Barubaru
JF-Expert Member
- Apr 6, 2009
- 7,161
- 2,323
Hatubishani, labda wewe ndio waona tunabishana, kwani mimi naandika nayoyajua na wewe una yako..Ukieleza one side of the coin nami nakupa upande wa pili ambao wewe hutaki. Mtu anaweza kuja hapa akadai Mohammed Said anautetea Uislaam JF, nami nikaja na kusema hapana ni katika harakati za kutangaza na kuuza kitabu chake. - Hapo, mkweli atakuwa nani zaidi ya Mohammed Said mwenyewe? bahati mbaya yote uloyaandika wewe wahusika karibu wote wameisha kufa! - Ukweli ni upi? ndio mjadala tulokuwa nao hapa..
Laa basi wewe hatari sana... zaidi ya mpira wa mchangani na Saigon ulichezea timu gani vile?.. Na muziki umewahi kupigia bendi gani ya taarabu au naomba basi copy ya muziki wako maana utakuwa umeuzika kama vitabu vyako....Samahani, nilikuuliza sana mkuu wangu hivi wewe una umri gani hajanambia bado!
Mkandara,
Usiharibu mnakasha kwa kutaka kututoa nje ya darsa letu adhimu.
Kwani kila wakti unabishana mara Zenji ni nini (pamoja na kufafanulia kwa fus'ha arabic, sasa unarudi na Saigon.) Sisi tunachotaka kama una paper au utafiti wowote ulionao iwe kwa kijitabu au hata makala tuwekee hapa tuichambue na kuijadili kuliko kutaka kututoa nje ya mada.
Nakupa pole.