Makamanda wa Polisi (Iringa & Dar) watofautiana sakata la Abdul Nondo

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
39,702
71,013

Wakati RPC Iringa akieleza mapema kuwa Nonda aliripoti saa moja asubuhi siku iliyofuata kituo cha Mafinga Polisi, bwana mkubwa Mambosasa yeye anasema Nonda hakupata kuripoti popote hata serikali ya mtaa na kuwa alikuwa anaendelea na maisha na kimada wake.
Kwa nini Polisi Dar wanapotosha Habari hii?

Jeshi la polisi nchini limetofautiana katika taarifa zake kuhusu kupatikana kwa Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), Abdul Nondo ambapo RPC wa Iringa alisema kijana huyo alifika mwenyewe kituo cha polisi huku Mambosasa akipinga hilo.

Katika taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Juma Bwire Machi 8, 2018 imeonyesha kutofautiana na kauli iliyotolewa jana Machi 13, 2018 na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, kamanda Juma Bwire alisema haya.

"Jana tarehe 7 mwezi wa tatu majira ya saa moja Abdul Nondo alifika katika kituo cha polisi Mafinga wilaya ya Mufindi na kuelezea kuwa ametekwa na watu wasiofahamika, jeshi la polisi mkoa wa Iringa limefungua jalada la uchunguzi ili kubaini ukweli kama alikuwa ametekwa na kama kweli alikuwa ametekwa tunaahidi kwamba sisi jeshi la polisi tukiwapata watuhumiwa sheria itachukua mkondo wake" alisema kamanda Bwire

Taarifa ya RPC wa Iringa imeonyesha kukinzana na taarifa aliyotoa jana Kamanda Mambosasa ambaye amedai kuwa Abdul Nondo hakuripoti sehemu yoyote ile na kudai kuwa walimkuta akiendelea na shughuli zake.

"Mnamo tarehe 7 Machi mwaka huu jeshi la polisi kanda Malaamu ya Dar es Salaam lililetewa taarifa kutoka polisi mkoa wa Iringa kwamba mwanafunzi huyo aliyekuwa amedaiwa kutekwa na watu wasiojulikana alipatikana mkoani humo wilaya ya Mafinga akiwa na afya njema na mwenye kujitambua akiendelea na shughuli zake na wala hakuripoti tukio lolote kabla ya kukamatwa ili kuthibitisha kile kilichokuwa kikisemwa ametekwa na watu wasiojulikana. Hakuripoti mahali popote si kwa Mwenyekiti wa Mtaa, si kwa Afisa Mtendaji wa Kata, wala kituo chochote cha polisi mkoani Iringa bali alikamatwa akiwa Mafinga akiendelea na shughuli zake" alisisitiza Mambosasa

Mpaka sasa jeshi la polisi linaendelea kumshikilia Abdul Nondo, kwani kwa mujibu wa wakili wa mwanafunzi huyo anasema kwamba mpaka jana Machi 14, 2018 hajafanikiwa kukutana wala kuongea na mteja wake.

Chanzo: EATV

Polisi.jpg

Polisi wetu wanafanya kazi kama vile RPC wa Iringa na Dar wako nchi tofauti. Huyu RPC wa Dar weledi kautia mfukoni ni kama vile anataka kuthibitisha madai ya Makonda na Meigulu. Mambosasa amekubali ku-compromise na wanasiasa na atajikuta anapelekeshwa na interests za wanasiasa.

Vv
Tatizo ni ceremonial post mkuu nothing else
Kama vp weka cv yake hapa
 
Umeandika wewe au EATV wewe ukakopi na kupest

Wewe ndo umechanganya habari kichwa cha habari unasema polisi wa DODOMA &DAR

Kwenye habari unatuletea iringa dar sasa wapi na wapi?

Wewe unataka kuufanganya umma

Teh
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom