Makala: Shujaa alieshindwa kuhimili changamoto za ndoa

Ushimen

JF-Expert Member
Oct 24, 2012
37,217
85,352
DUNIA nzima imemlilia Nelson Mandela, hata wale aliowatukana kwamba hawana akili na ni wapumbavu, walifika Afrika Kusini kumlilia.

Tumeshuhudia Rais mstaafu wa Marekani, George Bush, akija kumlilia na kutoa heshima zake za mwisho kwa Mandela, mtu ambaye aliukosoa kwa ukali utawala wake.

Hata waliomchukia Mandela, walifika kumlilia, pamoja na mambo mengi ya kumsifia Mandela, heshima yake ilipanda juu zaidi baada ya kujitokeza kama mtu mwenye kusamehe na kusahau.

Mandela, aliwasamehe waliomfunga na kumtesa kwa kipindi cha miaka 27, aliwasamehe wale walioendesha mauaji ya Waafrika wa Soweto, watoto wa Soweto waliokufa wakitetea haki zao za msingi, aliwasamehe wauaji na kukaa nao meza moja, ingawa alishindwa kabisa kumsamehe mkewe wa pili, Winnie Mandela.

Tunapomlilia Madiba, ni muhimu kujiuliza maswali yenye majibu; kwa nini Mandela aliwasamehe watu wote hadi wauaji, akashindwa kumsamehe mke wake? Winnie alifanya kosa gani kubwa kiasi cha kutopata msamaha?

Swali la pili ambalo linafanana kwa kiasi na la kwanza, kwa nini matatizo ya ndoa ya Mandela na Winnie, anabebeshwa Winnie peke yake?

Hata wanawake ambao katika hali ya kawaida wangekuwa upande wa Winnie, wanamlaumu Winnie, kwamba alimsaliti Mzee Mandela. Wanamlaumu alimtesa Mzee Mandela.

Je, si ukweli kwamba Nelson Mandela ni shujaa aliyeshindwa kuhimili changamoto za ndoa? Wengi tunajua jinsi ndoa ilivyo na changamoto kubwa. Wengine wana mawazo kwamba Mungu, hakupanga taasisi hii (ndoa) iwe ilivyo sasa, ya mme mmoja na mke mmoja au hata kufunga ndoa; kwamba alituumba tuishi kama wanyama! Bila kuwa na kifungo cha ndoa!

Haya yanasemwa baada ya ndoa nyingi kukumbwa na changamoto. Mahatma Gandhi, alifikia hatua ya kutaka kuishi na mke wake, kama mtu na dada yake.

Walifanya kiapo cha kuacha uhusiano wa kimwili ? uhusiano wa ndoa, ili waishi kama ndugu. Hakuvunja ndoa yake kama alivyofanya Mandela, bali alitaka yeye na mkewe waishi kama mtu na dada.

Walijitahidi, ingawa kuna ushahidi kwamba kuna wakati walishindwa kutimiza ahadi hiyo na kuomba toba kwa Mwenyezi Mungu. Labda na Mzee Mandela angeendelea kuishi na Winnie kama mtu na dada yake leo hii angekuwa miongoni mwa wale wanaohimili changamoto za ndoa na labda kuleta imani na roho mpya katika taasisi hii inayoyumba.

Hoja ninayoijenga hapa ni kwamba Shujaa Mandela, ameishinda mitihani mingi maishani mwake lakini ameshindwa mtihani unaowashinda wengi, uvumilivu na kusamehe katika maisha ya ndoa.

Pamoja na heshima zote tunazompatia Mzee Mandela, alibaki ni mwanamume wa kiafrika mwenye kuutukuza mfumo dume.

Wanaoandika historia ya maisha yake, wanataja Mzee Mandela kumfanyia unyanyasaji wa kijinsia mkewe wa kwanza Evelyn, kiasi cha kuwaleta wapenzi wengine kwenye kitanda chao cha ndoa na kumlazimisha Evelyn kulala uvunguni mwa kitanda.

