Makamba achochea wagombea wa CCM waliobwagwa Ubunge wakatae matokeo mahakamani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Makamba achochea wagombea wa CCM waliobwagwa Ubunge wakatae matokeo mahakamani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nickname, Nov 20, 2010.

 1. nickname

  nickname JF-Expert Member

  #1
  Nov 20, 2010
  Joined: Dec 20, 2009
  Messages: 516
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  [​IMG]
  Yusuf Makamba
  Baada ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupoteza majimbo 53 ya ubunge katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 31, mwaka huu, Katibu Mkuu wake, Yusuf Makamba sasa ameamua kila mgombea ubunge na udiwani aliyeshindwa afungue kesi ya kupinga matokeo.


  Hatua hii inayotafsiriwa kama kukutaa kutambua matokeo ya uchaguzi wa wabunge na madiwani, inathibitisha mtikisiko ndani ya chama hicho na wagombea wote walioshindwa wa ubunge na udiwani wametakiwa kufungua kesi mahakamani katika kipindi cha siku 30 kuanzia kutangazwa kwa matokeo hayo.

  NIPASHE ina taarifa za barua ya siri iliyoandikwa na Makamba kwenda kwa Makatibu wote wa CCM nchini ikiwataka wagombea wote wa CCM walioshindwa uchaguzi, kufungua kesi mahakamani.

  Barua hiyo ambayo NIPASHE imeiona yenye kumbukumbu namba CCM/OND/636/VOL.11/122 iliyoandikwa Novemba 9, 2010, ikiwa imesainiwa na Makamba na inaonyesha kuwa ilipokewa na makatibu wa CCM wa mikoa.

  Katika barua hiyo, Makamba anawataka wagombea wa ubunge kufungua kesi katika Mahakama Kuu ya Tanzania huku wagombea udiwani walioangushwa kwenda kufungua kesi katika mahakama za mahakimu wakazi ndani ya siku 30, tangu ulipofanyika uchaguzi huo Oktoba 31, mwaka huu.

  Makamba anawaagiza makatibu wa CCM wa mikoa kwa kushirikiana na makatibu wa CCM wa wilaya na kata kuwasaidia wagombea hao walioshindwa kwenye uchaguzi kuandaa hoja za malalamiko na vielelezo kwa ajili ya kupeleka mahakamani.

  Aidha, Makamba ameagiza kuwa baada ya hoja hizo za malalamiko kukamilika zipelekwe katika ofisi ndogo ya CCM jijini Dar es Salaam au kuwasiliana moja kwa moja kwa mawakili ambao ni makada wa CCM ili kuandaa hati za malalamiko ndani ya muda huo.
  "Kwa barua hii, mshirikiane na makatibu wa CCM wilaya/kata na wagombea husika kuandaa hoja za malalamiko na vielelezo/ushahidi na kuwasilisha CCM ofisi ndogo Dar es Salaam au kuwasiliana na mawakili ambao ni makada wetu moja kwa moja ili kuandaa hati za malalamiko ndani ya muda huo," ilisema sehemu ya barua hiyo ya Makamba.
  Katika barua hizo, Makamba pia amewaahidi wagombea wasiokuwa na uwezo wa kifedha kuwa chama kitachangia gharama za mawakili ili kuwasaidia kufanikisha azma hiyo.
  "Chama Cha Mapinduzi Makao Makuu kitachangia gharama za mawakili kwa wagombea ambao hawana uwezo wa kifedha," ilisema sehemu ya barua hiyo.

  Katibu huyo wa CCM Taifa anahitimisha barua yake kwa kuwataka makatibu wa CCM wa mikoa kusimamia ipasavyo maagizo hayo ili kuhakikisha kuwa kesi hizo zinafunguliwa mahakamani.

  Akizungumzia barua hiyo,Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Wilaya ya Mbeya Mjini, John Mwambigija, alisema shinikizo hilo la CCM kwa wagombea wake kukimbilia mahakamani linaonyesha kuwa chama hicho kinataka ushindi wa nguvu badala ya kuridhika na maamuzi ya wananchi.

  Alisema kwa kuwa chama hicho kina fedha nyingi, kinataka kuzitumia kuzima demokrasia, na ndiyo sababu kubwa ya kuwataka wagombea wake walioangushwa kwenye uchaguzi kukimbilia mahakamani huku kikiwaahidi kuwasaidia gharama za kuendesha kesi.
  Uchunguzi umebainisha kuwa baada ya agizo hilo kuwafikia mmoja wa viongozi wa CCM wa Wilaya ya Mbeya Mjini, ameonekana akiwaita wagombea wa udiwani walioshindwa akiwataka wakafungue kesi mahakamani....

