Majukumu ya Afisa Mtendaji wa Mtaa (MEO)

Status
Not open for further replies.

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Aug 7, 2018
625
938
IMG_20210329_123753_989.jpg

Ni mtendaji wa shughuli zote za Mtaa, Mtunzaji wa kumbukumbu zote za vikao pamoja na mali za Mtaa, rejesta ya wakazi wa Mtaa na barua zote. Mwajiriwa wa Halmashauri ya Mji, huwajibika kwa Halmshauri ya Mji na huwajibika pia Serikali ya Mtaa.

Mshauri Mkuu wa wananchi na mhamasishaji wa utekelezaji wa shughuli zote za maendeleo ya Mtaa. Mwasilishaji taarifa zote muhimu za Mtaa kwa Afisa Mtendaji wa Kata (WEO). Mlinzi wa amani (anaweza kumkamata mtu yeyote anayeonekana kuhatarisha amani katika mtaa wake).

Msimamizi wa utekelezaji wa sheria ndogo katika mtaa wake. Kupanga na kuhakikisha kupitishwa ratiba za vikao vya mkutano wa Kamati ya Mtaa. Kwa kushirikiana na Mwenyekiti kuandaa ajenda za vikao mbalimbali.

Kuandaa taarifa mbalimbali za kamati ya mtaa kwa ajili ya mkutano wa wakazi wa mtaa pamoja na makisio na hesabu za mapato na matumizi. Kuwashauri wenyeviti wahusika juu ya taratibu za kuendesha vikao, kufanya maamuzi na kuandika mihtasari ya vikao na kuhifadhi katika daftari.

Kufanya mawasiliano na ngazi zingine za utawala kwa niaba ya Mtaa. Msimamizi wa mapato na kodi za Mtaa. Msambazaji wa habari na taarifa mbalimbali kwenye mtaa. Kuwa daraja kati ya Mtaa na Asasi zingine kwenye mtaa au nje ya Mtaa kama Zahanati, Shule, Mashirika yasiyo ya Kiserikali n.k.

Mfuatiliaji wa miradi ya Mtaa na kutoa taarira kwenye kamati ya mtaa. Mfuatiliaji wa utekelezaji wa maamuzi ya vikao mbalimbali vya Mtaa. Muandaaji wa semina na warsha za wakazi kwenye mtaa na viongozi wa Mtaa.

Kamati ya Mtaa kupitia Mkutano wa Wakazi wa Mtaa inaweza kupendekeza kwa Halmashauri ya Mji ili Afisa Mtendaji wa Mtaa (MEO) aondolewe au achukuliwe hatua na kuwajibishwa. Hufanya lolote linalofaa koboresha utawala na utendaji wa serikali ya Mtaa.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom