Elections 2010 Makamba akiri Dr Slaa ni tishio kwa Kikwete na CCM

Inawezekana Makamba alitamka maneno hayo "DR.Slaa ni tishio kwa Kikwete" bila kujijua; si unajua tena mgosi mara nyingi anajisahau na analopoka lopoka hovyo!!
 
Hongera sana Makamba, kwenye ukweli uwongo hujitenga. Watanzania wekeni kumbukumbu ya maneno ya makamba. Dr Slaa na Chadema yatumieni kwa faida. Makamba amekiri kwa kinywa chake kwamba Dr. Slaa ni tishio kwa Kikwete. Dr Slaa yuko juu kuliko Kikwete, ni kama anga ilivyo juu kuliko nchi kavu. Makamba alishawahi kusema kuwa Kikwete ni maarufu kuliko CCM. Kwa kuwa Kikwete ni maarufu kuliko CCM, Makamba anakiri kuwa Dr. Slaa yupo juu kuliko Kikwete na CCM. Kwa hiyo Dr. Slaa ni tishio kwa Kikwete na CCM yote kwa sababu Kikwete ni maarufu kuliko CCM.
Tatizo ni kwamba Watanzania wengi hawatafikiria hivyo! wewe umetumia shule mkuu wangu kuchambua pumba hizi lakini kwa Wadanganyika itakuwa Lipumba ni mbora kuliko Dr.Slaa ili kuzigawa kura za Upinzani..

CCM wenyewe hawana taabu na kura zao hata kidogo ndio maana umeona wasomi kina Mtanzania wanagombea ubunge kwa tiketi ya CCM pamoja na mabaya yote wanayoyazungumza humu. Tena wapo wengi ajabu wananchma wa JF wamejiandikisha kugombea Udiwani na Ubunge kwa tiketi ya CCM..
 
Lakini kukiri kwake kuko sahihi, Kikwete huwezi kumlinganisha na Slaa, kielimu hawaendani, kiutendaji hawaendani, nilishangaa sana pale makamba aliposema eti kikwete ana la kujivunia wakati Slaa ahana hata alichofanya, sijui huyu mtu kama ana kumbukumbu kichwani mwake, maana kumbukumbu zinaonyesha kwamba Slaa ndiye aliyekuwa anaongoza kuchangia bungeni, ndiye aliyekuwa anaiwajibisha serikali ya CCM, so ukija kiutendaji unaweza kukuta Kikwete alikuwa anacopy na kupaste hoja za Slaa na bahati mbaya hakuna alichofanyia kazi---------mimi naona katika 5yrs ya utawala wa kikwete Slaa amepaform zaidi kuliko hata huyo mkuu wa kaya, nafikiri Makamba anaelekea kwenye no thinking limit, naafikiri na uzee nao unaelekea kutawala fikra na mwili and at the end anaelekea kwenye EXTINCTION, am very sorry for that.
 
Jana niliona TBC walimpa airtime ya kutosha kumwaga upupu wake, kama hawamhofii kelele za nini?

Ndo kawaida yao hao, ila hiyo CD ya zamani itakpokuja kurudiwa itakuwa ni baada ya miaka mitano ijayo, that means, amekubali kuwa mwaka huu n Slaa tu, yeye na ccm yake waende Bumbuli kumsaidia mwanae kuiba kura, tukae mghoshi makamba
 
Tatizo ni kwamba Watanzania wengi hawatafikiria hivyo! wewe umetumia shule mkuu wangu kuchambua pumba hizi lakini kwa Wadanganyika itakuwa Lipumba ni mbora kuliko Dr.Slaa ili kuzigawa kura za Upinzani..

CCM wenyewe hawana taabu na kura zao hata kidogo ndio maana umeona wasomi kina Mtanzania wanagombea ubunge kwa tiketi ya CCM pamoja na mabaya yote wanayoyazungumza humu. Tena wapo wengi ajabu wananchma wa JF wamejiandikisha kugombea Udiwani na Ubunge kwa tiketi ya CCM..