  Source : NIPASHE 20th Novemba 2010
   
 2. nickname

  nickname JF-Expert Member

  #2
  Nov 20, 2010
  Joined: Dec 20, 2009
  Messages: 516
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  Atakayeleta vurugu zote na machafuko nchini ni Makamba,Kikwete HAFAI bora amuondoshe Makamba.

  Ndio tatizo la kuweka wanajeshi kuendesha demokrasia,kila wakati maamuzi yake ni kutumia nguvu tu :angry:
   
 3. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #3
  Nov 20, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Walishasema kwa gharama yeyote ile ni lazma wanyakue ushindi.
  So sishangai.
   
 4. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #4
  Nov 20, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Me nadhani huyu mzee sasa nae anazeeka vibaya sasa yeye haangalii hali ya kisiasa inavyokwenda sasa hajaona kwanini Wao CCM walipoteza majimbo muhimu na kutafakari ilikuwa nini ikawa hivyo na kuwaeleza wana CCM.

  Yeye Hajajiuliza kwaniniCHADEMA walitoka Bungeni na kumwacha Rais means wali susia hotuba ya JK, Hivi ni vitu vya kujiuliza kwanza kwa Katibu wa CCM Taifa yeye ni kama vile sasa anatakaenda kuchoche machafuko, Hakuyaona yaliyotokea Mwanza,Mbeya ,Iringa, Arusha bado anatangaza kuwa wakapinge matokeo Mfano mzuri tu najaribu kwakumbusha na jinsi navyo fuatilia siasa za bongo tokea Mfumo wa vyama vingi uanzishwe ni lini CCM ilisha shinda kwa kura za wananchi Jimbo la Arusha Mjini na siku zote huchukua jimbo mahakamani. Which means wananchi hawawataki CCM katika jimbo hilo, Nao CCM ni ving'ang'anizi hawakai na kujiuliza why?& where do they go wrong, Tokea lini kuna kuwa na siasa za mabavu maamuzi ya wananchi wanayazarau na kuwanayang'anya haki zao za kupiga kura, huu ni uchu wa madaraka au kuipotosha Democrasia? Serikali gani ambayo haitaki heshimu maamuzi ya wananchi wake?

  Makamba nadhani anajisahau sasa NEC ililalamikiwa na vyama vya upinzani kwa kuwa na mikakati mibovu ya kuhesabu kura, na mapungufu mengi tuu na vyombo vya usimamizi vilivyokuja navyo vilikosoa NEC still makamba anawambi wabunge walio shindwa waende mahakamani yeye haoni karoso mpaka hapo?

  Kama anata kweli waende mahakamni basi Kuundwe tume huru ya kuyapitia tena matokeo ya uchaguzi na kulinganisha matokeo yaliyoko mikoani na waliyonayo NEC kama yatakuwa sawa na ndipo hao wabunge waende mahakamani uone kama watasubutu hata kuta kumsikia makamba.

  Nilitegemea CCM chama tawala kuonyesha mabadiliko ya kidemocrasia ili kizidi kuitawala nchi hii matokeo yake ndio kinaharibika na wana CCM wengi wanaliona hili kwani kuna matabaka makubwa mengi tuu ndani ya CCM Wenye Maslahi yao binafsi , wenye maslahi ya Nchi, na walio kati wao ni bendere kufuata upepo.

  Nilitegemea Makamba kwa muda huu ndio muafaka wa kujipanga na kuipangua safu za uongozi na kusimika nguvu mpya za UVCCM kujiandaa kwa chaguzi zijazo na kuachana na zengwe tuwe na siasa za kujenga nchi na sio za kukipendelea CCM, Inamaana CCM wao ni bora tuu hapa nchini na wengine sio raia wanao stahiri kuona matunda ya serikali yao

   
 5. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #5
  Nov 20, 2010
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,202
  Likes Received: 1,007
  Trophy Points: 280
  Sambamba na agizo la Makamba ni vizuri pia madiwani na wabunge wote wa upinzani walioshindwa na ccm wafungue kesi mahakamani. Wakati wa uendeshaji kesi zinaweza kuibuliwa hoja za kisheria za kupima uadilifu wa nec kwa kuomba kura zote za udiwani ubunge na urais kutizamwa upya kuona kama zinawiana na zile zilizotangazwa na nec. Hapa patatusaidia kujirizisha na kura za rais kama zilikuwa sawa.
   
