Majina ya Mitaa na Historia ya Uhuru wa Tanganyika

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,903
30,243
MAJINA YA MITAA YAHIFADHI HISTORIA

Ndugu zanguni hivi sasa kuna mradi wa Anuani za Makazi (Post Code).
Naamini sote tunashausikia kwa kuwa serikali imeutangaza.

Mradi huu ulitakiwa uchukue miaka 5 lakini Rais Mama Samia ameamua huu mradi uwe "Operation Anuani za Makazi" na ukamilike kwa miezi 5 yaani January hadi May 2022.

Katika mradi huu kupitia serikali za mitaa wakazi wa wana fursa ya kubadili jina la mtaa kwa sababu maalum.

Mathalan Mtaa wa Tandamti ni mtaa akiishi marehemu Mzee Mshume Kiyate ambae mchango wake katika kupigania uhuru wa Tanganyika hakuna asiyeufahamu.

Hii ni fursa nzuri ya kubadili jina la Mtaa wa Tandamti kuwa Mtaa wa Mshume Kiyate.

Muhimu tuwafahamishe na wengine ili ikiwa ipo haja na wao wabadili majina ya mitaa yao kwa kuenzi historia ya Dar es Salaam na wazee wetu waliofanya makubwa katika mji huu.

Halikadhalika tuwazindue na wenzetu walioko mikoani wabadilo mitaa kuipa majina ya wazalendo waliopigania uhuru wa Tanganyika.
Tanga: Rashid Heri, Sheikh Abdallah Rashid Sembe na wengineo.

Moshi: Mama bint Mwalimu, Amina Kinabo, Halima Selengia, Yusuf Olotu na wengineo.
Tabora: Bilal Rehani Waikela, Zarula bint Abdulrahman, Nyange bint Chande na wengineo.

Dodoma: Omari Suleiman, Haruna Taratibu, Alexander Kanyamala na wengineo.
Lindi: Yusuf Chembera, Salum Mpunga, Suleiman Masudi Mnonji na wengineo.

Mikindani: Msham Awadh, Ahmed Adam na wengineo.
Kilwa: Abdulkarim Hajj Mussa Jamadar, Mwinyi Mcheni Omar na wengineo.

Hawa wazalendo wako wengi nchini kote ni jukumu la wakazi wa sehemu zote wawatambue hawa mashujaa waliopigania uhuru wa Tanganyika.

PICHA: Nyumba ya Ahmed Adam ndiyo nyumba aliyolala Mwalimu Nyerere safari yake ya kwanza Mikindani mwaka wa 1956.

Mwalimu Nyerere Kilwa alikuwa akilala nyumba ya Mwinyi Mcheni Omar na alikuwa akipakiwa kwenye pikipiki ya Abdulkarim Hajj Mussa Jamadar kuzunguka vijijini kuitangaza TANU.

Ofisi ya kwanza ya TANU Southern Province ilikuwa nyumbani kwa Suleiman Masudi Mnonji, Makonde Street.

Screenshot_20220218-212306_Facebook.jpg
 
YAAN HAO WAPIGANIA UHURU WOTE WALIKUA WAISLAMU ?????? HATA MOSHI DUUUHH?????
Mdogo...
Watu wengi wamepata kuniuliza swali hili kwa nini Waislam wanaonekana wengi katika TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika?

Watu wengi wamepata kuniuliza imekuwaje historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika hawa wazalendo unaowataja katika historia ya uhuru hawajatajwa popote?
 
Hayo majina ni kamati ya ujenzi wa msikiti au.acha udini
Mdukuzi,

Abdulrahman Ali Msham sasa ni mtu mzima na ana umri wa miaka 65.

Wakati TANU inaasisiwa Dar es Salaam mwaka 1954 yeye alikuwa mtoto wa miaka minne.

Majuma machache yaliyopita alikisikia kipindi kilichorushwa na Radio Kheri 104.10 FM kuhusu safari ya Mwalimu Nyerere UNO mwaka 1955.

Kwa kauli yake mwenyewe anasema kipindi kile kilimrudisha nyuma sana akamkumbuka marehemu baba yake Ali Msham ambae alikuwa mmoja wa wazalendo waliokuwa mstari wa mbele katika kupambana na ukoloni.

Abdulrahman Ali Msham akawa na hamu kubwa ya kukutana na aliyekuwa akieleza safari ile ya kihistoria.

Alikuwa na hamu kwa kuwa na yeye alikuwa na machache angependa kueleza nini baba yake Mzee Ali Msham alifanya katika TANU miaka ile ya 1950.

Abdulrahman alianza kwa kueleza kuwa baba yake alikuja Dar es Salaam kutoka Kilwa katika miaka ya 1950 akiwa fundi seremala na likuwa akifanya shughuli zake za kutengezeza samani Mtaa wa Kariakoo na Congo.

TANU ilipoasisiwa mwaka wa 1954 baba yake alijiunga na kuwa mwanachama kwa kukata kadi ya TANU.

Makazi yake yalikuwa Mtaa wa Jaribu Magomeni Mapipa ambako alikuwa akiishi kwenye nyumba yake mwenyewe.

Katika hamasa zile za kupambana na ukoloni baba yake alitoa chumba kimoja katika nyumba yake akafungua tawi la TANU na yeye mwenyewe akiwa mwenyekiti.

Katika harakati zile za kupambana na ukoloni alisikitishwa na hali ya ofisi ya Mwalimu Nyerere pale New Street kwa kuwa haikuwa na samani za maana sawa na hadhi ya rais wa TANU.

Baba yake alirejea kwenye kiwanda chake pale Mtaa wa Kariakoo na Congo akatengeneza meza ya ofisi yenye hadhi ya rais wa TANU pamoja na viti kadhaa.

Mzee Ali Msham alimwalika Mwalimu Nyerere kwenye tawi la TANU la Magomeni Mapipa ili amkabidhi samani mpya kwa ajili ya ofisi yake.

Mwalimu Nyerere alifika pale kwenye tawi la TANU na katika sherehe fupi Mwalimu Nyerere akakabidhiwa samani ile.

Kumaliza mazungumzo yetu Abdulrahman Msham alinikabidhi picha za baba yake za wakati ule wa kupigania uhuru.

Picha hizo nami naziweka hapa kwa ajili ya kuhifadhi na kuthamini mchango wa wazee wetu mashujaa waliopigania uhuru wa Tanganyika lakini kwa bahati mbaya michango yao haijathaminiwa.

1645288655018.png

Picha hiyo inamwonyesha Mwalimu Nyerere akipokea samani hiyo iliyotengezewa na Mzee Ali Msham na aliyesimama wa kwanza kulia ni Mzee Ali Msham mwenyekiti wa tawi la TANU Magomeni Mapipa wakati TANU inawaunganisha wananchi kupigania uhuru wa Tanganyika.
 
Kiongozi mimi ni Muislam lakiSri
Sri...
Udini gani ambao mimi nimeleta hapa katika mambo ya kitaifa?

Hebu angalia hii picha hapo chini iliyopigwa nje ya tawi la TANU nyumbani kwa Ali Msham Magomeni Mapipa mwaka wa 1955.

Siku hii wanachama wa TANU walikuwa wamekusanyika hapo kufanya dua kwa ajili ya safari ya kwanza ya Mwalimu Nyerere UNO.

Kutafiti na kuihifadhi historia hii ni kuleta udini?
Hairuhusiwi kueleza michango ya wazalendo kama Ali Msham?

Ikiwa ni makosa tafadhai nijulishe.

1645289188581.png
 
Ana udini fulani

Sema ndiyo hivyo tunamheshim

Ova
Mrangi,
Nakuwekea picha hiyo hapo chini na nifahamishe nini usichokipenda hapo kwani hao wote ndiyo waliokuwa na Ali Msham na Mwalimu Nyerere katika kupigania uhuru wa Tanganyika.

Kuna ubaya gani kueleza historia ya wazalendo hao?

Ushahidi ni kuwa Mwinjuma Mwinyikambi kapewa barabara kwa mchango wake, halikadhalika Bi. Tatu bint Mzee na Bi. Titi Mohamed.

Tatizo liko wapi kwa mimi kuandika historia za wazalendo hawa na wote wako hapo chini kwenye picha.