Mandela, hakutaka Winnie afanye kazi yoyote, alimtaka akae nyumbani na kuwalea watoto. Ukisoma barua ambazo Mandela alikuwa akimwandikia Winnie, kutoka gerezani alikuwa akirudia na kusisitiza akae nyumbani na kuwalea watoto, na kwamba yeye atafanya jitihada zote kutafuta fedha za kuitunza familia, na daima alimalizia ujumbe wake kwa maneno ?.. natumai utaishi kwa kuyatekeleza matumaini yangu..?, tafsiri ni yangu, inamaanisha ? Utaishi kwa kutekeleza mapenzi yangu,? kana kwamba Winnie mwenyewe hakuwa na mapenzi yake mwenyewe?

Si kwa ndoa ya Winnie pekee, hata ndoa yake ya kwanza na Evelyn, ilipata matatizo hayo hayo ya kutekeleza ? Mapenzi ya Mandela? au Mapenzi ya Baba mwenye nyumba.

Evelyn, alikuwa mkristu mwenye itikadi kali, hakukubali kuchanganya dini na siasa. Na hakukubali kutekeleza mapenzi ya baba mwenye- nyumba. Hata hivyo, kinyume cha ndoa ya Winnie, kwa Evelyn, aliyeshinikiza ndoa hiyo kuvunjika si Mandela.

Evelyn mwenyewe ndiye aliweka masharti ya ama Mandela kumchagua yeye au kuichagua siasa na Mandela, akaamua kuichangua siasa na ndoa yao ikavunjika.

Mbali na tatizo hili la mfumo dume la mwanamke kutekeleza mapenzi ya baba mwenye nyumba, mfumo ambao umezivuruga ndoa nyingi za kiafrika au kusababisha wanawake wengi wa kiafrika kuishi maisha magumu kwenye ndoa zao, Mzee Mandela alikuwa na tatizo la kutopata nafasi ya kutosha kusoma na kuelewa tabia za wapenzi wake.

Alikuwa akivutiwa na sura, muda mfupi anatangaza ndoa. Ilitokea kwa Evelyn, ilitokea kwa Winnie na hata kwa mkewe wa mwisho, Graca.

Kwenye kitabu chake cha-Long Walk To Freedom, ukurasa wa 101 anasema; ?Siku chache baada ya kukutana na Evelyn, kwa mara ya kwanza, niliomba kumtoa. Haraka haraka tulianza mapenzi na miezi michache baadaye niliomba tufunge ndoa, akakubali..?. Pia anaelezea jinsi Evelyn alivyokuwa msichana mzuri na wa kuvutia.?

Na ukurasa wa 214, Mandela anaandika: ?Siamini kama kuna mapenzi ya papo kwa papo, lakini nilipokutana na Winnie Nomzamo, kwa mara ya kwanza, niliamini nataka awe mke wangu..?

Na ndivyo ilikuwa, walifunga ndoa na Winnie, muda mfupi baada ya kukutana. Na historia iliyofuata, haikumpatia nafasi Mandela, kumfahamu Winnie. Harakati za kupigania uhuru na hatimaye kifungo cha miaka 27, ulikuwa ukuta mkubwa kati ya Winnie na Mandela.

Baadhi ya vyombo vya habari vilieleza jinsi uhusiano wa Graca Marchel na Mzee Mandela ulivyoanza. Mara ya kwanza alipokutana na mama huyu, Mzee Mandela aliuliza wasaidizi wake ? Huyu Mama mzuri hivi ni nani??

Wakamjibu ni ?Mke wa marehemu Samora Marchel?. Alipokutana na Graca, mara pili, Mzee Mandela, hakukumbuka alishatambulishwa, aliuliza swali lile lile ?Huyu Mama mzuri hivi ni nani?? Akajibiwa tena ni ?Mke wa Marehemu Samora Marchel?.

Ilipotokea mara ya tatu akaamua kutupa karata ya kufunga ndoa. Yawezekana kwa ndoa hii ya tatu, Mzee Mandela, amepata nafasi ya kuangalia mbali zaidi ya sura. Wake zake wawili wa mwanzo Evelyn na Winnie, alitamani sura zao na kuwataka wayatimize ?mapenzi yake?, hakupata nafasi ya kuangalia na kujifunza kwa undani karama zao na kuziachia karama hizo kuchanua.

