Makabila ya wasanii na watu maarufu wa Bongo

Mkuu inategemea na kabila. Kuna patrilineal na matrilineal commnunities.
Patrilineal communities, mfano watu wa bara na jamii nyingi za wafugaji, mtoto ni wa baba. Hata urithi unaenda kwa mtoto wa kwanza wa kiume. Mtoto wa kwanza anarithi mali (ardhi, mifugo) ambayo kwa kizazi hiki hizo mali hazipo, lakini pia anakuwa na jukumu la kutunza wadogo zake wote mfano kuoza/ kuozesha, kusomesha etc. Hata dada akiachika anarudi nyumbani kwa kaka mkubwa.

Matrilineal community mfano Luguru, Yao, Makonde, Mwera (I stand to be corrected), hawa ukoo/ ubin unakuwa upande wa mama. Mjomba ndio ana nguvu kwa mtoto. Binti akiolewa yeye ndio muamuzi mkuu na mahari anapanga yeye. Mwanaume kama ana mali, urithi unatakiwa kwenda kwa mtoto wa kiume wa dada na siyo mtoto wake wa ndoa. Mtoto wa kiume wa mwanume atarithi vya mjomba wake. Ulishasikia ule wimbo wa zilipendwa, mjomba amechachamaa amekuja juu harusini.....ndio hayo mambo ya Matrilineal community.

Katika kazi zangu, niliwahi kukutana na famila ambayo watoto baba ni Luguru na mama wa bara. Wale watoto waliniambia wakienda kwa mama bara ni kama wameenda kutembea tu maana kwa baba ni uluguruni, wanajulikana siyo kwao. Wakienda kwa baba pia wanajulikana wao ni wa bara huko ujombani.

Cultural barriers nilikutana nayo pia kwa mahari yangu. baba Sukuma mama wa Pwani and Tanga. Wajomba wakataka kupanga mahari na kuwa vinara wa shughuli. Baba akawaambia kwa wasukuma, huyu ni mtoto wangu siyo wenu. Kama wa kwenu, mbona hamkumsomesha. Pia nilivyovunja ungo baadhi ya ndugu wa pwani walitaka kuniweka mwali na kunicheza ngoma ili wanizawadie kanga na vitenge, Dingi akawagomea.

I am proud of my Dad kwa kweli hasa upande wa mama walipokuwa wanataka nijifunze kuhudumia mume na familia, baba anasema muacheni mwanangu asome. Mpaka leo huwa nawaambia uncles mimi ni msukuma siyo wa huko kwenu.

Baba yako kwa sababu anazozijui yeye amekupotosha..Mjomba kuwa na nguvu kwa hayo maeneo ni katika ushauri na malezi tu ktk kumsaidia dada yao na haina uhusiano na urithi or something..wewe kuwa msukuma ni haki yako !! .. inaoenekana umekuzwa ku hate upande wa mama... .!! .. na hilo ndio tatizo la wasukuma!..
 
#Diamond na Ali Kiba: Almost every body know about them

1. Sugu ( Joseph Mbilinyi) - Mkinga
2. Professor Jay (Joseph Haule ) - Mngoni
3. Lady Jay Dee ( Judith Wambura Mbibo) - Mkurya
4. Inspector Haroun - Msukuma/ Mzaramo (Baba ake na Haruna marehemu Mzee Rashid Juma Kahena alilowea uzaramuni " Kisarawe vijijini" miaka ya sitini, akaoa Mzaramo ( mama Zena/ mama ake Haruna) then baadae akahamia Kisarawe mjini then Temeke. Kwa miaka yote aliyo kaa uzaramuni Mzee huyu alijikuta akiwa ame integrate kwenye uzaramuni.

5. Luteni Kalama (Kalama Bakar) - Mzaramo.
6. Juma Nature (Juma Kassim Kiroboto) - Mzaramo/ Mngindo.
7. Solo Thang (Msafiri Kondo) - Mzaramo.
8. Tid (Khalid Mohamed) - Mmakonde (but anadai ana asili ya ungazija)
9. Jay Moe (Juma Mohamed Mchopanga)....Mmakonde.
10. Mr. Blue (Heri Sameer) - mama Mzaramo wa Mlandizi Baba Msudani.
11. Chid Beenz (Rashid Abdallah Makwiro) - Baba wa Tanga (probably Mzigua au Mdigo) mama wa Iringa probably Mhehe.
12.Lord Eyes - Baba Mjita mama mchaga.
13. JCB (Jacob Makala) - Msukuma.
14. Wema Sepetu - Mama mtu wa Singida, Baba Mnyamwezi.
15. Hamisa Mobeto - Mnyamwezi.
16. Swebe - Mnyamwezi.
17. Dyna Nyange - Mrangi.
18. Jux - Mmakonde.

Endelea kuiririka na wewe
G-nako?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waha hujiita wamanyema, hawapendi waitwe waha
Sheta -mngoni
Gelly wa rhymes-mngoni
Godzilla (r.i.p)-mngoni
Izo b-nyakyusa
Gigy-nyakyusa
Lulu diva-mpare
Marioo-mndengereko
Alikiba-manyema
Diamond-manyema
Mboso-mndengereko
Ruby-wa tanga(Sasa sijui kabila gani)
Nandy-mchaga
Maua sama-mchaga
Linasanga-m'bena


Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dokii- mjita kotekote kwa baba na Mama aliishi Musoma Kamunyonyonge kasoma musoma alizaliwa Kendu bay Kenya

Maringo- Musoma Kamunyonge!

JIrambwene- Mugango-kwibara

Diamond- kigoma baba mruri
Wakati rich mavoko na uyo uliyemtaja ni blood kabisa, sasa rich mavoko ni kutoka morogoro au unababaika na lafudhi ya kikenya? Masanja ukoo wake ni Mgaya ambao ni wahehe.

Nafikiri umenisoma hapo
 
Msaga sumu -Mmawiya
Mrisho mpoto - Mmalaba
20% - Mmawiya
Harmonize - uchicheme uchi mumunye
Mzee WA BWAX - msukupai
Shetta - mnachilingo
Marioo - shirshama
Jay melody - wa2 wa Kwny apocalypse ya Jaguar
Rayvanny - mnyakusa
AY - mmakonde pure
KR - naluhokwe
Ferooz - naluhokwe
Meja kunta - mmapengo
 
Mtoto wa Dandu dah!

Na mapigo yake ya kiKofi Olomide na korasi yake ile:

Kolobelaga lukumo lwane
Jaga ng'wigulya
Jaga ubagisha shikamoo
Abakolobela ng'weli..

Halafu anakupa....

Ng'wanamalia.
Nabiza wagalama
Nulunagaja gubugeni nadiko gwigashiji gogo
Mpaka lisumbe lyang'hana...

Apumzike kwa amani Mtoto wa Dandu. Angekuwepo sijui angefika wapi...
Umenichekesha sanaa brother, umenikumbusha kitambo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom