Makamanda wa Polisi (Iringa & Dar) watofautiana sakata la Abdul Nondo

Hii ishu sasa inachosha, kila mtu anaongea lake anyway labda mahakamani ukweli utajulikana.
 
Labda tungemsikia na nondo akieleza ndio tutajua nani mkweli
 
"Jana tarehe 7 mwezi wa tatu majira ya saa moja Abdul Nondo alifika katika kituo cha polisi Mafinga wilaya ya Mufindi na kuelezea kuwa ametekwa na watu wasiofahamika, jeshi la polisi mkoa wa Iringa limefungua jalada la uchunguzi ili kubaini ukweli kama alikuwa ametekwa na kama kweli alikuwa ametekwa tunaahidi kwamba sisi jeshi la polisi tukiwapata watuhumiwa sheria itachukua mkondo wake" alisema kamanda Bwire

"Mnamo tarehe 7 Machi mwaka huu jeshi la polisi kanda Malaamu ya Dar es Salaam lililetewa taarifa kutoka polisi mkoa wa Iringa kwamba mwanafunzi huyo aliyekuwa amedaiwa kutekwa na watu wasiojulikana alipatikana mkoani humo wilaya ya Mafinga akiwa na afya njema na mwenye kujitambua akiendelea na shughuli zake na wala hakuripoti tukio lolote kabla ya kukamatwa ili kuthibitisha kile kilichokuwa kikisemwa ametekwa na watu wasiojulikana. Hakuripoti mahali popote si kwa Mwenyekiti wa Mtaa, si kwa Afisa Mtendaji wa Kata, wala kituo chochote cha polisi mkoani Iringa bali alikamatwa akiwa Mafinga akiendelea na shughuli zake" alisisitiza Mambosasa

Siku hizi ukitaka kuamini yale yanayosemwa na Jeshi la Polisi unatakiwa uwe na akili za mwendawazimu, na hapo ndio itakuwa rahisi hata kuelewa risasi ikipigwa hewani kwenda juu inapinda kona kuifuata daladala, au askari wa FFU waliopiga raia huko Ukonga sio FFU, nk.
 
Chakaza Kwa hiyo unataka kusema nini???!!! Huyu Nonda sijui Nondo au nani sijui siyo issue tena....Issue nzima ni ya kitoto, kuanzia wote wanaoshabikia kinachoitwa kutekwa na ambacho kimekanushwa na hata sisi wenyewe tunaoendeleza mjadala usio na tija...
 
Kwa hiyo unataka kusema nini???!!! Huyu Nonda sijui Nondo au nani sijui siyo issue tena....Issue nzima ni ya kitoto, kuanzia wote wanaoshabikia kinachoitwa kutekwa na ambacho kimekanushwa na hata sisi wenyewe tunaoendeleza mjadala usio na tija...
Mjadala usio na tija wakati unahusu maisha ya mtu yanayochezewa?
Utakuwa na tatizo wewe!
 
Njia ya mwongo ni fupi, tuwaache waendelee kujitoa ufahamu kama vile nchi hii na raia wake wametununua kutoka kwa Mwenyezi Mungu! Siku usiyo na jina watalia na kusaga meno mbele ya hukumu! Mungu anawaona
 
Siwezi kimlaumu Mambosasa, na hili najua mambosasa na yule mwenzake wa Iringa wamelikosea makusudi kumwaibisha aliyewalazimisha ama kuwapikia na kutoa ripoti ya huyu Nondo, haiwezeka mambosasa awe hakujua alicho sema mambosasa wa Iringa.

Hongera Mambosasa wote wawili.
 
Kurzweil Jamani hivi nani anawadanganya kwamba hadithi kama hizi zitafuta taswira ya kutekwa kwa huyu kijana? Hata picha yake alipookotwa asubuhi tayari ilikuwa inatia shaka.

Ninaona nguvu kubwa sana inatumika na uvccm kuwenye mitandao kulazimisha watu waamini kwamba eti alikwenda Iringa kwa mpinzi wake.

Nani ataamini habari za Mkenya wa Ulimboka? Tafadhali msiwachezee Wananchi kwa kwa kudhani kwamba hawana akili.
 
Ni wazi kuwa Mambosasa katoa kauli hiyo kuback up matamshi ya Mwigulu na Makonda na sio kwa weledi wa kazi yake
 
Back
Top Bottom