Makada wa CCM waongoza kwa wizi na Uhujumu wa Umeme Tanesco!!

Ngaliba Dume

JF-Expert Member
Oct 6, 2010
1,710
3,669
Siku chache baada ya Waziri wa Nishati "kumlipua" mmiliki wa St.Mary's Sec. School ambaye ni Mbunge wa Viti Maalumu(CCM) Mch.Rwakatare kuwa ni mwizi sugu wa umeme na uhujumu wa miundo mbinu ya Tanesco kama "Mita" za Luku n.k,hali hiyo imejitokeza tena kwa kada mwingine CCM.

Jana ktk kuongea na vyombo vya Habari,Maafisa wa Tanesco wamemtaja Ndugu Julian Bujugo mmiliki wa Shule za Green Acres kuwa ni miongoni mwa wezi sugu wa umeme na uhujumu wa miundombinu ya Tanesco...na kuwa ndugu Bujugo ameeibia Tanesco umeme kwa kujiunganishia umeme toka mwaka 2005 na hivyo kudaiwa mabilioni ya fedha ktk shule ya Green Acres-Salasala(DSM)

Itakumbukwa kuwa Mh.JULIAN BUJUGO ni diwani wa kata ya Magomeni na anahusika na uuzaji wa eneo la wazi (Open Space) la Magomeni lililo pembeni ya Magomeni kanisani..mpaka sasa ukipita pale Bustan ya Magomeni kuna Bar ya Wazi imefunguliwa ndani ya hiyo Open Space. Ukifuatilia utajua,Viongozi au makada wengi wa CCM wanaomiliki baadhi ya taasisi mbali mbali,wanatumia vyeo vyao na nafasi zao kuiba umeme,na wanatumia network yao kuwatisha watumishi wa TANESCO.
 
Ngalibadume ccm ni mafisi kila kitu wao ni safishasafisha
 
Last edited by a moderator:
Mi nasubiri waje kwanza masalia ya ccm hapa jf wakina ritz ,rejeo then nitarudi
 
Ndio maana baada ya uchaguzi 2015, kazi ya kwanza ni kusafisha nyumba kwa kuangamiza wadudu wote waharibifu kama mende, panya, mbu nk i.e. CCM .

Farijala Hussein (fisadi wa EPA) na huyu Bujugo ni mifano midogo na rahisi yenye kuwakilisha taswira pana na sahihi ya CCM.
 
Walishaambiwa wakitaka biashara zao zisibuguziwe wapeperushe bendera ya Kijani!

Jamaa ni kati ya Wafadhili wakuu wa CCM. Uchaguzi wa 2010 aliwabeba sana CCM na kwa kauli yake mwenyewe anasema ametumia zaidiya 450m. Madiwani wengi amewawekakwa fedha zake maana alikuwa agombee umeyawa Dar kabla ya kutoswa. Nape angeanza na watu kama hao ambao wanafadhili CCM kwa fedha chafu!
 
Tutasikia mengi kuhusu ccm na mafisadi wake mpaka masikio yetu yapasuke
 
Mi nasubiri waje kwanza masalia ya CCM hapa Jf wakina ritz ,rejeo then nitarudi.
Asubuhi leo wakati radio clouds wanasoma magazeti, pamoja na hiyo shule kuna vituo kadhaa vya mafuta vilivyobobea kwa wizi huo wa umeme, lakini gazeti liliogopa kuvitaja kwa majina, nadhani mmiliki wake kama sio mtoto basi ni Mshua ndio maana wakabana majina yake.
 
CCM sio tu wezi kwenye umeme bali kila nyanja wanafanya hivyo, kwenye maji, maliasili, nk.
 
Back
Top Bottom