Makafara katika ujenzi wa magorofa

Makafara katika ujenzi wa magorofa

Yaani jamaa kama ulikuwepo vile kuna mjengo unajengwa hapa, fundi 1 keshafariki na mwingine juzi kanusurika baada ya kuporomoka na kung'oka meno mawili ya chini na kuteguka kiuona.
 
mshana jr tupe ilim kidogo kuhusu kafara zinazofanyika ktk ujenzi wa madaraja makubwa.

hasa yale yaliyo katiza ktk mito mikubwa na bahari,mfano like la kigamboni na mengine duniani.kuna hadithi nyingi sana za ajabu kuhusu ujenzi wa hayo "madude". funguka mkuu.

kwanini mengi hujengwa usiku wa manane?.unaamka asubuhi unakuta bimu zishapanda....wiki,mwezi,miezi Mara dude hilo lishakamilika,lakini hujui lini na saa ngapi walikamilisha hiki na mile.
 
Last edited by a moderator:
mshana jr tupe ilim kidogo kuhusu kafara zinazofanyika ktk ujenzi wa madaraja makubwa.

hasa yale yaliyo katiza ktk mito mikubwa na bahari,mfano like la kigamboni na mengine duniani.kuna hadithi nyingi sana za ajabu kuhusu ujenzi wa hayo "madude". funguka mkuu.

kwanini mengi hujengwa usiku wa manane?.unaamka asubuhi unakuta bimu zishapanda....wiki,mwezi,miezi Mara dude hilo lishakamilika,lakini hujui lini na saa ngapi walikamilisha hiki na mile.

Usijali stay tuned...!!! Topic yake coming soon
 
Last edited by a moderator:
Mtu asikudanganye, dunia hii ina pande mbili ulimwengu tunauona na ule tunauhisi/ hatuuoni. lakini hizi zote zinafanya kazi kwa kutegemeana, mambo yote yanaanza kufanyika kwenye ulimwengu tusiouna kwanza halafu matokeo yake ndiyo tunayaona mwilini, yaani phyisical world. mtu akipata kitu alikipata kizuri au kibaya, kilikuwepo rohoni kwanza ndipo kikaja mwili.

Wapo wanaoona mambo haya, wachawi waganga wa kienyeji, watakatifu, baadhi ya viongozi wa dini zenye muunganiko wa kweli na Mungu wanaona.Hivyo ndiyo maana ni rahisi kumwambia mtu fanya hivi au hivi utashinda. mfano anayesema chumvi na mfupa wakitimoto alipata wapi hayo maneno? lazima aliambiawa na waona fahamu eimu hii. ni elimu njema kuijua maana ndiyo chimbuko la kufanikiwa kwetu.

Mtu akikwambia uongo mambo haya hayapo. either yeye anafaidika na upande huo na hataki wewe ujue ili usimpinge, au hajui kwa maana ni kipofu au anatumiwa aseme hivyo ili usifahamu. Kwa kawaidaa binadamu akifahamu kitu ukombozi unakaribia maana ataanza kupambani ili atoke, hivyo anayefaidika na ujinga wako hatapenda ujue ukweli.

Ndoto ni kigezo kikubwa cha kujua upande ulioko, kama unaota mabaya tu ujue jambo baya lipo upenuni linakuja, na kama unaota mema, ujue pia jambo jema lipo upenuni linakuja pia. ukiwa na maarifa unaweza kuyapinga mabaya na yasije, na ukiwa na maarifa unaweza kuyaita mema na yakaja.

Hivyo ni vyema sana kutafuta nafsi na kujifunza juu ya jambo hili kwani ndimo ufanisi wa ubinadamu ulimo. Kuna watu wamejaliwa kabisa wanaona mambo haya, japo inaweza kuwa kwa kipindi fulani kisha uwezo unapotea kulingana na alivyo jipanda na source ya uwezo huo.
 
Utakuwa "mshirikina" si bure. News zako nyingi nizahivihivi . Badilika Bro . Usituharibie Birthday ya Yesu .
 
Ni jambo la kificho mno, lisilojulikana na wengine wengi lakini ukweli ni kwamba magorofa mengi uyaonayo yana roho za watu au imevunja mifupa ya watu kwa njia za ajali au yamekunywa damu ya kikafara
Si mara zote wafanyao mambo haya ni wamiliki la hasha bali mambo haya hufanywa pia na wakandarasi na hata waliopewa tenda mbali mbali kwenye site husika... Nia na lengo ni moja tuu kupata zaidi au kujikinga kishirikina
Kama tungekuwa na takwimu za kitaifa si ajabu kati ya kila magorofa kumi saba yamesababisha maafa vilema na makovu... Hili jambo lina level zake kuanzia kutoa kafara dogo la mtu mmoja mpaka ibada za makafara zifanywazo na makandarasi wakubwa kufikia viwango vya freemason
Ndio maana kwenye ujenzi wa mahekalu makubwa ya ibada hufanyika ibada maalum za kumwomba Mungu aepushe mbali mabaya yote kwenye ujenzi husika mpaka mwisho wa ujenzi wake.
Hata wewe kwa kutambua hili fanya hivyo kwenye ujenzi wako hata kama si ghorofa ili nyumba yako isije kuwa ni chanzo cha mabalaa na mitihani ya dunia
mshana jr Wakati Upo Mdogo Ulishawahi Kutamani Kuja Kuwa Mganga? Ndani Ya Wiki 2 Huu Nadhani Ni UZI Wako Wa Pili Wa Masuala Ya USHIRIKINA. Kulikoni Mkuu Kama Vipi Tuweke Wazi Kama Nawe UMEBOBEA Ktk Kamati Za UFUNDI Ili Nami Nije Unitengenezee Dawa Magu Aniteue Ubunge Wa Ghafla.
 
Last edited by a moderator:
Mh....
Niliwahi uliza wakuu enzi hizo nikiwa kid, wao wakinunua site walikuwa wakiitest kwa kupanda chochote kama mbojo au maharage... Vingine sijui maana sijawahi hata kufikiri hayo.. Zingine naziona ni ajali za kawaida
 
Damu ya yesu inapatikana wapi msaada pls

amini katika bwana yesu na unapoanza ujenzi sali na na kuomba nuru ya bwana wetu yesu kristo na damu yake iliyomwagika msalabani itawale eneo lako nakuhakikishia hakuna mchawi wala nguvu ya giza zitakushinda
 
mshana jr Wakati Upo Mdogo Ulishawahi Kutamani Kuja Kuwa Mganga? Ndani Ya Wiki 2 Huu Nadhani Ni UZI Wako Wa Pili Wa Masuala Ya USHIRIKINA. Kulikoni Mkuu Kama Vipi Tuweke Wazi Kama Nawe UMEBOBEA Ktk Kamati Za UFUNDI Ili Nami Nije Unitengenezee Dawa Magu Aniteue Ubunge Wa Ghafla.

Ndani ya wiki 2? Sio mbili tuu ziko zaidi ya nne... Masharti ya kupata ubunge utayaweza???
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom