Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 359,882
- 828,451
''Sina wa kumlaumu,niilijipoteza mwenyewe, Kwa sehemu kubwa Jamii hainitazami tena kwa jicho la Usaidizi, Jamii inanitazama kama Mlevi au Teja,Lakini pengine Mimi ni Mfano hai unaoweza kutumika kusaidia kizazi kingine kinachoteketea kimya kimya. Nilikuwa Msanii Pekee wa Hip Hop niliyekuwa Hot kiasi kwamba nikashirikishwa mpaka kwenye nyimbo za Bolingo…
kumbuka FM Academia!…haikuwa ajabu Mimi kufanya Show India Jukwaa moja na P Square , Haikuwa ajabu Katika Fietsa Concert tour Mimi kuwa na Msafara wangu Binafsi wa Magari wakati wasanii wengine wote wakiwa kwenye Isuzu jorney na Costa, Hayo yote ninayozungumza si kwa Lengo la kujisifu la hasha!...watu watasema mengi lakini naumia kuona nipo hivi leo..naumia kwa Ulevi niliouingia...ulevi ambao mara kadhaa nimejaribu kuuacha..
.Ulevi huu ni Pingu, leo King Kong Mwili Jumba nimebaki na Mwili huu? niseme tu wazi sisi kama wasanii hujaribu vilevi vingi hasa pale tunapokuwa Hot na fedha inaingia...kumbuka wasanii muda wote ni watu wa safari na show,...wengi tunashindwa kuji-manage na Starehe...Maisha yanayotuzunguka hutulevya..Maisha ya vilevi na wapambe.
Mimi nimewahi kulipiwa Mamilioni na watu mbalimbali kwa upendo tu ili kupata Rahabilitation kutoka katika kifungo hiki lakini nikabaki kwenye ulevi ule ule. Nakumbuka mwanzoni mwa mwaka 2015 siku moja wakati nipo Maisha Club Basement alikuja Mtu Mmoja nisiyemjua akaniambia "Chidy hii si sawa...Chidy umekwisha, Mimi ni Mshabiki wako..Afya yako inatisha...tafadhali chukua hii namba kesho nipigie nione namna ya kukusaidia" Basi kesho yake nikampigia simu yule jamaa,.alichofanya ni kunichukua na kunipeleka Sober House (Pemba)...akalipa Gharama zote.
Sasa wakati nipo Pemba kuna pesa zangu za kazi ya Muziki ziliingia ilikuwa kipindi cha Uchaguzi Mkuu..Millions of Money...kwa kweli ilitaka sana Moyo kwa mtu mwenye Addiction kama mimi kuvumilia kukaa Sober House while huko nje kuna Milioni zangu kadhaa...Nikaondoka Rehab kwa lazima...hii ilikuwa sawa na mgonjwa anatoroka Dozi hospitali....nikarudi Jijini....jijini Dar es Salaam nikakutana na Mamilioni yangu, Washkaji, Vileo na Wapambe...nikaanza bata...nikarejea kwenye ulevi wa vilevi vyote kikiwemo kile kikuu kinachoniangamiza....home sikukaa, nilikaa hotel..nikatumia....kiasi cha fedha nilipeleka kwenye Ujenzi ambao haukufika mbali...leo nazungumza hapa zimekwisha zote…..Maisha haya sio sifa bali ni utumwa....utumwa ambao sishauri mtu mwingine kujaribu kujiingiza...Brother hata wewe usije ukajaribu kamwe...huu ni utumwa mkuu kuliko Minyororo ya Mjerumani.
Mimi ni Muhanga mmoja hadharani lakini kuna maelfu wako Gizani....Nyinyi mmepata Fursa ya kuniona Mimi Chidy kwa sababu nilikuwa maarufu na mwenye impact ktk sanaa na Jamii...je vipi kuhusu wale wasijulikana, wasio maarufu na wanahitaji Msaada?. Narudia, kipo kizazi kinachoendelea kuteketea kimya kimya bila Awareness yeyote, na lipo daraja linalonufaika na hali hiyo'- Chidy Benz (Katika Mahojiano na Saint Pio).
Credit: Pio Pius
s