friendsofjeykey
Senior Member
- Aug 12, 2010
- 129
- 13
mbona kazi rahisi mpigie chadema basi mtaona atakuja kuomba msamhamakamba kashikwa pabaya na omari kimbau. Kalazimisha uchaguzi urudiwe kwenye makao makuu ya kisiwa cha mafia mpaka mpwa wake bwana omari kimbau kapita kwa kura tano huku watu zaidi ya 50 wakizuiwa kupiga kura na cha kuchekesha zaidi ni kuwa mjumbe wa kamati ya siasa naye hakuweza kupiga kura kisa? Jina lake halimo!
Huyu huyu omari kimbau ndiye aliyekuwa ana gawa pesa kama njugu hapa kisiwani na baadae akawa anatoa amri kwa polisi kukamata watu ovyo kisa ni wapinzani wake wa kisiasa.
Yufuf makamba na mama yake omari kimbau ni ndugu na sisi watu wa kisiwa hichi tunashangaa kwa nini aismtafutie huyu omari jimbo huko tanga kama alivyomtafutia january kule bumbuli?
Hivi sisi watu wa mafia tumekufanyia nini mpaka ultulipe kwa hili ulilotufanyia wewe makamba?
Taarifa ni kuwa ccm mkae mkijua kuwa jina la omari likipita sisi tunawapa jimbo hili cuf maana hata chadema hatuwaoni.
Makamba kashikwa pabaya na Omari Kimbau. Kalazimisha uchaguzi urudiwe kwenye makao makuu ya Kisiwa cha Mafia mpaka MPWA WAKE bwana OMARI KIMBAU kapita kwa kura tano huku watu zaidi ya 50 wakizuiwa kupiga kura na cha kuchekesha zaidi ni kuwa MJUMBE WA KAMATI YA SIASA naye hakuweza kupiga kura kisa? JINA LAKE HALIMO!
Huyu huyu Omari Kimbau ndiye aliyekuwa anagawa pesa kama njugu hapa kisiwani na baadae akawa anatoa amri kwa polisi kukamata watu ovyo kisa ni wapinzani wake wa kisiasa.
Yusuf Makamba na Mama yake Omari Kimbau ni ndugu na sisi watu wa Kisiwa hichi tunashangaa kwa nini aismtafutie huyu Omari jimbo huko Tanga kama alivyomtafutia January kule Bumbuli?
Hivi sisi watu wa Mafia tumekufanyia nini mpaka ultulipe kwa hili ulilotufanyia wewe Makamba?
Taarifa ni kuwa CCM mkae mkijua kuwa jina la Omari likipita sisi tunawapa jimbo hili CUF maana hata CHADEMA hatuwaoni.
Kabla ya kuwa mwanasiasa, Yusufu Makamba alikuwa msanii mtoa burudani fulani kule jeshi la wananchi. Kuchaguliwa kweke kwenye NEC ya CCM ambayo ndiyo ilifungua njia yake ya kisasa, alitumia kampeini ya kuwa nimewapa burudani kwa muda mrefu, sasa ni zamu yenu pia kunipa burudani kwa kunichagua kuwa muumbewa NEC.
Nafahamu kuwa Dada Halima (Mke wa Ayoub Kimbau) anatokea Tanga,lakini nilikuwa sifahamu kuwa ni Ndugu na Mzee Makamba.Kama habari hii ni ya kweli basi CCM sasa wanaibaka Demokrasia,maana kama sio rushwa utasikia ubabe wa namna hii wa kutaka wanayemtaka Ashinde hata kama wananchi hawamtaki.Kuna nafasi nyingi za Wabunge wa kuteuliwa,ningemshauri Mzee Mkamba ampendekeze na Omari katika nafasi hizo ili kuwapa watu wa Mafia uhuru wa kumchagua mtu (kiongozi) wanayempenda.
Omari ambaye Baba yake mzazi kanali mstaafu Ayoub Kimbau aliwahi kuwa kuwa Mbunge wa Mafia kwa kipindi cha miaka 25, (1975 - 2000)Mzee Kimbau alipata pia kumuandaa mdogo wake wa mwisho Dr.Hamis Kimbau (RIP) kuchukua nafasi hiyo.Hamis alifariki kabla ya kutimiza Azma hiymari ambaye ni Diwani wa Kijitonyama inaonyesha kuwa alishindwa ktk kura za awali,kwa kutumia uzoefu na ukaribu wake kwa Viongozi wa CCM wa Wilaya/Mkoa na Taifa walitaka uchaguzi huo urudiwe,kwa madai ya kuwepo rushwa na ukiukwaji wa taratibu nyingine za Uchaguzi.
Si malalamiko hayo tu yanayoihusu Familia ya Kimbau katika uchaguzi huu,Dada yake Omari ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Jimbo la Ubungo,Mayasa Kimbau analalamikiwa kwa kushinda kimizengwe kwenye kinyang'anyiro cha Udiwani Kata ya Makuburi,Tawi la Makoka "A".Mshindi wa Uchaguzi huo alikuwa Ndg.Justine Sangu aliyepata kura 432 akifuatiwa na Bi.Mayasa Kimbau aliyepata kura 426.lakini kwa Mshangao wa wengi katibu wa CCM wa wilaya alimtangaza Bi.Mayasa kuwa ndio mshindi.Wakazi wengi wa Tawi hilo wamechukizwa na matokeo hayo na kutishia kuwa katika Uchaguzi mkuu wa Oktoba watawapigia kura Chadema.
Kama Omar Kimbau atashinda katika kura za maoni,atakuwa amefuata nyayo za Wazazi wake kwa kuingia katika Bunge la Jamhuri ya Muungano,Mbali na Mzee Kimbau,ambaye kwa sasa ni mjumbe wa board ya AICC,Mke wa Mzee Kimbau Mama Halima Kimbau ni Mbunge wa CCM wa kuteuliwa kutoka Mkoa wa Pwani Wilaya ya Mafia.
Yule mama daktari mfanyakazi wa UN wameona hafai?
YES Mkuu NN, naona hii kansa inaenea kwa kasi..Hivi Omari kweli anaziweza siasa au anatafuta kula tu?
friendsofjeykey kwa kuwa uchaguzi haujafanyika mbona kazi iliyo mbele yenu wana Mafia ni ndogo tu ifikapo tarehe 31st October 2010 ikiwa hamtaki huyu Kimbau awe mbunge wenu. WAPENI KURA WAPINZANI