Majukumu ya mwanamke kwenye ndoa ni yapi?

Karibu Mkuu.


Nitajibu kwa kuchukulia muktadha wa ndoa. Kwa kifupi kabisa, nafasi ya mwanamke ni kumkamilisha mwanaume.

Hii ni kwa kumsaidia:
• Ushauri sahihi katika mambo mbalimbali hasa yanayohusu familia
• Malezi ya familia na watoto
• Kumpa faraja, kumuunga mkono na kumtia moyo katika mambo na hali zote
• Kukaribisha na kuwakarimu wageni wote
• Kumrekebisha, kwa kutumia busara na upendo wa hali ya juu, pale anapokosea
• Kuwa chanzo cha furaha na amani, n.k.

Bottom line: wajibu wa kwanza wa mwanamke (primary responsibility) ni kumtii mumewe katika mambo mema yote yampendezayo Mungu.


Nafasi ya Roho Mtakatifu kwa wanadamu wote, akiwemo mwanaume, ni kutufariji na kutuongoza kupitia mapaji yake saba: elimu, hekima, akili, nguvu, ibada, shauri na uchaji wa Mungu.

Roho Mtakatifu anatusaidia na kutuonesha njia zitupasazo kuzifuata na kuziishi ili kumpendeza Mungu na kuendelea kuwa watoto waaminifu wa Mungu.

Roho Mtakatifu anatufundisha na kutushauri tuweze kutawala mazingira yetu na kufanikiwa bila kuharibu utaratibu aliotuwekea Mwenyezi Mungu wa kuendelea kuifanya dunia mahali pema na salama pa kuishi; sisi na viumbe wengine.


Utofauti wao ni:

• Wakati mwanaume anamsaidia mwanamke na mwanamke anamsaidia mwanaume; Roho Mtakatifu anawasaidia wote, mwanaume na mwanamke.

• Mwanamke anamsaidia mwanaume kimwili (physically) zaidi wakati Roho Mtakatifu anatusaidia sote kiroho.

• Mwanamke anamsaidia mwanaume kwa msaada wa Roho Mtakatifu wakati Roho Mtakatifu mwenyewe (bila msaada wa yeyote) anamsaidia mwanaume na mwanamke.

Tofauti kubwa kuliko zote: mwanamke ni mwanadamu na anaweza kuwa na mapungufu yake hasa katika kutimiza nafasi yake kama mke; wakati Roho Mtakatifu ni Mungu na amekamilika, hana mapungufu.

Wasalaam.
Ahsante Sana
 
Ni kupika,kupeana raha ,kuzaa,kufua nunua mashine ya kufulia huna hela tafuta mtu wa kufua.
Niliwahi kuwa na Star mmoja wa Bongo enzi za nyuma akiwa na washkaji na marafiki zake aisee huwezi hata kumtamani. Anayoongea kwa nyodo na dharau alikuwa anatisha hadi wanaume walimuogopa. Akiwa mitandaoni ndio kabisa. Yeye anasema kwanza hawezi kuwa na mwanaume asiye na pesa. Pili anasema swala la kuolewa kwake sio option na hata akiolewa hataki upumbavu wa kuambiwa kupikia familia wala kufua au kuchota maji. Kwakuwa alizaliwa familia ya kishua yeye anasema vyakula vya hovyo hovyo hawezi kula na kama unamtaka ujipange. Kwakweli alikuwa anakera kwa maneno yake. Mwanaume usingemtamani japo alikuwa mzuri.

Na akaongeza kusema yeye akizaa watoto asiulizwe mtoto anakula nini wala ada ya mtoto sijui nini.

Kama mwanaume nikajitosa na ukabwela wangu enzi hizo naishi chumba kimoja chenye joto kali. Na nilikuwa napika. Akanikubalia kuwa mpenzi wangu.

Cha ajabu alikuwa akija geto kwangu anapika maharage. Mchicha na vyakula vingine tunakula. Ananifuria nguo mashuka boxer na usafi ndani. Nilikuwa namla mavituzi mpaka baasi.

Nilikuwa sina pesa ya kumtoa out kali kali nampeleka viwanja vya Bunguruni( low class- cheap)

Nilijiuliza yale mashauzi na maneno nayoobgea kwenye mitandao na kwa marafiki zake huwa anamanisha nini?? Au ni kutaka kuwapoteza wengine??

Nikaamini kweli Woman do not mean what they say. Usiwasikilize kama una jamho lako la lufanya.

Na wewe unaweza kuwa kama yeye. Mchawi wa mwanamle ni mwanamke mwenyewe. Mnadanganyana hapa mitandaoni wakati mnaishi tofauti
 
Hero100 umenifurahisha na kunichekesha. Umeongea pointi.

Hata sisi makachelo na mabachela tukianza maisha ya meghetoni swala la.kupika haliepukiki lakini eti siku hizi unakuta mschana kabisa kupika hajui lakini anataka ndoa.

Vichekesho sana.
Mkuu nimeshuhudia hawa viumbe wanaagiza mpaka wali kwa kupiga simu tu yaani hawapiki kabisa mbaya zaidi uende na zawadi za nyama sijui nyanya anawagawia majirani zote...sema ukiona hivyo ujue nikupiga tu nakuondoka na ukirudi lazima utaukwaa
 
Napendekeza ustawi wa jamii wajikite kutoa elimu na majukumu ya ndoa kuliko kufuatilia wanaume wanaoterekeza wanawake na watoto wakati chanzo ya kuterekeza wanawake na watoto ni kutokuwa na elimu ya ndoa.