Mkandara;
Mkuu haya umeyatoa wapi? ni yupi mwanaJF uliyemwona anagombea ubunge CCM? Sidhani kama hii lugha ni njema katika jamvi hili hata kidogo, na kama wapo wewe waache kwani sisi hatuishi kwa hisia, bali tunaongozwa na mitima ya mioyo yetu

Mkandara;tia akili ndugu yangu hiki ni kipindi cha kutafakari sana, kujitenga na wale wote wasaliti wa Taifa letu.
 
kwa nini anakuwa subject kama hawamuhofii!!?

Hawa CCM hawataki ku-admit kuwa Dr. Slaa ni tishio kwao. Mi naona hayo ni maneno ya ccm tu yanayotokana na wasiwasi walionao juu u upizani wa safari hii. Pia wanakumbuka madahmbi mengi yaliyofanywa na chama chao (CCM) hivo wanatafuta njia ya kukabiliana nayo.

Waache wananchi tufanye maamuzi... Ni wakati wa kuthamini kura zetu na si vinginevyo
 
MAKAMBA = CHEMICAL ALI a.k.a vuvuzela

Mkuu Jibaba Bonge, Kumlinganisha Makamba na Chemical Ali si sawa na hawafanani kwa lolote.

Hayo ndo madhara ya kupeana vyeo kishkaji kwani, ktk Makatibu wakuu wa CCM wote waliopita Mbumbumbu ni yeye tu. Je, anaweza kuingia hata robo ya Philip Mangulla? Hilo la Uvuvuzela ndo sawia kabisa.
 
Wekeni audio au video hapa kwa authenticity kama mnaweza, waandishi wenyewe hawaeleweki na hawako coherent. Bila hivyo itakuwa habari ya muwamba ngoma huvutia kwake, hyperboles za hyperboles.

Unakuta story moja, event moja, coverages mbili tofauti katika magazeti mawili tofauti.

Wengine wanakwambia Makamba kasema CCM haimuhofii Dr Slaa inamuhofia Lipumba, wengine wanasema Dr. Slaa anahofiwa na Kikwete, ili mradi vurugu mechi hata ukisoma hakuna mtiririko unaoeleweka.
 
Mkandara;
Mkuu haya umeyatoa wapi? ni yupi mwanaJF uliyemwona anagombea ubunge CCM? Sidhani kama hii lugha ni njema katika jamvi hili hata kidogo, na kama wapo wewe waache kwani sisi hatuishi kwa hisia, bali tunaongozwa na mitima ya mioyo yetu

Mkandara;tia akili ndugu yangu hiki ni kipindi cha kutafakari sana, kujitenga na wale wote wasaliti wa Taifa letu.
Sasa wewe unamtisha ama? Ni vema kutoa maoni yako juu ya ukweli. Kuna wanaJF kadhaa wameingia ulingoni kugombea nafasi za ubunge na udiwani kwa tiketi ya CCM. Zaidi kuna mmoja anamalizia mikutano yake ya kutafuta wadhamini katika kugombea urais kwa tiketi ya chama chingine.
 
Sasa wewe unamtisha ama? Ni vema kutoa maoni yako juu ya ukweli. Kuna wanaJF kadhaa wameingia ulingoni kugombea nafasi za ubunge na udiwani kwa tiketi ya CCM. Zaidi kuna mmoja anamalizia mikutano yake ya kutafuta wadhamini katika kugombea urais kwa tiketi ya chama chingine.

Kibunango mbona unasema zaidi kuna mmoja anamalizia mikutano ya kutafuta wadhamini katika kugombea urais? Mimi niliambiwa kuwa Ridhwani huwa anatembelea humu jf na kama ni hivyo basi Jk pia anatembelea kwani hawa ni wamoja; hivyo basi tutakuwa na wagombea urais wawili kama sio watatu kutoka janvini!! Not to mention that you Kibunango and Malaria are Muungwana's listening posts hapa janvini!
 
Mkandara;
Mkuu haya umeyatoa wapi? ni yupi mwanaJF uliyemwona anagombea ubunge CCM? Sidhani kama hii lugha ni njema katika jamvi hili hata kidogo, na kama wapo wewe waache kwani sisi hatuishi kwa hisia, bali tunaongozwa na mitima ya mioyo yetu

Mkandara;tia akili ndugu yangu hiki ni kipindi cha kutafakari sana, kujitenga na wale wote wasaliti wa Taifa letu.

Sasa wewe unamtisha ama? Ni vema kutoa maoni yako juu ya ukweli. Kuna wanaJF kadhaa wameingia ulingoni kugombea nafasi za ubunge na udiwani kwa tiketi ya CCM. Zaidi kuna mmoja anamalizia mikutano yake ya kutafuta wadhamini katika kugombea urais kwa tiketi ya chama chingine.

Kibunango mbona unasema zaidi kuna mmoja anamalizia mikutano ya kutafuta wadhamini katika kugombea urais? Mimi niliambiwa kuwa Ridhwani huwa anatembelea humu jf na kama ni hivyo basi Jk pia anatembelea kwani hawa ni wamoja; hivyo basi tutakuwa na wagombea urais wawili kama sio watatu kutoka janvini!! Not to mention that you Kibunango and Malaria are Muungwana's listening posts hapa janvini!
Mkuu Bulesi, hebu msome huyo Isaya, yaani yeye ameshindwa kabisa kujua kwamba kuna baadhi ya wanaJF wapo kwenye kutafuta nafasi za uwakilishi. Yeye JF kwake ni huo moto na mabua na magugu mengine katika kugombea urais na ubunge,

Sina hakika kama JK anapita hapa, na wala mimi sio msemaji wa JK hali kadhalika Ridhwan, kama wapo hapa, hapana shaka kwamba watajibu umbumbu wa Isaya. Manake jamaa anaweza kuwa ni kituko cha mwezi huu.
 
Makamba siyo mtu wa kumnukuu kwa vile amejaa wivu na chuki,yeye tangu azaliwe hajawahi kupata nafasi yoyote kwa kuchaguliwa na watu , yeye siku zote amekuwa akipata nafasi za kuteuliwa na wakubwa kwa vile ni bingwa wa kuwalamba miguu wakubwa, hivyo akiona mtu anayependwa na watu roho inamuuma sana. Hivi kumlinganisha Makamba na Dr Slaa ni sawa na kulinganisha panya buku na tembo,YM yuko chini saaaana, ndiyo maana matamshi yake ni ya kijiweni tu.

Kweli tupu umenena
 
Kalinganisha vema kabisa...Moto wa mabua ni very efficient....haraka na kazi kubwa kwa mda mdogo...ndivyo JK atakvyong'olewa haraka na kwa uifanisi mkubwa....
Hivi Makamba na akili kweli? Anlinganisha Mrema na Dr. Slaa! Hivi kweli hawa IQ zao zinaweza linganishwa ? Mrema ilikuwa misifa na njaa iliyomtuma lakini Dr. Slaa yy ni uzalendo na mapenzi mema kwa nchi ndio vinamsukuma.

Makamba ni mtu muflisi asiyekuwa na chembe ya "intellectual knowledge" (hana uwezo wa kujenga hoja). Ni kada aliyozoea kuropoka, kuzomea, kuzonga, kuandama na kubeza tu. Hata aliyemteua kushika wadhifa huo katika Chama analijua vizuri. Huwezi kumlinganisha Makamba na Kolimba au Mangula. Lakini aliyemteua anajua lengo lake la kumweka kada dhaifu kama yeye katika wadhifa mzito kama ule.
 
Damn! there is no love for Luteni Makamba in this board. The old comrade knows his politics more than a lot of wanasiasa hapa nyumbani. Slaa and em are political neophytes to Luteni by far. I think he is more calculated than folks here gives him credits. Anyways, November sio mbali. Lets wait and see--
 
slaa_199.jpg



UTEUZI wa Dk. Willibrod Slaa kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano, "unamweka pabaya" Rais Jakaya Kikwete ambaye anatetea nafasi hiyo kwa muhula wa pili, MwanaHALISI limeelezwa.
"Huyu ni mtu makini sana. Haongei bila utafiti na takwimu sahihi. Atatusumbua sana katika uchaguzi huu," amekiri mmoja wa viongozi wastaafu wa ngazi ya juu serikalini.
Amesema, "Hawa watu wamejipanga. Huyu ni mtu anayeaminika. Anaheshimika. Jamii inamfahamu. Anaweza kutoa upinzani; tena si upinzani mdogo."
Dk. Slaa ameteuliwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuwa mgombea urais. Atathibitshwa na mkutano mkuu wa chama hicho mapema mwezi ujao.
Woga uliopo ni kwamba pamoja na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwepo kwa miaka mingi na kuwa na uzoefu wa kampeni, Dk. Slaa ana uwezo mkubwa wa kujenga hoja kwa takwimu ambazo CCM haiwezi kuzijibu.


