nngu007
JF-Expert Member
- Aug 2, 2010
- 15,862
- 5,797
KITAIFA
By Raymond Kaminyoge
Posted Monday, October 29 2012 at 12:18
IN SUMMARY
"Nawaasa viongozi wa serikali mkiwa madarakani huku mkitembelea magari yenye bendera za taifa, mtazungukwa na marafiki lakini baadhi yao ni wanafiki."
WAZIRI wa zamani, Edgar Maokola Majogo amejitokeza amesema baada ya kustaafu nusu ya marafiki walimkimbia kutokana na kutambua kuwa tena msaada kwao.
Majogo ambaye amekuwa waziri katika wizara mbalimbali, alisema akiwa madarakani alikuwa na marafiki wengi waliokuwa karibu naye.
Akizungumza kwenye kufunga maonyesho ya wajasiriamali Dar es Salaam juzi, Majogo alisema marafiki wanakuwa karibu pindi kiongozi anapokuwa madarakani, wakijua watapata msaada.
"Walipogundua sina cheo tena serikalini walinikimbia mmojammoja," alisema Majogo na kuongeza:

Alisema wengi wataonyesha unyenyekevu lakini baada ya kustaafu watashangaa hawaonekani.
Alisema jambo la msingi kwa viongozi na wananchi wanatakiwa wanapokaribia kustaafu wajiandae kuwa wajasiriamali.
"Watu wafahamu kwamba kuna muda wa kustaafu na wajiandae kwa hilo, kwa kuanza kuwa wajasiriamali," alisema Majogo.
Akitoa mfano wake, alisema baada ya kustaafu aliomba mkopo benki na kuanza ujasiriamali na hivi sasa ana kiwanda cha kubangua korosho.
"Niliweka dhamana nyumba yangu nisiporudisha mkopo kwa wakati, nyumba inaweza kuuzwa ili kulipia mkopo huo," alisema.
Majogo alisema kiwanda hicho kilichopo Dar es Salaam kimetoa ajira kwa zaidi watu 100, wengi wao wakiwa wanawake.
"Kwahiyo ukijiandaa mapema baada ya kustaafu utaishi maisha ya raha na starehe," alisema Majogo
Alishauri serikali kuandaa utaratibu wa kuvisaidia vikundi vya wajasiriamali ambavyo vimeonyesha uwezo wa kujiendeleza kupambana na umaskini.