Majina yetu jamani

Majina yetu jamani

Jina ni jina tu liwe la kizungu au kibantu, ilimradi liwe na maana nzuri.

Wazungu wangapi wana jipa majina ya Kiafrika as opposed to Waafrika wanaojipa majina ya kizungu? Kwa nini wenzetu wame shikilia majina yao?
 
Hodi!! naingia ilikuungana nanyie kweli tunaenda wapi? . majina tunayo mazuri na yanamaana nzuri .kwani jina hujiiti ?unaitwa na wazazi,wako. na ukikua unlibadilisha kwamatakwa yako je.?yule aliekuita anajisikiaje?. inamaana wewe unaona alikosea?. kwa kukuita jina hilo? pia majina mengine nikumbukumbu ya wazazi wetu. leo unalifuta je?.unawapenda wazazi wako? hilo tulitazame .vinginevyo tutapoteza utamaduni wetu bila kujua.wewe unaona jambo dogo kumbe kidogo huzaliwa na kikubwa.
 
Vingapi mlivyoiga toka uzunguni? Halafu leo majina yawe tija.

Pretty,

Tafadhali usiongelee ujumla! Mimi Mzalendohalisi! Wewe Pretty! Wanangu wote wana majina ya Kiafrika..na ninajivunia sana majina niliyowapa wanangu!

Haujajibu swali: Kwa nini tuige hata majina? God is Not Eurocentric..hivi Zawadi, Amani, Furaha, Shida, Ombaeli..je majina haya yana matatizo gani?

Kwa nini sisi Waafrika hatuwezi hata kuthamini vitu vyetu??

Mindset??
 
Good point.....

Halafu kwa nini mtu aitwe Grace na sio Neema? Au Rose na sio Waridi?
 
Vingapi mlivyoiga toka uzunguni? Halafu leo majina yawe tija.

Mtu una azima kama umekosa kitu sasa sisi tume kosa majina? Kuiga haikatazwi kwenye vitu vya lazima lakini mpaka majina unaona there is a need kuazima toka wa wenzetu?
 
sisi wa huku musoma tuna utaratibu wa majina, kanuni simple tu, majina 3 kwa wanaume, ambayo ni chacha, mwita na marwa, na majina 3 ya kike ambayo ni rhobi, bhoke na ghati. hivyo ukizaa mtoto unakuwa na unampa majina kulingana na hayo matatu makuu kwa jinsia zote, kama una watoto zaidi ya 3, kuna mengine pia ya ziada ambayo pia hutolewa kulingana na generation ya babu zako. kwa mfano mie mtoto wangu wa kwanza akiwa wa kiume nitampa jina la baba yangu ambalo ni mwita, kama akiwa wa kike, nampa jina la mama yangu ambalo ni rhobi. ila pia tunakuwa na kanuni ya kuwa mke achague jina la mtoto wa kike kutoka kwenye ukoo wake.
 
You! hahahahaha

Me what? Mi naitwa Nyani Ngabu...sasa huo uzungu unatoka wapi?

Mimi nadhani ni wewe. Badala ya kujiita Mrembo, Mzuri, au kisura umekimbilia kujiita Pretty? Sista duuu wewe....
 
Pretty,

Tafadhali usiongelee ujumla! Mimi Mzalendohalisi! Wewe Pretty! Wanangu wote wana majina ya Kiafrika..na ninajivunia sana majina niliyowapa wanangu!

Haujajibu swali: Kwa nini tuige hata majina? God is Not Eurocentric..hivi Zawadi, Amani, Furaha, Shida, Ombaeli..je majina haya yana matatizo gani?

Kwa nini sisi Waafrika hatuwezi hata kuthamini vitu vyetu??

Mindset??
watu wanaamua kuita haya majina ya kizungu kwa kuwa yanasound good, majina mengine ya kibantu kwa kweli kazi kweli kuita, inabidi uite hadi ushibe.
Mie sipingi haya majina ya kibantu, ila kwa kuwa ni science na technology hivyo watu tunaiga kila kitu kutoka kwa wazungu., hata kuvaa tu siku hizi ni uzungu tupu, tumeacha mavazi yetu halisia ya kibantu.
 
Me what? Mi naitwa Nyani Ngabu...sasa huo uzungu unatoka wapi?

Mimi nadhani ni wewe. Badala ya kujiita Mrembo, Mzuri, au kisura umekimbilia kujiita Pretty? Sista duuu wewe....
Pretty ndio jina langu la kibantu ndugu yangu.
 
Mkitoka kwenye majina mtakwenda kwenye mavazi na vyakula na kuendelea hehehe!!
 
watu wanaamua kuita haya majina ya kizungu kwa kuwa yanasound good, majina mengine ya kibantu kwa kweli kazi kweli kuita, inabidi uite hadi ushibe.
Mie sipingi haya majina ya kibantu, ila kwa kuwa ni science na technology hivyo watu tunaiga kila kitu kutoka kwa wazungu., hata kuvaa tu siku hizi ni uzungu tupu, tumeacha mavazi yetu halisia ya kibantu.

Pretty,

1. Pretty inasound good kwa nani?? Kwani Waridi/Mrembo haisound good??

2. Kuvaa inakuta mtu Dar na joto na mitai ya ajabu na jasho tele!! Why??

Mindset tu mbaya!

We have to learn also to appreciate good things of our own!!
 
Ukikataa majina ya "kizungu" (ambayo mengi yana asili ya kiyahudi kwa kweli, wala si "kizungu") na kukumbatia dini za kigeni, ambazo ndizo hasa mzizi wa haya majina, utakuwa unaacha ugonjwa na kujaribu kutibu dalili.

