Makamanda mbona hamsomeki?

Makamanda mbona hamsomeki?

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Posts
97,070
Reaction score
136,458
Ni kitambo kidogo sijalonga na hawa washikaji zangu ‘makamanda’.

Lakini leo nadhani ni siku muafaka ya kulonga nao.

Sasa nyie makamanda, tokea Rais Samia ameshika hatamu za uongozi, nyie ndo mmekuwa mstari wa mbele kabisa kuimba mapambio kwake.

Mmekuwa na furaha isiyo na kifani! Furaha yenu hiyo inatokana na imani yenu ya kwamba yale mazonge mliyokuwa nayo enzi za hayati Rais Magufuli, sasa yamekwisha.

Kwamba eti yeye alikuwa mkali sana. Yeye alikuwa katili sana. Yeye alikuwa mshamba sana. Yeye alikuwa fisadi sana. Yeye alikuwa hivi na vile sana.

Sawa. Hayo ni maoni yenu tu. Na maoni yenu si lazima yawe ndo uhalisia wa hali au mambo.

Leo ngoja niwaulize swali: kama nyinyi sasa hivi ndo mmekuwa viongozi wa kuimba mapambio ya Rais Samia na CCM yake, kwa nini sasa leo mmenuna, mmevimba, na mmefura kisa tu ex-kamanda mwenzenu aitwaye Lazaro Samweli Nyalandu karudi CCM ili aweze kuunga mkono uendeleaji wa kazi za Rais Samia?

Kama nyie mnamuunga mkono Rais Samia, na yeye anamuunga mkono Rais Samia, wote nyie lenu si ni moja?

Mapovu ya nini sasa?

Ndo kusema hamjielewi kiasi hicho au?

Nimalizie kwa kuwaaga kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania…..

Au niwaage kwa People’s……

Teh teh teh 🤣🤣🤣
 
chadema kwisha habari yao viongozi wamekimbia nchi waliobaki wanabaki kubweka tu na kina mdee hawana kazi za kufanya badala ya kuimarisha chama wao kazi ni kina mdee kila siku uchaguzi ukifika mtasema mmeibiwa kura wakati hamzitafuti sasahivi
 
Nothing new hapo, Nyalandu alikuja Chadema kwa mapenzi yake na ameondoka kwa mapenzi yake, hakuna kesi, zaidi yeye ndio nimemuona mshamba kwa zile pumba alizoongea, ngoja aje dikteta mwingine huko CCM tuone atakimbilia wapi.
 
Ila mama anatuvuruga sana, sio Makamanda wala S. Gang wote tumevurugwa. Sijui tuungane maana naona sote tumekuwa watoto wa nje ya ndoa.
Au nasema Uongo #Nyani Ngabu
 
Back
Top Bottom