Majukumu ya mwanamke kwenye ndoa ni yapi?

Ahsante Sana
 
Ni kupika,kupeana raha ,kuzaa,kufua nunua mashine ya kufulia huna hela tafuta mtu wa kufua.
Niliwahi kuwa na Star mmoja wa Bongo enzi za nyuma akiwa na washkaji na marafiki zake aisee huwezi hata kumtamani. Anayoongea kwa nyodo na dharau alikuwa anatisha hadi wanaume walimuogopa. Akiwa mitandaoni ndio kabisa. Yeye anasema kwanza hawezi kuwa na mwanaume asiye na pesa. Pili anasema swala la kuolewa kwake sio option na hata akiolewa hataki upumbavu wa kuambiwa kupikia familia wala kufua au kuchota maji. Kwakuwa alizaliwa familia ya kishua yeye anasema vyakula vya hovyo hovyo hawezi kula na kama unamtaka ujipange. Kwakweli alikuwa anakera kwa maneno yake. Mwanaume usingemtamani japo alikuwa mzuri.

Na akaongeza kusema yeye akizaa watoto asiulizwe mtoto anakula nini wala ada ya mtoto sijui nini.

Kama mwanaume nikajitosa na ukabwela wangu enzi hizo naishi chumba kimoja chenye joto kali. Na nilikuwa napika. Akanikubalia kuwa mpenzi wangu.

Cha ajabu alikuwa akija geto kwangu anapika maharage. Mchicha na vyakula vingine tunakula. Ananifuria nguo mashuka boxer na usafi ndani. Nilikuwa namla mavituzi mpaka baasi.

Nilikuwa sina pesa ya kumtoa out kali kali nampeleka viwanja vya Bunguruni( low class- cheap)

Nilijiuliza yale mashauzi na maneno nayoobgea kwenye mitandao na kwa marafiki zake huwa anamanisha nini?? Au ni kutaka kuwapoteza wengine??

Nikaamini kweli Woman do not mean what they say. Usiwasikilize kama una jamho lako la lufanya.

Na wewe unaweza kuwa kama yeye. Mchawi wa mwanamle ni mwanamke mwenyewe. Mnadanganyana hapa mitandaoni wakati mnaishi tofauti
 
Hero100 umenifurahisha na kunichekesha. Umeongea pointi.

Hata sisi makachelo na mabachela tukianza maisha ya meghetoni swala la.kupika haliepukiki lakini eti siku hizi unakuta mschana kabisa kupika hajui lakini anataka ndoa.

Vichekesho sana.
Mkuu nimeshuhudia hawa viumbe wanaagiza mpaka wali kwa kupiga simu tu yaani hawapiki kabisa mbaya zaidi uende na zawadi za nyama sijui nyanya anawagawia majirani zote...sema ukiona hivyo ujue nikupiga tu nakuondoka na ukirudi lazima utaukwaa
 
Hata kuoga tu ni lashalasha anajimwagia maji lakini ukoko anaobaki nao huko chini si wa nchi hii. Yeye anashinda na smartphone tu anachati asubuhi hadi jioni.
 
Ama liwe somo ktk mitaala mashuleni
Somo:Mahusiano
Litumike kutoa elimu juu ya wanawake na wanaume,watoto,saikolojia ya mahusiano,dini,mila,sheria ya ndoa nk nk
Ili kujenga social skilss za kumudu mahusiano kama taifa,walau watu wapate knowledge basic
 
Wa hi
Mkuu nimeshuhudia hawa viumbe wanaagiza mpaka wali kwa kupiga simu tu yaani hawapiki kabisa mbaya zaidi uende na zawadi za nyama sijui nyanya anawagawia majirani zote...sema ukiona hivyo ujue nikupiga tu nakuondoka na ukirudi lazima utaukwaa
Huyo sasa yeye ni dharau yaani unaenda na nyama anagawia watu? Sometime ni vile hajui kupika ndio maana anaogopa.
 
mshauri?? yaani unasikiliza ushauri wa mwanamke?

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu,

Lengo la ushauri ni kukuongezea machaguo (options) na kukufafanulia mambo ili uweze kufanya maamuzi sahihi.

Unaweza kuufuata wote, kufuata sehemu yake au kutokuufuata kabisa. Huo ndio ushauri.

Kama amekupa ushauri mzuri, kwanini usiufuate?
 
Mkuu,

Lengo la ushauri ni kukuongezea machaguo (options) na kukufafanulia mambo ili uweze kufanya maamuzi sahihi.

Unaweza kuufuata wote, kufuata sehemu yake au kutokuufuata kabisa. Huo ndio ushauri.

Kama amekupa ushauri mzuri, kwanini usiufuate?
mwanaume mzima unategemea ushauri wa mwanamke?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe ni Ali Kiba mkuu?

Anyway nafikiri ni kuwa msaidizi kwanza sababu unaweza ingia kwenye ndoa msikae sana mume akaumwa yupo kitandani, au mkapata shida ya kupata mtoto na mambo mengi ya duniani lakini usaidizi wa mwanamke kwa mumewe ukasimama kwa kila mahala. Kuuguza, kushauri, kusaidia, kuliwaza nakadhalika.
Mkibarikiwa zaidi basi heri na majukumu yanaongezeka... watoto, kushauri na kulinda mali zao, kubeba majukumu ya nyumbani nk.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante mkuu
Ningependa pia uongezee vifungu vya Biblia vinavyoelezea majibu yako pale juu

Sent using Jamii Forums mobile app
Majibu yangu ni mchanganyiko wa Maandiko Matakatifu na Utamaduni wetu kama Waafrika.

Kwa upande wa Maandiko Matakatifu soma:
• Mwanzo 2:18, 24
• Mathayo 19:5
• Wakolosai 3:18
• 1 Wakorintho 7:3-4; 11:3, 10-11
• Waefeso 5:22-24
• 1 Petro 3:1-6

Na mingine mingi.
 
Asante
Naomba katika kila point uliyotoa uniwekee kifungu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…