Majina ya utani enzi za utoto!

Majina ya utani enzi za utoto!

CharmingLady

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2012
Posts
18,304
Reaction score
12,997
Habari za usiku wanaCC....

Miss u mingi wapendwa, hope mko mwake mwake babaake!!

Dah, leo nimekumbuka majina ya utani enzi za utoto, hapa nitataja baadhi ya majina ya utani ya marafiki zangu wa utotoni na langu nitalitaja humohumo ila sitaliweka wazi maana kuna watu humu wanaweza kunistukia....

Nawe pia unaweza kuongeza jina lako au la marafiki zako wa utotoni!!!!!

Kuna dogo mmoja alikuwa akiitwa Pendo, yeye tulimtungia Pendo mshua alikuwa.mshua kweli, Dogo mmoja tulikuwa tunamuita Maudaga ( mihogo iliyokaushwa kwa ajili ya kusagwa kuwa unga) yeye huyu kichwa chake kila siku kilikuwa na vidonda donda visivyopona.

Mwingine tulimuita pengo tochi, baada ya kung'ooka meno mapengo yake yalikuwa makubwa kweli. Hata baada ya meno kuota jina lake la utani likawa pengo tochi...

Mwingine tulimuita Miss Coke.. huyu alikuwa msichana mweusi ti, yaan ule weusi wa mng'ao sana!

Mwingine tulimuita Mchomoko, yaan huyu msichana alikuwa anaongea saaana, afu alikuwa hajatulia, mara yuko. hapa mara kule ya ana kiherehereeeeeee........

Hebu ongezea!!!!!
 
Namkumbuka jamaa mmoja primary alikuwa anaitwa Nyanya, kisa macho yake......na mpaka mtaani alikuwa maarufu kwa jina hilo.
 
Namkumbuka jamaa mmoja primary alikuwa anaitwa Nyanya, kisa macho yake......na mpaka mtaani alikuwa maarufu kwa jina hilo.

Hahahahaaaa.... nyanyaaaaaa, vipi macho yake yalikuwa makubwa au mekundu???
 
Hahahaaa cousin umenikumbusha mbali ujue... Enzi hizo naitwa mdolii... Kisa eti nilikuwa napenda kupepesa macho kama ile midoli ya plastic.
 
Hahahaaa cousin umenikumbusha mbali ujue... Enzi hizo naitwa mdolii... Kisa eti nilikuwa napenda kupepesa macho kama ile midoli ya plastic.

Teh teh teh cousin... Mie nilikuwa na mdoli nilioupenda saaana kuliko kitu chochote.... Unajua nini kilitokea, Nilipopata mtoto wa kike si wakamuita jina la yule mdoli wangu... Yan nilichukia kama nini ila ndo kwanza lile jina la mdoli limekolea kuliko jina lake halisi!!!
 
Wengine tulikuwa very cool
sijui ushamba ulikuwa mwingi
sikumbuki hata kama nilikuwa na jina la utani.
 
Teh teh teh cousin... Mie nilikuwa na mdoli nilioupenda saaana kuliko kitu chochote.... Unajua nini kilitokea, Nilipopata mtoto wa kike si wakamuita jina la yule mdoli wangu... Yan nilichukia kama nini ila ndo kwanza lile jina la mdoli limekolea kuliko jina lake halisi!!!

hahahaaa, ukilichukia jina la utani wenzio ndio kwanza wanazidisha kuliita mimi mpaka leo waleniliyokuwanao wakiniona wananiita mdolii,
 
hahahaaa, ukilichukia jina la utani wenzio ndio kwanza wanazidisha kuliita mimi mpaka leo waleniliyokuwanao wakiniona wananiita mdolii,

Yaan acha kabisa... Imenibidi nami nizoee tu kumuita hivyo make limeshika sanaa?!
 
hahahahahaha mimi na raki yangu hadi leo tukikutana tuna itana majina ya utani mimi alikuwa ana niita kibodi na yeye nilikuwa na muita kitambi na haya majina yalioshika hadi leo hii.
 
Hahahaaa cousin umenikumbusha mbali ujue... Enzi hizo naitwa mdolii... Kisa eti nilikuwa napenda kupepesa macho kama ile midoli ya plastic.
nilijua tuu wewe ulikuwa unaitwa mdoli.
 
daaa kuna shemeji yangu humu alikuwa anaitwa ngumi jiwe alikuwa anapigana sana yani kuna sikun alipiga wasichana wenzie kama sitta hadi tukampa uongozi wa darasa shule ya msingi na alikuwa akipigana ana hakikisha amekung"ata kabisa.
 
Back
Top Bottom