MAKAMBA ampitisha mpwae OMAR KIMBAU

Mungu akusamehe wewe unayejiita friendsof JK, ni wazi kuwa unahitaji maombi kwa mtazamo wako finyu katika karne hii ya sayansi, huyo mama mwenye digrii mbili msomi wa hali hiyo, kwa akili yako ndogo unadhani anahitaji kuvua chupi ili apewe cheo? ni msomi kuliko wanaume wote waliogombea, ana cheo kikubwa huko UN. DC wa MAFIA atampa nini? Ni wakati muafaka uamke na kujua sio kila mwanamke kwenye siasa anategemea rushwa ya ngono, najua unaongea hivyo na kumponda huyo mama na Kimbau eti tu kwa sababu huyo ajiyefoji cheti Buji, kwa jina halisi Mohamedi kashindwa hatuhitaji vihiyo yeye ni dereva akaendeshe magari huko. nasikia kaishia kuona mke wa kisiasa na siasa zenyewe haziwezi.


Mtamalizana wajamaeni!

Degree hata kumi haziwezi kuzuia mwanamke kuwa hawara! Umalaya ni hulka ya mtu na sio amesoma kiasi gani! Pia umalaya hautegemei unapewa nini!
 
Ndugu zangu natumaini hatima ya Mafia iko mikononi mwa wana Mafia, hivi kama Kimbau hafai mbona wamemchagua, na kama kutoa rushwa wote hao Kimbau na Buji walitoa rushwa ila awamu ya pili, Buji imekula kwake. Bwana haya mambo yanakwenda kwa wakati jamaa alishatesa miaka kumi kafanya nn visima visima tatizo jamaa SHULE hakuna sisi tunataka wasomi bwana ngoja muone maajabu. Muda wa kuongozwa na watoa rushwa na madreva umekwisha.......nimesikia wana Mafia wanasema akipitishwa yule mama wamepata naibu Waziri, ndiye peke yake ana vigezo wengine wote bure kabisa
 
issue ni kuwa unasema amekuwa hawara ili apewe ubunge ndio maana anasema hivi kwa vigezo alivyonavyo anahitaji kutembea na mtu ili ashinde mawazo finyu hayo AMKENI ndugu zangu
 
Ndugu zangu natumaini hatima ya Mafia iko mikononi mwa wana Mafia, hivi kama Kimbau hafai mbona wamemchagua, na kama kutoa rushwa wote hao Kimbau na Buji walitoa rushwa ila awamu ya pili, Buji imekula kwake. Bwana haya mambo yanakwenda kwa wakati jamaa alishatesa miaka kumi kafanya nn visima visima tatizo jamaa SHULE hakuna sisi tunataka wasomi bwana ngoja muone maajabu. Muda wa kuongozwa na watoa rushwa na madreva umekwisha.......nimesikia wana Mafia wanasema akipitishwa yule mama wamepata naibu Waziri, ndiye peke yake ana vigezo wengine wote bure kabisa
Kama Dr. Slaa na wala sio wale madaktari wa kutunukiwa.
 
:A S 39:Jamaa dereva wa maroli kashafulia, haya wafuasi wake kazi kwenu..... unajua watu wengine hawana dili jingine siasa ikidunda vita.... nasikia huyo mama yuko kazini anapiga mazigo wakati Buji na Kimbau wanahangaika DODOMA kubembeleza mhh kazi kwao, mimi siasa zisifagilii, mutachinjana bure
 
CCM ni msitu wa mafisadi, nawashangaa ninyi wananchi mnaong'ang'ania kuwa kwenye huo msitu wa mafisadi
 
Mafia ni utata mtupu:

Katibu wa CCM Wilaya ya Mafia mkoani Pwani, Salehe Kikweo, amelazimisha kurudiwa kwa kura katika ofisi za chama wilayani chini ya usimamizi wake mwenyewe.
Taarifa kutoka Mafia zinaeleza kwamba marudio ya uchaguzi huo yaligubikwa na mizengwe ya kila namna, ikiwapo Katibu kutangaza kurudiwa kwa uchaguzi usiku wa manane katika ofisi za wilaya kinyume cha taratibu za uchaguzi.

Ilidaiwa kuwa Kikweo alimpigia simu Katibu wa tawi la Kilindoni, Emmanuel Luvanda, Agosti 10, majira ya saa 5:00 usiku na kumtaarifu kwamba uchaguzi katika tawi hilo ungerudiwa kesho yake yaani Agosti 11, saa 4:00 asubuhi.
Taarifa zaidi zinaeleza kwamba Luvanda alijaribu kumsihi Katibu huyo kurekebisha tarehe ya uchaguzi huo mdogo ili kutoa taarifa kwa wanachama, jambo ambalo hata hivyo lilipingwa na Kikweo.
"Ndipo Luvanda akanipigia mimi kama mmoja wa wajumbe na kunitaarifu juu ya taarifa hizo...asubuhi ya jana (juzi) tukaamka kuwaambia wanachama kwamba kuna uchaguzi, walioweza kujitokeza walikuja tawini kwa ajili ya kupiga kura," alisema mjumbe wa siasa wa tawi la Kilindoni, Ahmad Kubenea.

Kubenea alifafanua kuwa Kikweo alitaka uchaguzi huo usimamiwe na kamati ya siasa ambayo ilikataa jukumu hilo ndipo aliamua kuusimamia kwa kuanza kuita majina ya wanachama ambao walianza kupigakura.
"Zoezi limekwenda lakini baada ya muda mfupi vijana wakabaini kwamba kuna watu wanaweka kura mbilimbili wakatoa taarifa kwa Katibu (Kikweo) ambaye aliamua kuchukua ndoo ya kura na kuichoma moto...akatangaza tena kwamba uchaguzi utafanyika wilayani saa 8:30 mchana, huko kura zilipigwa hadi saa 5:00 usiku," alisema.
Hata hivyo, alisema baadhi ya wanachama walizuiwa kushiriki zoezi hilo kwa madai kwamba majina yao hayapo kwenye orodha ya daftari la wapigakura.

Taarifa zaidi kutoka Mafia, zinaeleza kwamba mbunge aliyemaliza muda wake, Abdulkarim Shah, juzi hiyo hiyo alikata rufaa kulalamikia mchezo huo na kupeleka nakala yake kwa viongozi wakuu wa chama hicho.
Katibu wa CCM tawi la Kilindoni, Luvanda, alithibitisha kuwepo kwa tafrani hiyo na kueleza kwamba majira ya saa 4:30 usiku wanachama walizuiwa kupigakura.
Source: IPP Media.
 
Back
Top Bottom