Makamba akiri Dr Slaa ni tishio kwa Kikwete na CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Makamba akiri Dr Slaa ni tishio kwa Kikwete na CCM

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Luteni, Jul 30, 2010.

 1. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #1
  Jul 30, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  "Dk. Slaa si tishio kwa CCM ila ni tishio kwa mtu binafsi…hawezi kuwa tishio kwa chama. Nani alikuwa maarufu kama Mrema. "Santuri mpya ikitoka itachezwa katika nyumba mbalimbali lakini baada ya muda watarudia ya zamani," alisema Makamba.

  Dk. Slaa ni moto wa mabua ambao huzimika baada ya dakika tano kama alivyozimika Mrema. Mtu ambaye tunamuogopa…tunayeweza kusema kuwa ni tishio ni Lipumba, maana yeye alikuwa wa pili katika uchaguzi uliopita," alisema Makamba.

  Wadadisi wa mambo wanaelezea hatua ya Makamba kulazimika kumuweka Lipumba juu ya Dk. Slaa, hasa wakati huu ambapo mgombea huyo wa CHADEMA anaonyesha dalili za kuungwa mkono, ni jitihada tu za chama hicho kujaribu kumshambulia yule wanayemhofia kuwa na nguvu zaidi katika kipindi hiki.
   
 2. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #2
  Jul 30, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba amenukuliwa na vyombo vya habari kwamba Mgombea urais wa Chadema, Dr Wilbroad Slaa ni kama santuri (yaani record ya muziki) mpya tu ambayo so muda itakuja kuchakaa.

  Kiongozi huyu msanii na propagandist mkubwa wa chama tawala ambaye kwake kusema yaliyo ya kweli ni mwiko anapaswa atambue kwamba ni bora azungumzie santuri ambayo tayari imeshachakaa – na siyo kujifanya mtabiri wa santuri itakayochakaa. Hataki kutambua kwamba santuri ambayo tayari imeshachakaa ni chama chake -- CCM – baada ya kukaa karibu miaka 50 madarakani.

  Halafu kuchakaa kwake ni kuibaya sana kwani kumezuka unyan’gau wa hali ya juu ndani ya viongozi wake – kama vile tunavyoshuhudia hivi sasa wanavyogombania milo – hakuna tofauti na alivyokuwa akisema Mwl Nyerere kwamba ubepari ni unyama tu.

  Wachunguzi wa mambo wanasema polepole CCM inajimaliza na huenda katika uchaguzi ujao (2015) wanaowania uongozi katika CCM wakatoleana bastola katika vikao au/na kujifyatulia risasi. Dalili zinaonekana kwani viongozi wakuu wa chama chenyewe hawawezi kujirekebisha au hata kujikemea kwa sababu kila mmoja wao yumo katika dimbwi la rushwa.

  Hivi sasa wanatumia Takukuru kama onyesho kwa wananchi kwamba wanajirekebisha – mpango ambao ni kiini macho kwani taasisi hiyo imeingiliwa kisiasa na mtandao mmoja wa chama hicho.

  Na kwa upande wake Takukuru imejikuta haina uhuru kamili katika mpango huu – na mfano ni namna afisa wake mmoja wa wa mkoa wa Kilimanjaro alivyoteremshwa cheo na kuhamishwa kwa sababu tu alimtia mbaroni DC mmoja kwa tuhuma za kugawa rushwa. Yale yale ya kulindana!

  Kwa kifupi Makamba anapaswa kuangalia uchakavu mkubwa wa chama chake kabla ya kusemea chama kingine ambacho wananchi wanakiona kama ni mkombozi mkubwa kwao kutokana na machafu yanayoendelea katika CCM.


   
 3. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #3
  Jul 30, 2010
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,641
  Likes Received: 21,852
  Trophy Points: 280
  Jana niliona TBC walimpa airtime ya kutosha kumwaga upupu wake, kama hawamhofii kelele za nini?
   
 4. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #4
  Jul 30, 2010
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Chakujiuliza ni kama ameshaweza kufikiria athari zinazoweza kuletwa na moto wa mabua, shambani au kwenye makazi ya watu. Lakini kama walivyo wabinafsi wengi, huchelewi kukuta anafikiria mabua ya kwenye bustani yake pekee na kusahau kwamba moto huo huweza kuruka shamba hadi shamba, kitalo hadi kitalo na hata kufikia sehemu zenye mazao yaliyostawi na kuyateketeza pia!!
   
 5. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #5
  Jul 30, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  CCM sasa inapumua kwa nguvu ya vyombo vya dola tu -- pasipo hivyo ni kwishnei. Itafika mahala hata hivyo vyombo vya dola vitashindwa kukisanifu chama hicho. Mfano wa huyo DC ni onyesho tosha la kushindwa kwa Takukuru kuisanifu CCM.
   
