Makabila zaidi ya 128 yanayopatikana Tanzania Bara

Ingefaa iyo list ya makabila iambatane na sehemu wanakotoka mf;

Wachaga --Moshi kilimanjaro
Wamasai --Arusha
Wambulu --Karatu
--
--
--
 
Wahutu, waha na wahangaza Wana asili moja, lkn makabila tofauti..alieleta ukoloni na mipaka alaaniwe
 
Kwa muda mrefu sana nimekuwa nikijiuliza kama kweli Tanzania ina jumla ya makabila mia ishirini.Kwa hesabu zangu sijawahi kufikisha hata hiyo mia bila baadhi ya makabila kujirudia,.

Je kuna ukweli katika dhana hiyo kama tulivyokaririshwa tangu tukiwa wadogo?.

Nawaomba wanaforum tufikiri kwa pamoja na tujaribu kuyataja makabila ya Tanzania 120 ili tuweke takwimu sawa.

Naomba kuwasilisha.

------------------------

Haya hapa mkuu, Ila Nyerere alikataza ukabila na umimi.


Waalagwa (pia wanaitwa Wasi)
Waakiek
Waarusha
Waassa
Wabarabaig
Wabembe
Wabena
Wabende
Wabondei
Wabungu (au Wawungu)
Waburunge
Wachagga
Wadatoga
Wadhaiso
Wadigo
Wadoe
Wafipa
Wagogo
Wagorowa (pia wanaitwa Wafiome)
Wagweno
Waha
Wahadzabe (pia wanaitwa Watindiga)
Wahangaza
Wahaya
Wahehe
Waikizu
Waikoma
Wairaqw (pia wanaitwa Wambulu)
Waisanzu
Wajiji
Wajita
Wakabwa
Wakaguru
Wakahe
Wakami
Wakara (pia wanaitwa Waregi)
Wakerewe
Wakimbu
Wakinga
Wakisankasa
Wakisi
Wakonongo
Wakuria
Wakutu
Wakw'adza
Wakwavi
Wakwaya
Wakwere (pia wanaitwa Wanghwele)
Wakwifa
Walambya
Waluguru
Waluo
Wamaasai
Wamachinga
Wamagoma
Wamakonde
Wamakua (au Wamakhuwa)
Wamakwe (pia wanaitwa Wamaraba)
Wamalila
Wamambwe
Wamanda
Wamatengo
Wamatumbi
Wamaviha
Wambugwe
Wambunga
Wamosiro
Wampoto
Wamwanga
Wamwera
Wandali
Wandamba
Wandendeule
Wandengereko
Wandonde
Wangasa
Wangindo
Wangoni
Wangulu
Wangurimi (au Wangoreme)
Wanilamba (au Wanyiramba)
Wanindi
Wanyakyusa
Wanyambo
Wanyamwanga
Wanyamwezi
Wanyanyembe
Wanyaturu (pia wanaitwa Warimi)
Wanyiha
Wapangwa
Wapare (pia wanaitwa Wasu)
Wapimbwe
Wapogolo
Warangi (au Walangi)
Warufiji
Warungi
Warungu (au Walungu)
Warungwa
Warwa
Wasafwa
Wasagara
Wasandawe
Wasangu (Tanzania)
Wasegeju
Washambaa
Washubi
Wasizaki
Wasuba
Wasukuma
Wasumbwa
Waswahili
Watemi (pia wanaitwa Wasonjo)
Watongwe
Watumbuka
Wavidunda
Wavinza
Wawanda
Wawanji
Waware (inaaminika lugha yao imekufa)
Wayao
Wazanaki
Wazaramo
Wazigula
Wazinza
Wazyoba

Hakuna kabila linaloitwa " waarusha " usitudanganye sisi hapa.

Moja ya utambulisho wa kabila ni Lugha (Kila kabila lina lugha yake) sasa nambie uliwahi kuona ama kusikia wapo watu wazungumza lugha ambayo inaitwa ki-arusha

Cha kuku saidia tu ili uelewe ni kwamba hao unaosema wanaitwa waarusha huwa wanazungumza kiswahili ila lugha yao ya kikabila kabisa hawana kwa hiyo huwezi sema wale ni kabila wakati hawana lugha yao ya kikabila .

Nimeishi Arusha kwa mda mwingi tu nimechangamana na watu wa makabila kadhaa kama wamasai n.k ila nikwambie tu kwamba hao unaowaita "Waarusha" huwa siyo kabila bali ni jamii tu flani ambayo kwa asili ni wamasai.

Yani kwa kifupi tunawaita ni wamasai waliozaliwa na kukulia mjini na mara nyingi unakuta hata kimasai hawajui kukizungumza kwa sababu wamezaliwa mjini na kukulia mjini kwa hiyo wanajikuta wanajua kiswahili kama lugha yao ya kwanza na ndo hao wanajjita waarusha ila ki asili kabisa ni wamasai
 
Kuna makabila mwawili yameongezeka tanzania kuna wahutu na watudi wakimbixi zaidi ya laki mbili ambao walipewa uraia wa Tanzania waliokuwa wanaishi makambini kwa miaka mingi kupewa uraia kwao kulitangazea na vyombo vyetu vya habari
 
Kuna makabila mwawili yameongezeka tanzania kuna wahutu na watudi wakimbixi zaidi ya laki mbili ambao walipewa uraia wa Tanzania waliokuwa wanaishi makambini kwa miaka mingi kupewa uraia kwao kulitangazea na vyombo vyetu vya habari
kwakweli, walikuwa Katavi na Tabora.
 
Back
Top Bottom