Kama unataka mabadiliko ya msingi katika fikra anzia kwenye dini, majina yatajibadilisha yenyewe.

Mobutu aliwabadilisha Wazaire (then) wote majina kwa nguvu, kwa kuanzia na yeye mwenyewe, kutoka Joseph Mobutu kwenda Mobutu Sese Seko Nkuku Ngbendu wa Za Banga, lakini ikaja gundulika zilikuwa ilikuwa ni circus trick ku distract attention kutoka issues za kiuchumi.

Juhudi za kuturudishia identity yetu kama watu kitamaduni ni lazima ziende sawa na juhudi za kuinua watu kiuchumi, ama sivyo itakuwa sawa na mambo ya Mobutu.

Mkuu Bluray, niko nyuma yako. Kikwazo kikubwa cha walio wengi kutokutumia majina ya kibantu ni dini zetu. Kwa mfano kanisa katoliki mpaka leo hii hawawezi kukubali kumbatiza mtoto jina ambalo haliko kwenye list ya watu wanaoitwa watakatifu. Huwezi kwenda kumbatiza mtoto jina kama Masatu. Wanataka Peter, Michael, John n.k. Kwangu mimi kuendelea kuyakubali haya majina ya kizungu ni kuendelea kukubali kutawaliwa kimawazo.

Najua hata wenzetu waislamu kama haujaitwa Seleman, Juma, Khalid, Haruna basi wewe haujawa mwislamu. Lakini ukweli unabaki pale pale kwamba religion has nothing to do with our names.

Baadhi ya dini zinzoitwa za kiprotestant (protestant to Roman Catholic), hazina matatizo na majina unaweza kumbatiza mtoto wako jina lolote la kikabila kwa mfano Lutheran church. Hawa wako liberal na hawataki kuhusianisha jina la mtu na dini hata kidogo.

Ili tufanikiwe katika hili, tuanze kujaribu kuwabadiri misimamo mapadre na mashekhe ili majina yetu ya kibantu yakubalike.

Tiba
 
Kanisa katoliki lina kitu kinaitwa UTAMADUNISHO. Sasa nadhani hii hawaifanyi fair kwani wanabagua baadhi ya maeneo kama hayo majina, ila wakati wa ibada katika baadhi ya sikukuu za kanisa watoto huvaa hadi vinyago. Hilo nalo walione na kulifanyia kazi
 
Majina ya kizalendo ni bab kubwa. Tutunze mila na desturi za kiafrika jamani, ili wazungu watuheshimu.....
Nawapongezene sana wenye majina ya kizaramo, kibena, kingoni, kiyao, kihaya, kimatumbi..na makabila mengine ya kitanzania na kiafrika..

TUTUNZE MILA ZETU, TUHESHIMIKE
 
Mkuu Bluray, niko nyuma yako. Kikwazo kikubwa cha walio wengi kutokutumia majina ya kibantu ni dini zetu. Kwa mfano kanisa katoliki mpaka leo hii hawawezi kukubali kumbatiza mtoto jina ambalo haliko kwenye list ya watu wanaoitwa watakatifu. Huwezi kwenda kumbatiza mtoto jina kama Masatu. Wanataka Peter, Michael, John n.k. Kwangu mimi kuendelea kuyakubali haya majina ya kizungu ni kuendelea kukubali kutawaliwa kimawazo.

Najua hata wenzetu waislamu kama haujaitwa Seleman, Juma, Khalid, Haruna basi wewe haujawa mwislamu. Lakini ukweli unabaki pale pale kwamba religion has nothing to do with our names.

Baadhi ya dini zinzoitwa za kiprotestant (protestant to Roman Catholic), hazina matatizo na majina unaweza kumbatiza mtoto wako jina lolote la kikabila kwa mfano Lutheran church. Hawa wako liberal na hawataki kuhusianisha jina la mtu na dini hata kidogo.

Ili tufanikiwe katika hili, tuanze kujaribu kuwabadiri misimamo mapadre na mashekhe ili majina yetu ya kibantu yakubalike.

Tiba
Ninaunga mkono hapa, sio dini tu bali imani ya mtu yeyote hata kama huna dini mfano; makabila ambayo wazazi hawaelewi hata maana ya majina ndo unakuta watoto wanayakimbia kwani akikua halina maana yoyote (as a lifes vision) bibi mtu anamtajia baba mwite "gagula" maana ni jina la bibi wa bibi yake mtoto akikua anauliza maana haambiwi, huyo mtu hana historia yoyote ambayo mtoto huyo anaitambua na kujivunia(Haikuandikwa wala baba haijui)
Haimkini huyu mtu akikua akaona Jina lenye historia iwe Nyerere au Mathew na kuipenda akajiita hivyo
Mfano mwingine ni makabila yanayoita majina yanayoeleweka kama wanyakyusa, wabena, wachagga etc Atuganile, Atuwene na Elibariki itakuwa ni ujinga mtu kulikana kwani linamtabiria mema na shukrani walioiona wazazi wake kwa kumpata huyo mtoto sasa niambie mtu anaita "Siwaajabu" hee unategemea atafanya nini cha ajabu?
Changamoto: Tunajifunza taratibu, tuishi maisha ambayo wajukuu watapenda na kutamani wawe kama sisi, hapo watajiita kama sisi angalia watoto wanaoitwa Obama, Nkurumah, Nyerere, Sokoine etc hata kama haitafsiriki lakini ni vision ya mzazi kwamba huyu mtoto atakuwa nani baadae. Na mtoto pia ataliona ktk maandishi historia yake na kuichukua kama kioo chake.
 
Back
Top Bottom