Mzee Mandela, alivutiwa na sura, lakini hakuwa tayari kuyapokea na yale ya ndani. Evelyn, alipotoa ya ndani, na kuonyesha kwamba yeye si sura tu bali ana na mengine yanayounda ?utu?- wake na upekee wa yeye kuitwa ni fulani, Mzee Mandela hakuwa tayari kuyapokea na ndoa yao ikaishia hapo.

Vile vile kwa Winnie, Mzee Mandela alivutiwa na sura yake, lakini hakuwa tayari kupokea yale ya ndani. Winnie, mpambanaji, Winnie mwanasiasa, kwa vile kwa kipindi kirefu hawakuishi pamoja kuweza kufahamu mambo ya ndani ya Winnie, alipotoka gerezani na kupata nafasi ya kumfahamu Winnie alivyo, Mzee Mandela, alishindwa kabisa kumpokea jinsi alivyo. Winnie, mwenye sura nzuri ya kuvutia, alikuwa sasa ni Winnie mwanasiasa na Winnie mpambanaji. Mzee Mandela, akafunga milango ya moyo wake na kuanza mbio nyingine za kumtafuta mwenza mwingine.

Ndoa, ni kuunganisha watu wawili wasiofanana! Watu wawili ambao si ndugu wala jamaa! Ndoa ni kuunganisha watu wawili wenye tabia tofauti na karama tofauti. Hivyo ukiweka mfumo dume pembeni, ndoa inahitaji uvumilivu wa pande zote mbili, kusameheana kwa pande zote mbili, kuchukuliana kwa pande zote mbili, kila upande ukiziachia karama za upande mwingine kuchanua. Hivyo ikitokea ndoa ikavurugika na kuvunjika, si haki mzigo kubebeshwa upande mmoja.

Inawezekana Winnie, alifanya makosa na labda alitembea nje ya ndoa kama wanavyosema wengine, lakini ukilinganisha na kujitoa kwake kwenye mapambano ya kuleta uhuru wa watu wa Afrika Kusini, kampeni za kufunguliwa Mandela na kuendeleza jina la Mandela, wakati Mandela akiwa gerezani, jinsi naye alivyokamatwa na kufungwa zaidi ya mara 23, uzalendo wake kwa nchi yake, yangefunika makosa yake madogo na hasa kwa mtu kama Mandela, ambaye anatueleza aligundua faida ya kutafakari akiwa gerezani.

?Kifungo ndicho kilinifanya kutambua kwamba mwanadamu anahitaji muda wa kutafakari. Nilishangaa ni kwa nini kabla ya kufungwa sikutambua kitu hiki, maana ningeweza kutenga muda wa kutafakari. Kusema kweli kutafakari kulinipatia nguvu, kulinipatia upeo mkubwa wa kutambua mambo mengi katika maisha mwanadamu...? haya ni maelezo ya Mandela kutoka katika mahojiano aliyoyafanya na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC).

Mandela, anatoa mifano mingi juu ya mambo yaliyotokea gerezani na kumsaidia kutafakari kwa kina. Kuna mfungwa aliyepigwa vibaya sna kuumizwa, Mandela, hakuvumilia kitendo hicho, aliamua kwenda kulalamika kwa mkuu wa gereza.

Mfungwa huyo alipohongwa kwa kupatiwa chakula kingi zaidi ya kile alichokuwa akipata kila siku, alimgeuka Mandela, na kusema kwamba Mandela alisema uongo kwa mkuu wa gereza, maana yeye hakupigwa wala kuumizwa.

Tukio hilo na mengine mengi ya namna hiyo yalimuumiza Mandela na kumfanya kutafakari kwa undani juu ya mwanadamu, jinsi mtu anavyoweza kuhongwa ili akubali ukiukwaji wa haki zake.

Kutafakari kulimsaidia Mandela, kutoka gerezani na kuwasamehe adui zake, maana aligundua kwamba mtu unaweza kufanya kitu kwa kusukumwa na mambo mengine ambayo yako juu ya uwezo wake au wakati mwingine udhaifu wa ubinadamu.

