Habari za leo wapendwa. Mwenzenu natafuta mchumba ili nioe ila nataka kujua Tabia za wanawake wa KISUKUMA. Mimi mwenyewe ni mzaramo wa Chamazi
Mkuu Francis Jr,
1.Kwa vile Wasukuma ndilo kabila kubwa kabisa nchini Tanzania, inamaanisha kuwa, kati ya wanawake wote Tanzania,
wanawake wa Kisukuma ndio wengi kuliko wanawake wengine wote!.
2. Kabila la Wasukuma, ni miongoni mwa makabila yanye orgin ya "communal by nature", kila jambo hufanywa kwa
upendo, umoja, uchangamfu, ukarimu, uchapakazi na ushirikiano wa hali ya juu, hivyo tabia kama
uchoyo ni aghlabu sana!.
3. Kufuatia Wanaume wa Kisukuma wale "chapa ng'ombe original", kuwa na nguvu sana, "poligamous relationships" ndio jadi yao, hivyo wanawake wa Kisukuma, hawatatizwi na tatizo kuu la wanawake wengi linaloitwa "
wivu"!.
4. Kufuatia wanaume wa Kisukuma ndio wanaoongoza kwa kupenda nchini kuliko wanaume wa makabila mengine yote, then automatically, wanawake wa Kisukuma wanategemea
kupendwa kiukweli katika kila idara, kitu ambacho itakuwa ni kazi kidogo ya ziada kwa Mzaramo.
5. Kufuatia kabila la Wasukuma kuwa ni la watu wanaoridhika sana, hivyo mwanamke wa Kisukuma ni mwanamke wa
kuridhika na hali yoyote uliyonayo,
hawana makuuu,
hawana tamaa na ni
wavumilivu na
wastahimilivu wa hali ya juu, hali ikiwa nzuri, hawajidai na hali ikiwa mbaya, anakaanga hata maji tuu na mnalalia, na hata ukiwa mtupu kabisa, analalia hewa kwa furaha kabisa na huduma nyingine zote kama kawa!.
6. Kufuatia Wasukuma kuwa ni familia za wake wengi na watoto wengi, the idadi ya watoto sio tatizo kwa mke wa Kisukuma, ikitokea unao hata wale wa majaribio, wewe walete tuu na kuwakabidhi
watapendwa bila ubaguzi wowote, na hata wakitokea wengine wa kona kona, kesi zake sio kubwa sana, hii inamaanisha wana
upendo wa dhati kwa wote!.
7. Kufuatia kuwa na maumbo ya shibe shibe, wewe you are expected uwe mtu wa shibe shibe katika nguvu za mwili, hatupendi dada zetu hawa kulazwa na njaa, ila pia ni waaminifu sana, hata ikitokea kumlaza njaa, bado atavumilia tuu bila kuchepuka, kufuatia uwezo mkubwa wa
ustahimilivu na
uvumilivu ila yakitokea mazingira ya mchezo wa "boxing"
usimtarajie atakuwa "punching bag" kama walivyo wanawake wengine, yeye atakuwa ni "opponent"!.
8. Kufuatia Kabila la Wasukuma kuwa ni "poliygamous" in nature, then wanaume wao ni watu wa "wengi" hivyo "problem ya the other woman" is not a big deal kwa mwanamke wa Kisukuma, hutahatarisha kabisa ndoa yako.
9. Kufuatia Wasukuma kupenda kujumuika pamoja kwenye good times na bad times, wanawake wao ni watu wa kujichanganya sana, na kwa vile Wasukuma ni ma spender wazuri, jitahidi usimletee ubahili wa Kizararamo, ukiwa nazo zitumie, zikiisha ataelewa tuu!.
10. Kwa vile Wasukuma ni watu wa
upendo na
amani wakati wate, tegemea mke wako atakuwa at peace all the time, hapendi maneno maneno na ghubu la aina yoyote, likitokea jambo likiisha limeisha, hivyo wewe kama Mzaramo ni watu wa kuchonga sana, itakubidi ubadilike!.
Natumaini umepata mawili matatu ya kukusaidia.
Pasco.