 6. M

  Mutu JF-Expert Member

  #6
  Jul 30, 2010
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  kwa nini anakuwa subject kama hawamuhofii!!?
   
 7. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #7
  Jul 30, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Umenifurahisha sana CCM ilivyo sasa ni sawa na mtu nayepumua kwa msaada wa mashine maalum ya oxygen ikiondolewa tu hatunaye.

  Kama ulivyosema CCM bila vyombo vya dola hakuna kitu hawana cha kuwaambia wananchi uongo wote wamemaliza.
   
 8. kilemi

  kilemi JF-Expert Member

  #8
  Jul 30, 2010
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 520
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kwani waweza kuunguza gogo bila kuwasha mabua kwanza?
   
 9. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #9
  Jul 30, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Umenifurahisha sana CCM ilivyo sasa ni sawa na mtu nayepumua kwa msaada wa mashine maalum ya oxygen ikiondolewa tu hatunaye.

  Kama ulivyosema CCM bila vyombo vya dola hakuna kitu hawana cha kuwaambia wananchi uongo wote wamemaliza.
   
 10. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #10
  Jul 30, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Huyo mtu binafsi anayetishiwa na Slaa ni nani?
   
 11. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #11
  Jul 30, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  No wonder MS,

  Tunajua unavyokonda kama mnazi kwa mapenzi yako kwa JKM na CCM.
   
 12. J

  Jibaba Bonge JF-Expert Member

  #12
  Jul 30, 2010
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 1,224
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  MAKAMBA = CHEMICAL ALI a.k.a vuvuzela
   
 13. Iza

  Iza JF-Expert Member

  #13
  Jul 30, 2010
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,848
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  ..Wanainama Wanainuka Wanaona Haya Haoooooooooo..!!
  Kivumbi baada ya Oktoba 31...
   
 14. L

  Lubaluka JF-Expert Member

  #14
  Jul 30, 2010
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 496
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Always " MIX WITH YOURS "
   
 15. TzPride

  TzPride JF-Expert Member

  #15
  Jul 30, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 2,420
  Likes Received: 392
  Trophy Points: 180
  Kalinganisha vema kabisa...Moto wa mabua ni very efficient....haraka na kazi kubwa kwa mda mdogo...ndivyo JK atakvyong'olewa haraka na kwa uifanisi mkubwa....
  Hivi Makamba na akili kweli? Anlinganisha Mrema na Dr. Slaa! Hivi kweli hawa IQ zao zinaweza linganishwa ? Mrema ilikuwa misifa na njaa iliyomtuma lakini Dr. Slaa yy ni uzalendo na mapenzi mema kwa nchi ndio vinamsukuma.
   
 16. O

  OgwaluMapesa JF-Expert Member

  #16
  Jul 30, 2010
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 10,948
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  yani ukutaka kujua makamba ana akili ndogo yani proffesor wake wa siasa ni mrema
   
 17. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #17
  Jul 30, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,932
  Likes Received: 2,084
  Trophy Points: 280
  Bora moto wa mabua unaoivisha chakula kuliko ule wa nini sijui unaounguza chakula. Moto ni moto tu ilimradi kuna fuel kiasi gani, yaani, mabua - Dr. Slaa ni sawa na mabua millions na JK ni fungu moja la mkaa!!!!! Lipumba ni moto wa pumba - unafaa kuchomea viazi tu!!
   
 18. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #18
  Jul 30, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Wananchi wa bumbuli kama Dr. Slaa ni moto wa mabua basi kwa mantiki hiyo januari makamba ni moto wa karatasi, kwani januari hajawahi kuwa hata wa tatu
   
 19. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #19
  Jul 30, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Kwani Makamba ana Elimu gani, usije kuta ni mwalimu wa UPE aliyekimbilia ukamisaa wa jeshi na kuambulia uluteni.
   
 20. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #20
  Jul 30, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,548
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Makamba siyo mtu wa kumnukuu kwa vile amejaa wivu na chuki,yeye tangu azaliwe hajawahi kupata nafasi yoyote kwa kuchaguliwa na watu , yeye siku zote amekuwa akipata nafasi za kuteuliwa na wakubwa kwa vile ni bingwa wa kuwalamba miguu wakubwa, hivyo akiona mtu anayependwa na watu roho inamuuma sana. Hivi kumlinganisha Makamba na Dr Slaa ni sawa na kulinganisha panya buku na tembo,YM yuko chini saaaana, ndiyo maana matamshi yake ni ya kijiweni tu.
   
Loading...