"Hofu yetu ni weledi wa Dk. Slaa katika kusimamia mambo kwa umakini. Haya ni mambo ambayo yanampa nafasi ya kipekee ya kuaminika na kuchaguliwa na wananchi," ameeleza kiongozi mstaafu kutoka serikali ya CCM. Kiongozi mstaafu ambaye ametaka jina lake lisitajwe amesema kuna uwezekano mkubwa wa Dk. Slaa kumfunika Kikwete mara baada ya kampeni kuanza.


"Huyu bwana hajawahi kugombea nafasi hii. Ni tofauti na wale ambao wameshagombea mara kadhaa na kushindwa ambao sasa tayari wamekosa mvuto. Nasema huu ni mkakati mzuri kwa Chadema, kwani wengi walidhani watachukua mgombea kutoka CCM," ameeleza.
Alipoulizwa amepokeaje uamuzi wa Chadema kumsimamisha Dk. Slaa, mjumbe wa Kamati Kuu (CC) ya CCM alijibu haraka, "Ni uamuzi mzuri.



Kwa kweli ataipatia heshima kubwa Chadema. Nadhani wamesimamisha mtu mwafaka kwa chama na wananchi kwa jumla," alisisitiza.


Hata hivyo, kiongozi huyo mstaafu alisema, "…lakini nasi katika CCM tumejipanga maana tunamgombea anayekubalika."
Kwa mujibu wa mahojiano ya gazeti hili na wananchi na viongozi mbalimbali wa vyama na serikali, Dk. Slaa ataibukia kwenye hoja za maendeleo na kushindwa kwa serikali ya Kikwete kutimiza matarajio ya wananchi.
Kwa mfano, umekuwa utamaduni wa CCM kuwaambia wananchi juu ya kile inachoita maendeleo yaliyofikiwa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.


Hakika orodha yake huwa ndefu, lakini hakuna jitihada za ndani ya CCM za kuhoji juu ya mafanikio hayo.



Tangu Kikwete aingie madarakani, miaka mitano iliyopita, hali ya uwekezaji nchini imezorota; wawekezaji wengi wamekimbia na Tanzania iliyokuwa inasifika kwa kuvutia uwekezaji imeporomoka katika viwango vya kimataifa vya uwekezaji.
Suala hili linaeleweka vema kwa Dk. Slaa na ana uwezo mkubwa wa kulifafanua kwa wananchi - hawa wa vijijini mpaka wakalielewa.
Mwaka 2005, kabla ya serikali ya rais mstaafu Benjamin Mkapa haijaondoka madarakani, Tanzania ilikuwa nchi ya pili nyuma ya Afrika Kusini, katika ukanda wa Afrika Mashariki, Kati na Kusini kwa kuvutia wawekezaji.
Lakini leo, Tanzania imeporomoka kutoka nchi ya pili katika ukanda huo, hadi kuwa nchi ya pili Afrika Mashariki.
"Mambo yote haya Dk. Slaa anayafahamu na kwa hakika ataweza kuyaibua wakati wa kampeni, jambo ambalo litaipa CCM wakati mgumu," taarifa zinaeleza.


Suala la ujenzi holela wa shule za msingi na sekondari - hasa za kata - limetajwa na viongozi wengi waliohojiwa kuwa litamletea matatizo Kikwete wakati wa kampeni.
Wakati CCM itakuja na takwimu za vyumba vya madarasa, Dk. Slaa atakuja na takwimu zinazoonyesha kuwa madarasa hayo ni matundu tu; hayana walimu wala vitabu vya kufundishia.
Hali ya shule ambazo CCM inajisifia zimeelezwa na mmoja wa viongozi serikalini kuwa "…si lolote. Ni magenge ya kukusanyia watoto wa masikini. Kule hakuna vitabu, hakuna walimu… pamekuwa kama madanguro ya kutilia mimba watoto."
Karata ya Kikwete itakwama pia juu ya masuala yanayohusu wazee na wenye ulemavu.


