Majirani wazuia jeneza la kijana kuingia kwa wazazi wake

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,377
8,121
Page-3-BEDA-780x470.jpg
Wananchi wa Mtaa wa Maganga, maeneo ya Nurulyakini, Temeke, Dar es Salaam wamezuia mwili wa marehemu Pius Beda maarufu Stahimili (32) kuingia nyumbani kwa wazazi wake, kuonesha hasira zao kwamba wazazi hao walishindwa kumhudumia alipokuwa hai.

Kijana huyo alikutwa amekufa kwa kujinyonga nyumbani kwa jirani alikokuwa anasaidiwa mahala pa kulala.

Wakizungumzia mkasa huo Dar es Salaam jana, majirani wa Stahimili walisema amekuwa akiishi maisha magumu kiasi kwamba hata alipotafuta msaada kwa baba na mama yake wa kambo aliokuwa anaishi nao hakusaidiwa.

Walisema sababu ya kuzuia jeneza lililokuwa limebeba mwili huo ni kwa kuwa wazazi wake walishindwa kumsaidia pale alipohitaji msaada kiasi cha majirani kuingia jukumu la kumsaidia mahali pa kuishi ingawa bado chakula pia hakuwa anakipata.

“Tulizuia maiti isiingie ndani kwa wazazi wake kwa sababu tulikuwa tunajua maisha anayoishi. Msaada wake mkubwa ulitoka kwa majirani wakati wazazi wake wana uwezo, sasa tukasema kama hawakumsaidia mwanzo watuachie wenyewe,” alisema mmoja wa majirani zake ambaye hakupenda kutaja jina lake.

Jirani mwingine ambaye wazazi wake walimpa hifadhi kijana huyo alisema Stahimili ambaye alikuwa pia na matatizo ya kiafya, alikuwa na mgogoro na familia yake na alipokuwa akijaribu kutafuta suluhisho hakusikilizwa.

Kwa mujibu wa jirani huyo, kijana alikwenda nyumbani kwao kuomba msamaha ili kuweka mambo sawa ila mambo yalishindikana.

Alisema alikuwa akifanya kazi viwandani baadaye kazi iliisha kwa sababu ya matatizo yake ya kiafya (kupoteza fahamu mithili ya kifafa), baadaye alikosa fedha za kula na kulipa kodi akaamua kurudi nyumbani kwao kuomba msaada ila alielezwa hana nafasi kwao labda aende kwa baba yake mdogo.

Baada ya vurugu za wananchi wa eneo hilo la Temeke Maganga kuzuia maiti, iliwekwa nje ya jumba moja bovu alikolazimika kuishi, jirani na nyumbani kwao na kuagwa.

Lakini wazee wa busara na viongozi wa dini walituliza hali, kukawa tulivu. Wakati wa kupeleka mwili kwa ajili ya kuupumzisha kwenye nyumba yake ya milele katika Makaburi ya Wailes, Chang’ombe wananchi walizuia pia asibebwe na gari lililokuwa limekodiwa na wao wakaamua kuubeba wenyewe.

Baba wa kijana huyo, Beda Malya alikataa kuzungumzia sakata hilo huku mama yake mzazi, Segolina Alphonce aliyekuwa akiishi Moshi, Kilimanjaro na ambaye alikuja kwa ajili ya msiba wa mtoto wake akisema mwanaye alikuwa akiishi na baba yake tangu akiwa na umri wa miaka saba na hakujua lolote linaloendelea ila anamwachia Mungu.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Temeke kwa Maganga, Jaffar Shoo alisema sio vizuri kutoa hukumu kwa wazazi wa kijana huyo na kwamba watafanya uchunguzi wa kile kinachoelezwa kama ni kweli ila anachoamini kijana huyo ni mtu mzima na hakuna aliyemlazimisha kujiua isipokuwa siku yake imefika.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro alisema atafuatilia sakata hilo kujua kinachoendelea.

HABARI LEO
 
Wazazi tuzae watoto tunaoweza kutunza ,hivi unamkataaje mwanao wababa wwchache sana hujali watoto
32 Years ?

Alexander the Great had a profound effect on world history. His conquests covered the entire known world at the time, and he was responsible for the spread of Greek culture throughout the ancient world. In Babylon in 323 BC, Alexander died when he was nearly 33 years old.

RIP kijana..., anyway si vema kuleta lawama kwa mtu yoyote yule..., In life we make our own beds hence we should be ready to lie on them....
 
32 Years ?

Alexander the Great had a profound effect on world history. His conquests covered the entire known world at the time, and he was responsible for the spread ...

Hujui kama afya ya akili ni factor katika mafanikio.

Hao kina Alexander hawakuishi maisha ya kulala njaa ama stress stress toka utotoni.. wamezaliwa familia zenye mali kwa enzi hizo
 
Hujui kama afya ya akili ni factor katika mafanikio.

Hao kina Alexander hawakuishi maisha ya kulala njaa ama stress stress toka utotoni.. wamezaliwa familia zenye mali kwa enzi hizo
Nope kuna wengi waliofanikiwa kutokana na hardships (ni kama paka ukimweka kwenye kona anaweza ku-react kama tiger).., Watu masikini wenye something to prove inaweza kuwafanya to work harder wakati wengine wamelala..., ndio maana immigrants mara nyingi wanafanikiwa kuliko wazawa.., a sense of prosecution gives them motivation to prove something...

When life gives you lemons, make lemonade..., Sisemi tusiwasaidie watu, au tuwa-exploit watu hapana lakini in the end tusiwe wepesi wa ku-point fingers kwa wengine...
 
Mfano mtu kama 50 Cent wote tunamjua sasa hivi lakini kwa mazingira aliyokulia ukifika miaka 25 na upo hai hujapigwa shaba unamshukuru Mungu...mbona wametoboa....32+ years ni nyingi sana kwa kijana kutoa kisingizio au lawama kama hajasaidiwa na wazazi
 
Am all kwa kutoa msaada lakini ni msaada sio obligation..., mfano mzazi ana wajibu wa kusomesha, kulisha na kutoa basic needs mpaka mtoto anapokuwa mtu mzima..., zaidi ya hapo sio wajibu tena bali ni ubinadamu...

Ndio haya mambo watoto wanakuombea ufe ili warithi yaani mali sio yako tena ni yao / yenu...

Mwisho wa siku ni appreciation which matters; hujaona mtu anasomesha mtoto wa mtaani alafu huyo mtoto anamkumbuka na kumjali maisha yake yote (appreciation) lakini mtoto wake binafsi mtu kauza mpaka shamba ili mtoto asome ila baadae mtoto analaumu hakupelekwa english medium kama mtoto wa jirani ?
 
Back
Top Bottom