Makala ya Mwigamba irudiwe na Magazeti yaliyo huru kweli kweli! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Makala ya Mwigamba irudiwe na Magazeti yaliyo huru kweli kweli!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Dec 20, 2011.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Dec 20, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,394
  Trophy Points: 280
  Kama vyombbo vya habari nchini - hasa vile vinavyodai kuwa viko huru - vinaamini kuwa makala ya Mwigamba ni makala ya maoni na kuwa maoni yake yanalindwa na uhuru wa maoni basi vyombo hivyo virudie makala hiyo kwenye magazeti yao kama ishara ya kutopishwa magoti. Wahariri wanaoamini kuwa Kibanda anaonewa na kuwa kinachofanyika ni njama tu ya kutisha vyombo vya habari basi huu ndio wakati wa kuonesha imani hiyo kwa vitendo - chapisheni makala ya Mwigamba tena jinsi ilivyo na muwe tayari kuungana na Kibanda.

  Au mnatakaa tuwaambie alichokifanya Robert Makange na Kheri Rashid Baghella? Au hata waandishi wetu na watoa maoni hawana mifano tena? Well.. kama mmepigishwa magoti na serikali ombeni radhi kuwa kuanzia sasa mtakaa kwenye mstari lakini kama kweli mnaamini katika uhuru wa maoni (hasa maoni yenye kuudhi na kukera watawala) basi rudieni makala hiyo na pia waelezeni wasomaji wenu (kwenye tahariri) kwanini mnafanya hivyo.

  I for one intend to do the same. Haki ya maoni haisemi ni haki ya maoni yenye kuwafanya watawala watabasamu na kucheka. Haki ya maoni ya kuudhi, kukera na kuwafanya watawale wawe nyongo inastahili kulindwa kama vile haki ya wale wanaotaka tuimbe wimbo wa "tunawapenda tunawapenda". Uhuru wa vyombo vya habari hauko kwenye kumiliki kwake au jina lake bali uko kwenye kuwa huru kutoa maoni pasipo kulazimishwa aina ya maoni ya kutoa.

  MMM
   
 2. Borakufa

  Borakufa JF-Expert Member

  #2
  Dec 20, 2011
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 1,503
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Haya kaka wapo hapa wamekuelewa! Kubenea na Jeneral wanaweza lakini wengine ha ha ha! makombo tu!
   
 3. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #3
  Dec 20, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mwenye uwezo wa kurudia hiyo makala ni kubenea pekee wengine awawezi hata kidogo.
   
 4. M

  Marigwe JF-Expert Member

  #4
  Dec 20, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 226
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 33
  Acha uchochezi wewe MM. Mwigamba na Kibanda kwa kuwa wanaudhi lazima washikishwe adabu!
   
 5. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #5
  Dec 20, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,971
  Likes Received: 2,967
  Trophy Points: 280
  Acheni uchochezi wewe.
   
 6. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #6
  Dec 20, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Ngoja niendelee kuwa Tomaso,

  Kuna watu leo lazima waende kugongesha bilauli....Hao ndio watakaorudia makala nzito (by any size of heavy weight) kama ile ya S. Mwigamba???


  DC!!
   
 7. L

  LATTICE BOND JF-Expert Member

  #7
  Dec 20, 2011
  Joined: May 30, 2011
  Messages: 219
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi wewe mwanakijiji kwa utalaam wako wadhani Tz kuna vyombo vya habari vilivyo huru? kuna waandishi wa habari walio huru?

  BONGO HAKUNA JAMBO KAMA HILO!!!!!!!!!
  Kwanza waandishi wa kibongo njaa kali!! ukiwaita kwenye press conference lazima uwape 20000 au zaidi usipotoa habari yako ama haitoki au unaandikwa vibaya!! Je, huo ni uhuru?
  WEWE NA MIMI SOTE TUNALIJUA HILI!!! SASA JE, HOJA YAKO HIYO NI KUPIMA WANGAPI WANAJUA UJINGA WENU AU NANI WANAJUA UONEVU ANAOFANYIWA KIBANDA????/
   
 8. Mwakalinga Y. R

  Mwakalinga Y. R Tanzanite Member

  #8
  Dec 20, 2011
  Joined: Oct 22, 2008
  Messages: 2,718
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  kweli kabisa MMM
   
 9. IsangulaKG

  IsangulaKG Verified User

  #9
  Dec 20, 2011
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 702
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 45
  Segmented Tanzania Media... wengi wanafyata mkia!
   
 10. Borakufa

  Borakufa JF-Expert Member

  #10
  Dec 20, 2011
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 1,503
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mla makombo lazima awe zuzu tena uzuzu ugeuka kuwa uzezeta wa kufikiri kama makombo yenyewe yanatokana na damu na jasho za watanzania. Siku yenu ipo! Kama Madikteta wengine wote nanyi pia mtapita tu ole wenu saa yenu itakaposimama.
   
