti.

covid na vita kiboko inazuia hadi serikali kushindwa kutangaza tozo tumekusanya shs. Ngapi.
 
Waziri anayeongoza kwa shutuma akiulizwa anasema tatizo ni uwaziri wake, kila siku shutuma mpya kwa mtu yule yule huku wajinga wakimtetea mnamuonea wivu!, utadhani waziri ni yeye pekee.

Kama hili taifa lingekuwa na vyombo vinavyoeleweka kuchunguza mienendo ya watu kabla ya kupewa vyeo naamini tusingefika hapa.

Tatizo vetting wanafanyiwa wasio na "connection", lakini wale wenye "connection" wanaingizwa serikalini bila kujali historia ya utendaji wao, na uadilifu wao.

Matokeo yake wanaenda kumchafua mpaka aliyewaweka kwa kujiegemeza kwake wakibanwa kwa udhaifu wao, japo naamini hayo ndio malipo ya wale wasioshughulisha akili zao, mzazi akiwa na mtoto mtukutu sifa mbaya ni zake pia.

Ushahidi wa shutuma upo, Magufuli alikuwa na shutuma nyingi mpaka za mauaji je ni kweli?
 
Kwani unahita PhD kujua ufisadi wa makamba..

Huyu rais ni mzigo kwa taifa..
Nchi za kiafrika itatuchukua muda kuondikana na umaskini.

Taifa linaongozwa kifamilia familia

We uliye na ushahidi tuambie kaiba wapi sio maneno ya kuambiwa
 
kwanini namimi nikishiba ugali nikaandika hapa JF, "Makamba mwizi" tayari ni shutuma au Makamba mwizi....
 
Kelele zimekuwa nyingi Makamba fisadi, Makamba mwizi, ndio zake hizo lakini hakuna hata ushahidi kuwa siku fulani alikula shilingi kiasi flani kwa mishe flani
 
Ni dhahiri sasa mabadiliko katika Baraza la Mawaziri hayakwepeki tena. Hii ni mara baada ya mawaziri kuanza kuitwa mbele ya KK ya NEC ili kujielekeza kuhusu malalamiko ya wananchi kuhusiana na wizara zao.

Ili kunusuru "future" ya kisiasa ya January, ni vyema sasa apelekwe wizara nyingine isiyokuwa na lawama nyingi kama hii anayoiongoza. Viatu vimekuwa vikubwa sana kwake katika kuiongoza wizara hii nyeti ya nishati.

Kwa kuwa meza zinapinduliwa kibabe, namuona Prof. Muhungo kama vile anaanza kupiga jalamba.
 
Mpuuzi at work!

Yani Makamba apelekwe wizara nyingine kwa chuki na wivu wako tu?
 
Kama unafuatilia habari za kisiasa. Hivi karibuni Makamba amekuwa akitajwa sana kwenye mitandao ya Jamii forums na Twitter kwa tuhuma mbalimbali.

Kuna wabunge pia wamemuattack directly kama wakina Luhanga Mpina na Msukuma.

Busara mara nyingi huwa ni kunyamaza ukweli ujitenge na uongo. Lakini kuna wakati inabidi kutoka na kuchukua hatua za ziada kabla mambo hayajaaminika.

Uongo ukisemwa sana hugeuka kuwa ukweli. Ni muda sasa wa Makamba kutoka na kukanusha habari hizo, na ikiwezekana kuchukua hatua za kisheria kama walivyofanya Fatma Karume na Membe dhidi ya Musiba.

Lakini pia kama yasemwayo ni kweli hebu jitafakari sana, hata kama una ukaribu sana na Rais ni vizuri ujiuzulu.

Rais Mwinyi aliwahi kujiuzulu ukweli ukafahamika na baadae akaja kuwa Rais.

Haina maana kung'ang'ania kitu kama kinazidi kuharibika.
Ni wakati uchague kati ya mawili toka ujitetee au jiuzulu.

Kukaa kimya kwa nyakati kama hizi ni kuzidi kuharibu mambo.
Jamaa ni msanii, atakanusha nini?
 
Back
Top Bottom