makahaba sasa waanza kutumia Hijab kuvutia wanaume

Jospina

JF-Expert Member
Apr 19, 2013
2,421
1,387
Makahaba katika baadhi ya sehemu za mji mkuu wa Kenya , Nairobi, wametupilia Mbali vazi la 'Mini skirt na kuanza kutumia Hijab kama njia ya kuwavutia wateja wao, jambo ambalo limekashifiwa vikali na wakuu wa dini ya Kiislamu.
Hijab huvaliwa na wanawake wa Kiislamu kama ishara ya kumcha Mungu, lakini makahaba katika mtaa wa Eastleigh, viungani mwa Nairobi wanatumia Hijab ili kuwafanya wateja wao kudhania kua wanatoka sehemu za Pwani.
Mwanamke mmoja ambaye hakutaka kutaja jina lake alisema kuwa yeye hupata wateja maradufu kwani huvalia vazi hilo la Hijab, wengi wa wateja wake wakimuona kama mwenye nidhamu.
Uchunguzi ulibaini kuwa wanawake wasio wa kiislamu wanavalia vazi hilo ili kuwavutia wanaume ambao wanaamini kuwa wao wana maadili zaidi ya wale wanaovalia nguo fupi au 'Mini Skirt'.
kwa upande mwingine chama cha makahaba nchini Kenya kimewatetea makahaba hao wanaotumia hijab huku likidai kwamba wanafanya hivyo ili kukidhi mahitaji ya wateja wao:
nini maoni yako mwana MMU??
 
Back
Top Bottom