 6. M

  Mikomangwa Senior Member

  #6
  Nov 20, 2010
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 100
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  MAKAMBA atalaaniwa duniani na hata mbinguni kwa kulazimisha ukweli uitwe uongo.
   
 7. tempo_user1

  tempo_user1 Senior Member

  #7
  Nov 20, 2010
  Joined: Sep 7, 2010
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  huyu mzee hovyo kweli, yaani badala ya kujiuliza kwa nini nchi nzima watu wanalalamika ccm imechakachua kura yeye anadhani wameonewa!!! Huu ni upuuzi wa makamba na inaonyesha bado ana kiburi cha chama kimoja. Ni vyema akafanya hivyo mapema ili ukweli udhihirike kwani kwa mwendo ulivyo inaonekana ccm wanaelekea kupoteza majimbo mengi zaidi kwani mengi ya hayo wamepora ushindi wa Chadema mfano. Karagwe, Segerea, Sumbawanga, Shinyanga mjini, Kilombero, Kibaha mjini, Kigoma mjini, n.k
   
 8. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #8
  Nov 20, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Makamba actions confirm that he has no interest whatsoever with the country, it his political games that count. that is the cost of recruiting a mediocre in such a high position

  In short, Makambas call in the kick in the chin to NEC meaning kwamba election was never fair and didnt follow procedure

  My call would be for every opposition candidate who lost also to do the same so that we can declare the whole election a flop

  THANKS MAKAMBA FOR ACCEPTING THAT UCHAGUZI HAUKUWA HURU NA HAKI... I OWE YOU ONE
   
 9. D

  Deo JF-Expert Member

  #9
  Nov 20, 2010
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 1,190
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Ninajiuliza Je ni nini maana hasa ya Makamba?
  Je hata wale walioshindwa kihalali(ambao ninaamini ni hao wote) wafungue kesi?

  Nisaidieni nini malengo ya Makamba kisiasa na kimshiko. Anakampuni ya uwakili anayotaka kuipa kazi? Au majaji walioteuliwa kwa upendeleo (kama wapo) walipe fadhila? Niambieni.

  Na je kwa hili tutafiuka kweli?
   
 10. v

  vicenttemu Member

  #10
  Nov 20, 2010
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jambo la muhimu sio kuhangaika na kesi. Waende mahakamani wakafanye nini sasa? Si wameshindwa, kwa nn asiwaambie na wabunge wa vyama vingine walioshindwa waende mahakamani!
   
 11. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #11
  Nov 20, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  he is just confirming the votes were not fair and just

  ana akili fupi ndio maana hakujua alichosema, sijui mwanae huwa anakua wapi wakati baba anabwabwaja
   
 12. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #12
  Nov 20, 2010
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,529
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Kwani Katibu huwa anatekeleza mambo yake au maamuzi yalifanywa na chama chini ya mwenyekiti?
   
 13. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #13
  Nov 20, 2010
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
  Ze faza..&...Ze sani is semu semu!
   
 14. nzitunga

  nzitunga Senior Member

  #14
  Nov 20, 2010
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 193
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nahisi kwamba kura zimeshachakachuliwa, masanduku yameshabadilishwa na hivyo mahakama inaweza kutaka recount of votes, mambo ambayo Lisu alikataa huko Singida. Ni jambo hilohilo liliwacost CHADEMA kule Kigoma Mjini.

  Lakini nahisi pia lengo la Makamba ni kuwapoteza watu muelekeo. Ionekane kuwa NEC isNotEqualTo CCM, kwamba hata CCM nao wameathirika na NEC

  Kama CCM watafungua kesi nchi zima basi huo ni ushahidi tosha kuwa NEC ilitangaza watu wake iliyowajua wao, including JK. Na hii tunaomba wanaharakati waitumie kama gia nzuri ya kupiga kelele kila pahali kwamba TUME huru ya Uchaguzi ndio suluhisho pekee.

  Nawakilisha.
   
 15. J

  Jibaba Bonge JF-Expert Member

  #15
  Nov 20, 2010
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 1,224
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Siyo kwamba anazeeka vibaya; hajawahi kuwa vizuri hata siku moja. Jaribu kuchunguza toka alipokuwa mwalimu (Ualimu Pasipo Elimu)wa shule ya msingi mifadhaiko ilikuwa haimwishi.
   
 16. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #16
  Apr 6, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  huu upuuzi ndio unaotuharibia kodi zetu.
   
Loading...