Makala ya Mwigamba irudiwe na Magazeti yaliyo huru kweli kweli!

Kwakweli MMM umenena na mm sina mashaka na wewe naamini unaweza! waandishi inabidi waungane juu ya hili uhuru wa vyombo vya habari uheshimike
 
Ni makala nzuri inayofikirisha sana. Ni dhahiri kwa mtawala yeyote mwenye uvumilivu mdogo(elements za udikteta) ataona kuwa makala hii ni kama mtu anawafungia mbwa wako kwenye chumba kidogo chenye chetezo kinachofuka moshi wa bangi na hivyo huenda moshi huo ukawapatia ukichaa na kumuuma wewe mwenyewe. Ila kwa mtawala anayefikiria beyond yeye binafsi ataona kuwa hii ni challenge inayopaswa kujibiwa positive kwa vitendo kwa kufanya utafiti juu ya yaliyosemwa na kuyafanyia kazi. Reaction ya kuiita makala ni ya uchochezi inaleta faida zaidi kwa mwandishi katika kufikisha maoni yake. Ni dhahiri kesi ya uchochezi iliyofunguliwa dhidi ya makala hii imefanya watu wengi kuwa na interest ya kujua ni nini klipo kwenye makala ghiyo?, na hiyo kuiongezea umaarufu. Binafsi sikuwahi kuisoma na kuijua zaidi ya leo hii hapa na kuona kuwa kumbe jamaa kaandika kitu cha maana zaidi.

Hii inanikumbusha mifano ifuatayo ambayo reaction ya watawala iliipa umaaru in excessive.
  1. Ule mtandao wa internet uliwahi kuchapisha picha ya kutengeneza ya mkuu wa nchi katika tendo la kishoga
  2. Habari za wikileak kuhusu kiongozi wa nchi kununuliwa suti
  3. ....
  4. ...
You name it. Makala hii ni maoni ya kawaida ya mtu na kuiita uchochozi ni kuchochea watu waitafute na kuisoma zaidi tena na tena. Ukiwa katika nafasi ya uongozi ujue kuwa kama waswahili walivyosema nature ya kazi inakufanya wewe kuwa jalala. Fuata misingi ya uongozi na tenda haki hakuna la kukufanya usilale. Kwani askari nao wana akili zao hawawezi kuwa na za kuambiwa tu na malkala kama hii au ya wakubwa zao, lazima wachanganye na za kwao. Ukiomba kuwa mwanandoa basi kulala bila kanchili si suala la kuogopa. Na unapoomba kuwa kiongozi basi kusikia maoni yanayokuudhi si suala la kuogopa ni sehemu na majukumu ya kazi hiyo.... Anayeongelewa hapo ni mtawala si mtu binafsi, ukiachia uongozi hakuna atakayekuwa na haja na wewe...

Tuwe wavumilivu, tusipende kuzi-surbodinate hisia zetu juu ya mamlaka yetu. Tukifanya hivyo uongozi utatushinda...

Hata mie kabla nilikuwa sijaisoma ila baada ya kuisikia sana ikabidi niitafute, kibaya zaidi kumbe jamaa kaelezea historia yake na ya kwao ambayo ni ya kawaida tuu, maana kasema ukweli kabisa ila unaogusa tabaka tawala.
 
Siku huo ugonjwa utakapopona ndani ya vichwa vya wadanganyika ndipo tutapata maendeleo ya kweli.

Maana si ajabu kwa mwalimu, mhandisi, mchumi, mwanahabari, mwanajeshi, askari polisi, askari magereza ama mwansayansi kukubali
ujira mdogo wa sh.135,000 kwa mwezi, wakati wanasiasa wanajikusanyia sh.330,000 kwa kukaa kitako siku moja tu!!
Na bado tunaendelea kuhamsishana kwa ujinga wa kwamba kazi fulani ni wito. Kwanini ubunge, uraisi, uwaziri, ukurugenzi, UDC, URC navyo visiwe wito??

hovyoooooo...!!

Hapo umegonga mapoiti matupu mkuu.
 
Rafiki yangu mwanajeshi anasema gazeti la Tanzania Daima lenye waraka huu limekuwa lulu kwenye kambi za jeshi.
 
hiyo makala imepotezewa wapi tena?.........
Ndio ile inayoelezea kuwa awali Mwandishi alisomea DIT na kuwa Telecoms Technician (FTC) na baadaye kujiunga na Jeshi la Megereza Chuoni Kiwira........na baadaye ikanichanganya kwani inaelezea mtu huyo huyo alisoma huko Magu then Mazengo Sec na Kufaulu na kuendelea hadi Chuo Kikuu na kupata kazi Umoja wa Mataifa........?

Ikumbukwe pia kuwa mbali na mapungufu ya kanuni za utekelezaji wa sheria zetu.........inakuwa mbaya zaidi tunapokuwa na incompetents from both sides i.e. raia na mwajiriwa........na bahati mbaya sana individuals wachache sana ambao wasimamiaji wazuri wa sheria zetu wanapigwa vita na wasiojuwa/wabinafsi walio wengi.......na wao pia wameingia mitegoni..........

Kwa ujumla nchi yetu inahitaji "overhaul"........je mafundi ni akina nani?.......
 