"Serikali imewatupa mkono. Karibu hospitali zote za serikali hazina dawa. Wajawazito wanapata shida, hata kama wamesamehewa gharama za matibabu, lakini hakuna dawa wala wahudumu."
Hizi zote ni silaha za kisiasa za Dk. Slaa ambaye ni mjuzi wa kujieleza, kufafanua na kuchambua mazingira na hali za wananchi.
Kwa mara ya kwanza upinzani umepata mmoja wa weledi katika hoja za ufisadi. Ni Dk. Slaa ambaye miaka mitatu iliyopita alitoa hadharani orodha ya watuhumiwa 11 wa ufisadi nchini.
Bila woga wala aibu, kiongozi huyo wa upinzani alisema anayepinga orodha hiyo ampeleke mahakamani, lakini hakuna aliyethubutu kufanya hivyo.
Safari hii Dk. Slaa amepata uwanja mpana. Hapa ndipo atafafanua kwa wananchi, wizi kuhusu kampuni ya Kagoga, Meremeta, Deep Green na miradi mingine feki iliyotumiwa kukwapua mabilioni ya shilingi kutoka Benki Kuu (BoT) na hazina.
"Hapa CCM iko taabani. Njia pekee itakuwa kukimbilia kuiba kura. Lakini hilo nalo si jambo salama kwa kuwa ndani ya chama wenyewe wamegawanyika; wanaibiana kura," ameeleza Filbert Kisungu mkazi wa Temeke Yombo, Dar es Salaam.
Baadhi ya viongozi wa ngazi ya juu katika CCM wamenukuliwa wakisema wizi wa kura unaweza kuitumbukiza Tanzania katika machafuko kama ilivyokuwa kwa Kenya.


Mmoja wao amekaririwa akisema, tena kwa sauti ya juu, "Wengine hatutakubali hilo. Hatutakubali kuishi nje ya nchi kwa faida ya wachache," akimaanisha vita vinaweza kuzuka na wengine kulazimika kukimbilia nje ya nchi.
Hoja nyingine kuu ambayo itakuwa ya msaada kwa Dk. Slaa ni kupungua au kukosekana kwa nidhamu katika utumishi wa umma.
"Hofu ya kuwajibika imeisha, ndiyo maana makusanyo ya kodi yamepungua kwa kiwango cha kutisha," ameeleza mmoja wa walioomba ubunge kupitia CCM na ambaye anaonyesha anaweza kuhama chama hicho iwapo ataenguliwa kwenye kinyang'anyiro cha sasa.
Mfumoko wa bei utakuwa mzigo mwingine katika kampeni za Kikwete. Kabla utawala wa Mkapa kuondoka madarakani, mfumuko wa bei ulishuka hadi kufikia asilimia saba, lakini leo umepanda hadi asilimia 14.
Mara baada ya Dk. Slaa kutangazwa kuwa mgombea urais, gazeti la kila siku la Mtanzania linalomilikiwa na Rostam Aziz, lilihusisha uteuzi huo na Kanisa Katoliki.
Gazeti hilo likiripoti taarifa hiyo lilisema kwamba Dk. Slaa amefunga mkataba na Kanisa hilo ili kumfanya kuwa rais wa jamhuri kwa faida yake binafsi. Tayari uongozi wa kanisa umekana madai hayo.
Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba alipoulizwa iwapo Dk. Slaa ni mgombea makini wa urais na kwamna anaweza kumtoa jasho Rais Kikwete alijibu haraka kuwa na chama chake kna mgombea makini.


Makamba alisema, "Hayo ni matusi. Kwangu mini Dk. Slaa siyo makini. Tutakutana kwenye kampeni. Labda ni makini kwako."
Naye Waziri Mkuu mstaafu Frederick Sumaye alipopigiwa simu na kuulizwa anamwonaje mgombea wa Chadema alisema anamfahamu na kwamba "anaweza kushindanishwa" na rais Kikwete.
Alisema kampeni "zinaweza kuwa nzuri." Alikataa kufafanua vipi.


Source: Mwanahalisi


Mimi nimeshanunua BOX langu la POP CORN.....The greatest movie is about to start....
 
Back
Top Bottom