Mzee Mandela, alijua, kwa vile hekima yake ilikuwa kubwa, kwamba binti mbichi kama alivyokuwa Winnie, kwa miaka yote hiyo 27, angeweza kuteleza lakini si kuanguka kabisa! Na hata kama alianguka, angeinuliwa na kusamehewa kama walivyosamehewa wengine wote waliotenda maovu makubwa Afrika Kusini. Kama maisha ya ndoa yangeshindikana, basi wangeishi kama mtu na dada yake kama alivyofanya Mahatma Gandhi.

Wakati wa ibada ya kitaifa ya kumuaga Mandela, dunia nzima ilimshuhudia Winnie Mandela, akimkumbatia na kumpatia busu tatu Graca Marchel. Tuna imani si kuigiza, bali huyu ni mama asiyekuwa na kinyongo wala chuki, ni mama aliyempenda Nelson Mandela kwa moyo wake wote.

Maisha ya mama huyu, mateso aliyoyapitia hadi ndoa yake kuvunjika ni ushahidi wa kutosha kwamba Mzee Mandela ni Shujaa, aliyeshindwa kuhimili changamoto za ndoa! Mungu amlaze mahali pema peponi.
 
umeongea meengi ila umesahau kuwa mama huyu alikuwa anajiachia wazi wazi na kiserengeti boy wa wakati ule.
huyo jamaaalikuwa mwanasheria.
mke wa mtu kama mandela hupaswi kuwa mzinifu.
tena wazi wazi
 
kuna mengi ya kujifunza kwa kusoma makala kama hizi.lakini c lazima ikubariki kwa vile utakavyo.
 
Umeandika vyoote ila haukugusia Mzee Mandela kupigwa na kufokewa na Winnie! Kwa akili yako ndoa ya aina hiyo ni ya kuivumilia? Au ulitaka atoke ndani na kuongea na wananchi kama kiongozi wa nchi huku akiwa na manundu ya kupondwa na mke kijana aliekuwa tayari keshaonja damu changa na nyingine alizoziua kwa ajili ya kusalitiwa? Tathmini yako haina mashiko kama hautaweka suala ilo la kupigwa alikokuwa anafanyiwa Mzee Mandela!
 
Umeandika vyoote ila haukugusia Mzee Mandela kupigwa na kufokewa na Winnie! Kwa akili yako ndoa ya aina hiyo ni ya kuivumilia? Au ulitaka atoke ndani na kuongea na wananchi kama kiongozi wa nchi huku akiwa na manundu ya kupondwa na mke kijana aliekuwa tayari keshaonja damu changa na nyingine alizoziua kwa ajili ya kusalitiwa? Tathmini yako haina mashiko kama hautaweka suala ilo la kupigwa alikokuwa anafanyiwa Mzee Mandela! Kwa taarifa mume afanyiwe vyoote lakini sio kupondwa na kudharauliwa na mke wake labda kama wewe sio mwanaume!
 
Kwa mara ya kwanza nimepata kujua kwamba Mandela alikua akipigwa hata kupata manundu, na huku akifokewa na Winnie:confused::what:
Pili jifunze kujibu kwa kujenga hoja au hata ukinukuu makala yeyote ili nasi tupate kujifunza aiseeee....
 
So, ina maana alisamehe usaliti. Then mama akaamua kumpanda kichwani baada ya kuona mabegani hapatoshi!!!

Kama ni kweli aliyosema Mjamii ni vigumu kwa mwanamme kubaki kwenye ndoa.
 
Last edited by a moderator:
Naona mtu anaweza vumilia yote lakini sio kuvumilia usaliti wa mahusiano
Ni kweli na hata biblia imeweka bayana katika kitabu cha Math 5:32 na 19:9 kuwa unaweza kumwacha mwanamke wa ndoa kwa sababu ya uzinzi tu.... Nakumbuka kuna jamaa yangu alimwekea mke wake ulinzi maana alikuwa amemshtukia kuwa si mwaminifu siku ya siku wife akazama Guest na njemba jamaa kapigiwa simu kuwa njoo sasa ushuhudie...Mwenye mke chap chap akafika wakaenda kwa dirishan kupiga chabo nasikia wife alikuwa yuko kwenye ile style ya kunyanyuliwa miguu yote miwili juu ya mabega...Jamaa ile kuona tu hivi akaanguka chini alipoteza fahamu siku nzima na kila alikuwa akizinduka anasema mama fulan chalii tena...
 
Back
Top Bottom