Nasema tuache upuuzi jamani,hakuna uchochezi katika makala ya Mwigamba,HAKUNA TENA HAKUNA WALA CHA KUFIKIRIA UCHOCHEZI KWA HAO ASKARI,NILISHASEMA HUMU,JAMANI RAIA HAWEZI KUMCHOCHEA ASKARI,HAITAKAA ITOKEE,ASKARI ANA MIIKO YAKE NA ANAUTEKELEZAJI WAKE WA KAZI,SIO KWA UCHOCHEZI TOKA KWA RAIA,HAKUNA KITU KAMA HICHO,Tuelezwe tu kama kuna kitu behind the curtain/capert.na kama wanaona kuna uchochezi basi hayo wanayoyanfanya ambayo Mwigamba aliyaeleza ni ya kweli hivyo wanapata hofu kuwa askari ataasi kwa kusikia uchungu juu ya wanayowatendea.Lakini to be honest hakuna raia anaeweza kuwachochea askari,labda nitakuja na thread nieleze kwa undani ni kwanini nasema raia hawezi kuchochea majeshi yetu,maana naona watu wanadhani hilo ni jambo rahisi tu kiasi kwamba makala hiyo inaweza kuchochea,hata hao waliowakata ni maelekezo ya wanasiasa tu.
 
mbona hilo rahisi; nimeshafanya hivyo na makalayangu ya kuunga mkono ya Mwigamba itatoka kesho, inshallah.

Ok hapo sawa na utakuwa umefanya kwa vitendo nitaifuatilia ikiwezekana nitaibandika hapa na nitaisambaza kwenye social network zote hata IGP Mwema nitamtumia.
 
Kwani sheria zinasemaje jamani???kuhusiana na huu waraka..
Kisheria, yuko kwenye hali ngumu. Kurudia makala ni upuuzi. Kwanini hao waandishi wasiandike makala zao?

Namaanisha,waandike makala kuwaambia wanajeshi wasifuate amri kama zinawakandamiza wananchi kwa maneno yao!
 
Kisheria, yuko kwenye hali ngumu. Kurudia makala ni upuuzi. Kwanini hao waandishi wasiandike makala zao?

Namaanisha,waandike makala kuwaambia wanajeshi wasifuate amri kama zinawakandamiza wananchi kwa maneno yao!

Thanks ZOMBY tumekuelewa!
 
Hata mimi naona ingefaa makala ile iwekwe hadharani na mwenye link atuwekee humu jamvini ili tuipime sisi ma Great Thinkers kama ni kweli ilikuwwa ya kichochezi au CCM wanakigwaya kivuli chao! Katiba ina provide haki ya kila mwananchi kuhabarishwa kwa mantiki hiyo hakuna ubaya wa kuichapa tena ili hata na wale wasiobahatika kuiona waione.
Angalisho: CCm wanaanzisha precedent mbaya kabisa ya kuwanyanyasa waandishi na wapinzani. Wafahamu kabisa kwamba wao pia watakaangiwa mafuta hayo hayo baada ya kusukumiwa upinzani.
 
hiyo makala imepotezewa wapi tena?.........
Ndio ile inayoelezea kuwa awali Mwandishi alisomea DIT na kuwa Telecoms Technician (FTC) na baadaye kujiunga na Jeshi la Megereza Chuoni Kiwira........na baadaye ikanichanganya kwani inaelezea mtu huyo huyo alisoma huko Magu then Mazengo Sec na Kufaulu na kuendelea hadi Chuo Kikuu na kupata kazi Umoja wa Mataifa........?

Ikumbukwe pia kuwa mbali na mapungufu ya kanuni za utekelezaji wa sheria zetu.........inakuwa mbaya zaidi tunapokuwa na incompetents from both sides i.e. raia na mwajiriwa........na bahati mbaya sana individuals wachache sana ambao wasimamiaji wazuri wa sheria zetu wanapigwa vita na wasiojuwa/wabinafsi walio wengi.......na wao pia wameingia mitegoni..........

Kwa ujumla nchi yetu inahitaji "overhaul"........je mafundi ni akina nani?......[/COLOR].[/QUOTE]

Samsoni Mwigamba ameshaanza, kazi kwa wengine nao kufanya sehemu yao.
 
Makala yake ni ya kawaida tu kwa jicho la mtu safi mbele ya wapiga kura wake!

Kwa hali ya nchi ilivyo, whereby elites wachache ndo wanaofaidi keki ya taifa, huu ni mwiba kwao!! Big up Mwigamba, its true si lazima ukabidhi akilli yako kwa mwingine just because wewe ni mwanajeshi...
 
Watawala wetu wamelikuza wenyewe jambo hili kwa kuwakamata akina Kibanda. Makala hii ilikuwa imetupita wengi tu. Kupingana na UKWELI kama huu uliomo kwenye makala hii ni kazi ngumu sana. Kuuita UCHOCHEZI ni kuchochea zaidi. Watu aina ya Mwigamba kwa sasa Tanzania hii ni wengi mno na wapo hata humo kwenye DOLA kwenyewe. Ni suala muda tu. Yataibuka mengi.
 
Back
Top Bottom