Chama,
Ndugu yangu sasa baada ya kusomesha historia unataka niingie
katika "semantics!"
Kwa ufupi ni hivi.
Chukulia hayo niliyoandika kama kitu tu cha kawaida unasoma
unaamini au unakataa.
Huna sababu ya kuteseka sana kutaka kujua hivi hii nisomayo
ni historia ya kweli au historia ya kweli ni ile niliyosomeshwa
na walimu wangu?
Si lazima uniamini.
Hadi leo Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam wanasomesha historia
rasmi.
Wala hapaja kuwa na maandamano.
Shule nyingi za Kiislam wanasomesha historia hii yangu hakuna
shida. Wanafunzi wanatembea kifua mbele. Washajijua.
Kuna vijana wa Kiislam walimu wa historia katika shule za Kiislam.
Hawa vijana wanasomesha ile historia ya Nyerere kuanzia 1954.
Wakimaliza wanasomesha historia hii ya kitabu changu.
Taarifa nipatayo ni kuwa darasa huchangamka kweli kweli.
Sasa kama kuna jipya Insha Allah tuendelee na mjadala.
Mohamed
Bwana Mohamed nadhani umeelewa nini nilichoandika; unataka kutumia hekima zako za kiusomi kukwamisha mjadala; wewe ndio mtoa mada sisi ndio wanafunzi ; hivyo tunahaki ya kuuliza maswali na kuomba ufafanuzi; jipya lipo lakini kabla sijaenda mbele nipe ufafanuzi wa nilichoomba.
Chama
Gongo la Mboto DSM