 11. Borakufa

  Borakufa JF-Expert Member

  #11
  Dec 20, 2011
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 1,503
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Zuzu lingine hili makombo yamelilevya
   
 12. HISIA KALI

  HISIA KALI JF-Expert Member

  #12
  Dec 20, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 694
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi binafsi sikupata bahati yakuona wala kusema hiyo makala. Hivyo basi tunaomba kama kuna mtu anaweza kuiweka hapa tafadhali
   
 13. Borakufa

  Borakufa JF-Expert Member

  #13
  Dec 20, 2011
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 1,503
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Nani sasa?? Kibanda, Mwigamba au Mwanakijiji???
  Au na wewe mpiga makombo??
   
 14. Lobapula

  Lobapula JF-Expert Member

  #14
  Dec 20, 2011
  Joined: Jun 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 1,431
  Trophy Points: 280
  Mzee.Acheni uchochezi wewe.

  Kama hii ni design ya wasomi/ma great thinker tulionao nina wasi wasi sana na huko tuendako kama Taifa.
   
 15. Mnama

  Mnama JF-Expert Member

  #15
  Dec 20, 2011
  Joined: Oct 13, 2010
  Messages: 1,651
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Tusikubali kamwe kwa vitisho kunyamazisha uhuru wa kutoa moani ya Mtu hata kama hayawapendezi watawala na vibaraka wao.
   
 16. Borakufa

  Borakufa JF-Expert Member

  #16
  Dec 20, 2011
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 1,503
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Hivi kwa kuisoma hii bado kuna kuda atang'ang'ana na makombo ya mafisadi wa damu yetu! wake up all kudas!
   
 17. Alwatan

  Alwatan JF-Expert Member

  #17
  Dec 20, 2011
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 409
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Hatutaki Mutiny ya jeshi Tanzania yetu hii, tunajua wengine mpo ulaya maisha mmeyapatia. Siye hatuna pa kukimbilia zaidi ya Tanzania yetu hii hii. Jeshi ni wito kama huyo mwigamba lilimshinda na akasepa, aendelee na kazi zake nyingine. Ningemuelewa kama angewashauri wengine nao wasepe kama yeye, sio kufanya uasi. Uasi wa jeshi ni chanzo cha machafuko. Na machafuko hayachagui sura. Hao viongozi watakua wa kwanza kupanda ndege kwenda uhamishoni, tutakaobaki patachimbika.

  Kamwe siungi mkono UHURU WA KIPUMBAVU usiokua na mipaka!... Sitaki kumquote Nyerere maana wengi wameshamquote kuhusu
  UHURU usio na mipaka.

  Besides ningependa Kubenea nayeye aichapishe ili aunganishwe kwenye kesi na Kibanda, ili kutupunguzia mzigo wa waandishi wachumia tumbo kwenye tasnia ya habari.... Maana kwa kweli wanachefua hawa walamba ****** wa mafisadi.

  Hangaikeni na mikesi mwenzenu EL kishaanza kusaka watu wengine watakaofanya kazi yenu ya kumsafisha!
   
 18. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #18
  Dec 20, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Sio katika jamii hii,
  sio kwa watanzania!
  Kwa watanzania mambo kama hayo watu watayapima kwa matumbo yao kwamba as long as mkono unaenda kinywani basi hata kama watakamatwa wanaharakati wote kila kitu kitaendelea kama kawaida... Tena hao wanaharakati ndio wataonekana wa ajabu na wakorofi.
  Ifuatilie hii thread, soma maoni ya watu.
  Sisi ndio watz tuliogawanyika katika masuala yote....
  HATUWEZI KITU
   
 19. kanyagio

  kanyagio JF-Expert Member

  #19
  Dec 20, 2011
  Joined: Dec 10, 2009
  Messages: 986
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  nimesoma makala hiii kama mara mbili sijaona tatizo.. sasa sijui tatizo wapi jamani..
   
 20. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #20
  Dec 20, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Hivi ni kweli hii makala ndiyo inawapeleka watu gerezani au kuna kitu zaidi ya hiki ? Hakika haya ni maoni na matukio yaliyo mtokea Mwigamba na neno uasi haupo hata mara moja .Wacha kesi ikianza kuunguruma tutajua ukweli .Watu wamekosa utashi wa kisiasa wana weweseka kila dakika .Hii bni dhambi kubwa mno ya uonevu na mwisho wake si mzuri maana hii niu kutaka kumuua paka kwenye chumba kimoja kidogo atageuka kuwa Simba .
   
Loading...