Majukumu ya mwanaume kwa mwanamke

Majukumu ya mwanaume kwa mwanamke

Ikiwa huoni faida kwa ya kuwa na watoto basi afya ya akili yako imeyumba.

Wewe pia ni mtoto kwa baba yako, je umewahi kusikia baba yako akiropoka kuwa haoni faida ya kuwa na mtoto kama mr pipa?
sio baba mwenyewe mtoto najiona sina faida kwa baba kwasababu sina msaada wababa ipo siku tutasema KATAA WATOTO haiwezekani unalisomesha litoto linakuwa na kazi linaoa pesa yote anakula mkewe mi mzee naambulia laki tena kwa kuomba kwa miez mitatu mara moja yote haya kisa ujinga wa mama kumwambia baba hajakulea, baba alikuwa ananipiga, mwisho wa siku litoto kwa upumbavu wake linagoma kumdhingatia ding matokeo yake uzee unafika baba anabaki mwenyewe sasa nahoji tena kunafaida gani kuwa na watoto wanaume wekezen mbele pesa iwasaidie ukitegemea mitoto utakuja kujuta mitoto yenyewe muda wowote inaweza kukugeuka ikuue irithi mali!! broo ulisikia wap dingi kajengewa nyumba na watoto wake? Pia niambie ni mtu gan maarufu kamtrendisha baba yake hapa bongo
 
Hongera Sana mkuu kwa kutuelimisha.Tuishi humo jamani.
 
unachapiwa mkeo mchana kweupe what hell is this....!!!!
Ukichapiwa mkeo huo ni uzembe wako mwenyewe kaka, jiulize kipi kitamfanya mkeo amvulie chupi mwanaume mwingine, hapo itakuwa ni wewe kuzembea ktk majukumu yako.
 
Hujui nguvu ya maombi wewe, naweza tamka neno hapa na mashine yako ikazima mazima, uwe na adabu kwa nyuzi za watumishi waombaji hapa sio pa kutafutia pisi kijana.
Umeanza vizuri but naona unajichanganya huku kwenye comments.

Napata wasiwasi hata hili bandiko umecopy sehemu, siyo akili yako ya kuwajibu ujinga watu humu kama ninavyokufahamu itakuwa ndo imeandika huu uzi.
 
Majamaa wa huku mnafeli padogo sana, Haya huyo mke unaemzungumzia kwenye maandiko ndo hawa ambao wanavaa mavazi ya ajabu?, ndo hawa wenye tamaa kuzidi fisi, Ndo hawa waliokosa uvumilivu, Ndo hawa wanaopenda maisha ya kushindana na wenzao?, Je ndo hawa ambao hawajiamini maana kila kitu kwao ni feki (Makalio,Kucha,Kope n.k), Ndo hawa ambao hawana haya wala hofu ya Mungu? Ukiongelea kulinganisha maandiko na hivi sasa usiangalie upande mmoja ukidhani upande mwingine utakupenda.... Inapofika suala la wajibu kila mmoja ana wajibu wake hata hayo maandiko hamna sehemu yamesema mwanaume ndo atafute hela peke yake ili aje ampe mwanamke... Kila mmoja ana wajibu wa kubeba madhaifu ya mwingine, Waliitwa wasidizi ili waje kusaidia popote panapohitaji msaada na sio kufua na kupika pekee bali hata kujenga uchumi wa familia.
 
Unapokuwa kwa myunani ongea kama myunani ili muende sawa, comments za mtu wa mataifa zitajibiwa kimataifa, hii ni kanuni ya kimishenari, hakuna majibu ya kijinga hapa bali tunawekana sawa kinamna na wasio sawa kwa kuwa kama wao.
 
2. Kutoa hela kwa mkewe
Mungu anaamuru kila mtu kutunza familia yake (1 Tim 5:8). Waume lazima tutoe hela. Kuna wakati mke wako anaweza kukusaidia katika mzigo wa kifedha wa familia, mkeo anaposaidia majukumu usiketi kwenye kitanda chako ama kulala mchana amka mapema katafute hela.
Haya ndiyo yanatufanya tudharaulike na watoto wetu uzeeni, wanamuona mama yao ndiyo kila kitu misaada yote wanaelekeza huko kumbe mama yao aliwapa hela niliyotafuta mimi baba yao
 
Majamaa wa huku mnafeli padogo sana, Haya huyo mke unaemzungumzia kwenye maandiko ndo hawa ambao wanavaa mavazi ya ajabu?, ndo hawa wenye tamaa kuzidi fisi, Ndo hawa waliokosa uvumilivu, Ndo hawa wanaopenda maisha ya kushindana na wenzao?, Je ndo hawa ambao hawajiamini maana kila kitu kwao ni feki (Makalio,Kucha,Kope n.k), Ndo hawa ambao hawana haya wala hofu ya Mungu? Ukiongelea kulinganisha maandiko na hivi sasa usiangalie upande mmoja ukidhani upande mwingine utakupenda.... Inapofika suala la wajibu kila mmoja ana wajibu wake hata hayo maandiko hamna sehemu yamesema mwanaume ndo atafute hela peke yake ili aje ampe mwanamke... Kila mmoja ana wajibu wa kubeba madhaifu ya mwingine, Waliitwa wasidizi ili waje kusaidia popote panapohitaji msaada na sio kufua na kupika pekee bali hata kujenga uchumi wa familia.
Huyo demu uliyekutana naye nightclub akakuvutia kwa makalio ya bandia kucha za kubandika, kope za bandia kisha ukamchukua na kumpeleka kwa apartment yako na kumuoa usiku huo huo, uliyakanyaga kijana.

Kuna mke mwema na kuna mke mwovu.

Biblia inamwelezea vizuri sana wapi anatoka huyo mke mwema.

Sikatai wapo wanawake wengi sana wenye tabia ulizo orodhesha nakazia kabisa wapo na ni wavurugaji nguli .

Lakini kwa upande mwingine wapo wasio na hizo tabia hivyo usijumlishe kila mwanamke ni wa kundi lililokuvuruga, mke mwema hutoka kwa BWANA
 
Haya ndiyo yanatufanya tudharaulike na watoto wetu uzeeni,
Tatizo la kudharaulika mara nyingi wanaume hujisababishia wenyewe kwa kutuma tu hela pasipo kukaa karibu na watoto.

Jifunze ujanani kukaa karibu na watoto wako na hawatakudharau huko uzeeni
 
Ukikaa na familia fedha itakufuata hapo ulipokaa kiongozi?
Sijamaanisha ushinde na watoto home, bali namaanisha uwe na muda maalum baada ya kazi urudi nyumbani mapema ucheze na vitoto vyako vikuzoee na vikikua vitakuheshimu hata ukiwa mzee uliyefulia uzeeni.

Niamini vitakubeba.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom