Raia Fulani
JF-Expert Member
- Mar 12, 2009
- 11,866
- 4,264
Kuna mambo ambayo ukitayatazama kijuujuu utaona kuwa ni madogo sana hasa katika kipindi hiki cha utandawazi. Hayo madogo kwa wingi wake ndio yanayofanya vitu vikubwa. Napenda kuzungumzia majina watu wanayopewa kutokana na jamii wanazotoka.
Ukitazama au kusikiliza majina mengi ya raia wa kikongo, mengi ni ya asili. Sina sababu ya kuyataja kwani kila mtu anayajua. Sijajua kama bado wanawapa wanao majina ya asili. Ni kitu cha kujivunia. Hii ilikuwa ni kampeni ya kitaifa huko Congo. Hapa ninachoshangaa ni kwamba, Mobutu aliwezaje kuyakataa majina ya kizungu na akakubali kuwa kibaraka.
Ukiangalia kwa undani zaidi na kuvuka mipaka ya Congo na Afrika, utafika Marekani. Wengi wa wamarekani weusi wana majina ya kizungu. Ukisikia jina tu bila ya kumwona mhusika hutajua asili yake. Niliposoma kitabu cha Booker T Washington- Up from slavery (uk. 24), niligundua kuwa wamarekani wengi walijipa majina wenyewe ama kupewa na mabwana wao. Booker alijulikana kwa jina hilo tu ila alipoanza shule alikuta wenzake wana majina zaii ya moja, hivyo mwalimu alipomuuliza anaitwa nani alijropokea tu-Booker Washington. Na ndio yakawa majina yake. Halafu alikuja gundua kuwa mama yake alimpa jina la Taliaferro alipokuwa mdogo, akaliongeza na kujiita Booker Taliaferro Washington (Booker T Washington)
Ikanikumbusha pia Kuntakinte. Kwamba, wazungu hawakuyapenda majina ya kibantu. Ni pale Kuntakinte alipokuwa akipigwa mijeledi ili akubali jina la kizungu (silikumbuki). Mwisho wa siku alilikubali baada ya kichapo kikali! Kuna wasaa ulinifanya nifadhaike sana. Nashukuru nilikuwa peke yangu wakati natazama hiyo filamu. Pale yule mzee alipomwambia pale chini alipolala kwa maumivu, naye akitokwa machozi, No matter what they call you. You will remain Kuntakinte. Nilifadhaika.
Sasa najiuliza, hii kasumba ya majina ya kizungu ni ya nini? Mbona wao hawajiiti majina yetu ya kibantu? Watanzania wengi hubadilisha majina yao angalau yafanane na ya kizungu. Japo si katika maandishi, basi matamshi. Heko kwa wale walio na majina ya asili, au hata kama si ya asili basi yanayotamkika Kiswahili kama Joni, Samweli, Daudi, Yohana, Mariki n.k. nadhani majina ya kiitaliano huwa mnayasikia. Heko pia kwa wale wenye majina ya bandia ya kiasili. Napenda kutolea mifano humu jamvini. Nyani ngabu, Mziwanda, Mzee Mwanakijiji, Kibunango, Kichuguu, Bubu , Mzizi mkavu, Mbu, Visenti, MwanaFA, Masanilo, Kuntakinte, Kizimkazimkuu, Msanii, Dingiswayo, (sitawamaliza)
Changamoto kwa akina Invisible, Field Marshall, Wos, Next level, Pretty, Fidel, Allien, Sasha Fierce, Lazy dog, Game theory, na wengine wengi.
Ningetamani kusikia wale wamarekani weusi wanajiita majina ya asili yao (Afrika). Na idadi kubwa ya watanzania tuwe na majina ya asili yetu. Tusijidanganye na majina ya magharibi nay a watakatifu na ya Mashariki ya kati. Ukarimu huanzia nyumbani.