Ukifuatilia ustawi wa jamii wakihojiwa na kutoa elimu wamejikita sana kwenye matokeo (out put) kuliko kujikita kwenye vyanzo vya matatizo kama haya.

Ni mwanaume gani asiyependa kula chakula cha mkewe ,asiyependa kufuliwa, anayependa nyumba liwe chafu. Elimu ya mashuleni tu haifundishi mtoto kuwa na elimu ya ndoa.
Ndio maana vijana wanawachezea lkn wanawaacha wanaoa wengine,mke/mpezi wako akijua majukumu yake kindoa ni rahisi kumsaidia kazi,ata akipika vibaya unajua tu ni bahati mbaya,

Hawa ma slay queen mm nawaona wachafu ,mwanamke umepaka make up hadi kujua bara analotoka mpaka umulize tena,kucha sasa hadi kero.kikubwa ustawi wa jamii wajikite kutoa elimu ya ndoa sio haki sawa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hata kuoga tu ni lashalasha anajimwagia maji lakini ukoko anaobaki nao huko chini si wa nchi hii. Yeye anashinda na smartphone tu anachati asubuhi hadi jioni.
 
Naona elimu ya ndoa itolewe na taasisi za dini, kila mtu na imani yake kwa vijana hasa, mfano kwa katoliki muda wa mafundisho ya ndoa ni miezi 3 hadi sita, mimi naona huo muda hautoshi. Wasisubiri hadi mtu atangaze ndoa ndio afundishwe, iwe kama miaka 5 hivi kwa yeyote anayehitaji, mtu ajiandae kwa miaka 5.
Ama liwe somo ktk mitaala mashuleni
Somo:Mahusiano
Litumike kutoa elimu juu ya wanawake na wanaume,watoto,saikolojia ya mahusiano,dini,mila,sheria ya ndoa nk nk
Ili kujenga social skilss za kumudu mahusiano kama taifa,walau watu wapate knowledge basic
 
Wa hi
Mkuu nimeshuhudia hawa viumbe wanaagiza mpaka wali kwa kupiga simu tu yaani hawapiki kabisa mbaya zaidi uende na zawadi za nyama sijui nyanya anawagawia majirani zote...sema ukiona hivyo ujue nikupiga tu nakuondoka na ukirudi lazima utaukwaa
Huyo sasa yeye ni dharau yaani unaenda na nyama anagawia watu? Sometime ni vile hajui kupika ndio maana anaogopa.
 
mshauri?? yaani unasikiliza ushauri wa mwanamke?

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu,

Lengo la ushauri ni kukuongezea machaguo (options) na kukufafanulia mambo ili uweze kufanya maamuzi sahihi.

Unaweza kuufuata wote, kufuata sehemu yake au kutokuufuata kabisa. Huo ndio ushauri.

Kama amekupa ushauri mzuri, kwanini usiufuate?
 
Mkuu,

Lengo la ushauri ni kukuongezea machaguo (options) na kukufafanulia mambo ili uweze kufanya maamuzi sahihi.

Unaweza kuufuata wote, kufuata sehemu yake au kutokuufuata kabisa. Huo ndio ushauri.

Kama amekupa ushauri mzuri, kwanini usiufuate?
mwanaume mzima unategemea ushauri wa mwanamke?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe ni Ali Kiba mkuu?

Anyway nafikiri ni kuwa msaidizi kwanza sababu unaweza ingia kwenye ndoa msikae sana mume akaumwa yupo kitandani, au mkapata shida ya kupata mtoto na mambo mengi ya duniani lakini usaidizi wa mwanamke kwa mumewe ukasimama kwa kila mahala. Kuuguza, kushauri, kusaidia, kuliwaza nakadhalika.
Mkibarikiwa zaidi basi heri na majukumu yanaongezeka... watoto, kushauri na kulinda mali zao, kubeba majukumu ya nyumbani nk.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante mkuu
Ningependa pia uongezee vifungu vya Biblia vinavyoelezea majibu yako pale juu

Sent using Jamii Forums mobile app
Majibu yangu ni mchanganyiko wa Maandiko Matakatifu na Utamaduni wetu kama Waafrika.

Kwa upande wa Maandiko Matakatifu soma:
• Mwanzo 2:18, 24
• Mathayo 19:5
• Wakolosai 3:18
• 1 Wakorintho 7:3-4; 11:3, 10-11
• Waefeso 5:22-24
• 1 Petro 3:1-6

Na mingine mingi.
 
Majibu yangu ni mchanganyiko wa Maandiko Matakatifu na Utamaduni wetu kama Waafrika.

Kwa upande wa Maandiko Matakatifu soma:
• Mwanzo 2:18, 24
• Mathayo 19:5
• Wakolosai 3:18
• 1 Wakorintho 7:3-4; 11:3, 10-11
• Waefeso 5:22-24
• 1 Petro 3:1-6

Na mingine mingi.
Asante
Naomba katika kila point uliyotoa uniwekee kifungu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom