Majini & Mapepo 👻🤔

Majini & Mapepo 👻🤔

Hii sometimes huwa ni akili yako ndio inakuendesha tu hasa kwenye hizi nyumba za ibada lakini uwepo wa mapepo wabaya upo sana, nakumbuka mwaka fulani nilienda kanisa fulani la Wanaijeria nilitajwq jina na yule Pastor bila hata kumwambia, tarehe,mwaka na mwezi wa kuzaliwa 😀 yaanj mpaka wilaya niliyozaliwa , hapo nilijiuliza sana japo haikuniletea suluhisho ya lile nililokuwa nalitaka.

Wakati mwingine Ubongo wetu hupenda sana mambo marahisi tofauti na uhalisia wa kile tunachokitaka, how come upate kazi nzuri bila kuangalia kwamba hiyo kazi ina ushindani ? Kwanini upate pesa kwa njia ya maombi tu bila kujua siri ya hiyo pesa ?

Ninachokumbuka lile kanisa niliombewa nikaruka mapepo kama yote 🤣🤣🤣 nikachana mpaka suruali yangu cadet kaliii na kiatu kikaachia sole 😂

Mapepo wapo lakini akili za waamini wengi zimeshapumbazwa na ujinga wa hawa wakujiita Manabii maana inashangaza kila mara mapepo yanakemewa die by fire 🔥 Holy spirit na blah blah kibao .

Hayo mambo ya mapepo na majini yapo kabisa na watu tushapigwa sana zongo. Nakumbuka sehemu fulani kuna dogo ni mtaalamu sana wa dua alibis viatu vyake msibani akaenda kununua misumari na dawa kwenye maduka ya dawa za asili akachanganya akasomea akatengeneza kitu ambacho hakionekani akakituma kikamtamfute aliyeiba vile viatu mbona mwizi alirudisha ?
Oyaaaa we unaamini hizi mambo nimekunyooshea mikono juu
 
Wewe unaona duniani kuna usawa?
Au nikupe binocular?
Usawa kwa muktadha upi yaani ?

Mimi nazungumzia usawa wa mambo kwa ujumla sio usawa ambao unakuwa kama upendeleo binafsi, kama unawazia usawa wa haki hapo utakuwa unakosea, kama kungekuwa na usawa wa haki Polisi, Mahakama, Magereza zisingekuwepo
 
Usawa kwa muktadha upi yaani ?

Mimi nazungumzia usawa wa mambo kwa ujumla sio usawa ambao unakuwa kama upendeleo binafsi, kama unawazia usawa wa haki hapo utakuwa unakosea, kama kungekuwa na usawa wa haki Polisi, Mahakama, Magereza zisingekuwepo
Usawa katika uumbaji
 
Mkuu, Mimi nitawaamini hao mapepo wachafu kama wapo siku wakinikata mtama kanisani.

Aidha, nitawaamini majini siku wakinilamba vibao bila huruma, sijui muda huo nikiwa sehemu gani, labda nikiwa napita maeneo ya makaburini.
Umeongea ukweli kabisa, watu tuliopita sehemu mbalimbali za watu huwa tunaona sio wabaya hata wazuri
 
Hapa naweza kukuelewa ni kweli kuna uwezekano dunia ina chanzo

Ila kwa hadithi za Qur’an na bible mapungufu ni mengi tena ya wazi
Niliwahi kuwa na rafiki wa kihindi na nilikuwa najaribu kuelewa imani yake kuhusu kuabudu ng'ombe ........ alisema wao hawaabudi ng'ombe tuu bali wananuiya vitu vikitimia wanaweka maagano... kuhusu Mungu alisema hawamwabudu ila wanaamini katika Nguvu ya asili inayotawala viumbe vyote kupitia iyo nguvu ndio wanaitumia katika vitu. Kwangu kumwelewa Huyu Muumbaji/Mungu hautakiwi uwe na fixed mind maana asili yake ni roho kamili utakayoiona kwenye maji,moto,hewa,udongo,viumbe,mimea,mwanga,giza ,nyota hivyo sidhani kuwa na maana moja itatosha kumweleza .Ukishamweka Mungu/muumbaji kwenye kipimo cha size au umbo umekosea.
 
Uumbaji upi sasa ? Viumbe hai au vitu vyote?
Mi naona unatoka njee ya mada umesema dunia inaishi kwa kanuni ili upatikane usawa nikakuuliza hii dunia inausawa ?

Haina kuanzia uumbaji na mengine mengi kuna wanaozaliwa wafupi wengine warefu wengine weusi wengine weupe walemavu wengine wazima hakuna cha usawa wala nini
 
Hapana hivi kuna faida?
Mbona kama unanibana mbavu ? Bila sababu au ulikuwa unanitafuta ? 😀😀😀 ulichojibu hapo hata sijakielewa faida ipi ? Kivipi ? Kwa lengo lipi ? Sijihusishi na hayo mambo lakini huwa ninasikia kwa watu na huwa najaribu kuwa mdadisi kujua uhalisia wa mambo ulivyo.

This is Afrika mdogo wangu, tuna ulimwengu wa pekee yetu 😂
 
Mbona kama unanibana mbavu ? Bila sababu au ulikuwa unanitafuta ? 😀😀😀 ulichojibu hapo hata sijakielewa faida ipi ? Kivipi ? Kwa lengo lipi ? Sijihusishi na hayo mambo lakini huwa ninasikia kwa watu na huwa najaribu kuwa mdadisi kujua uhalisia wa mambo ulivyo.

This is Afrika mdogo wangu, tuna ulimwengu wa pekee yetu 😂
Sikubani mbavu nataka fact tupu undugu hukoo hapa ni fact zitembee wewe umesema unaamini majini na mapepo yapo nimekuuliza

Je kuna faida gani kuamini kitu huna uhakika nacho?
 
Back
Top Bottom