1645289796691.png

Waliosimama wa pili kushoto ni Ali Msham (Mwenyekiti wa Tawi
la Magomeni Mapipa) na wa nne ni Bi. Khadija biti Jaffar wa tano
Bi. Mtendwa biti Iddi Sudi, wa sita biti Feruzi wa saba Mama Tindwa
waliokaa wa kwanza ni Mzee Mwinjuma Mwinyikambi na wa tatu ni
Bi. Titi Mohamed na pembeni ni mwanae na baada ya mwanae ni
Bi. Tatu biti Mzee.
 
Hayo majina ni kamati ya ujenzi wa msikiti au.acha udini
Mdukuzi,
Hiyo hapo chini ni kamati ya msikiti ambayo Julius Nyerere na John Rupia wamo?:

Hii si ndiyo historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika na historia ya Mwalimu Nyerere mwenyewe?

Lipi ambalo mimi nimeliweka halikuwapo?

1645290154703.png
 
Unamjua david zimbihile wewe au umekariri wamanyema wa kariakoo ambao bila shaka miaka hiyo mji wa dar es salaam ulikuwa na waisla wengi wengi,kesho inshaaalah nakuletea majina ya wagalatia waliopigania uhuru toka huko bara
 
MAJINA YA MITAA YAHIFADHI HISTORIA

Ndugu zanguni hivi sasa kuna mradi wa Anuani za Makazi (Post Code).
Naamini sote tunashausikia kwa kuwa serikali imeutangaza.

Mradi huu ulitakiwa uchukue miaka 5 lakini Rais Mama Samia ameamua huu mradi uwe "Operation Anuani za Makazi" na ukamilike kwa miezi 5 yaani January hadi May 2022.

Katika mradi huu kupitia serikali za mitaa wakazi wa wana fursa ya kubadili jina la mtaa kwa sababu maalum.

Mathalan Mtaa wa Tandamti ni mtaa akiishi marehemu Mzee Mshume Kiyate ambae mchango wake katika kupigania uhuru wa Tanganyika hakuna asiyeufahamu.

Hii ni fursa nzuri ya kubadili jina la Mtaa wa Tandamti kuwa Mtaa wa Mshume Kiyate.

Muhimu tuwafahamishe na wengine ili ikiwa ipo haja na wao wabadili majina ya mitaa yao kwa kuenzi historia ya Dar es Salaam na wazee wetu waliofanya makubwa katika mji huu.

Halikadhalika tuwazindue na wenzetu walioko mikoani wabadilo mitaa kuipa majina ya wazalendo waliopigania uhuru wa Tanganyika.
Tanga: Rashid Heri, Sheikh Abdallah Rashid Sembe na wengineo.

Moshi: Mama bint Mwalimu, Amina Kinabo, Halima Selengia, Yusuf Olotu na wengineo.
Tabora: Bilal Rehani Waikela, Zarula bint Abdulrahman, Nyange bint Chande na wengineo.

Dodoma: Omari Suleiman, Haruna Taratibu, Alexander Kanyamala na wengineo.
Lindi: Yusuf Chembera, Salum Mpunga, Suleiman Masudi Mnonji na wengineo.

Mikindani: Msham Awadh, Ahmed Adam na wengineo.
Kilwa: Abdulkarim Hajj Mussa Jamadar, Mwinyi Mcheni Omar na wengineo.

Hawa wazalendo wako wengi nchini kote ni jukumu la wakazi wa sehemu zote wawatambue hawa mashujaa waliopigania uhuru wa Tanganyika.

PICHA: Nyumba ya Ahmed Adam ndiyo nyumba aliyolala Mwalimu Nyerere safari yake ya kwanza Mikindani mwaka wa 1956.

Mwalimu Nyerere Kilwa alikuwa akilala nyumba ya Mwinyi Mcheni Omar na alikuwa akipakiwa kwenye pikipiki ya Abdulkarim Hajj Mussa Jamadar kuzunguka vijijini kuitangaza TANU.

Ofisi ya kwanza ya TANU Southern Province ilikuwa nyumbani kwa Suleiman Masudi Mnonji, Makonde Street.

View attachment 2123244
Uhuru tulioupata umetusaidia nini kutuondolea umasikini watanganyika au watanzania kilichobadilika ni mkoloni. Hivi sasa tupo na mkoloni mweusi aitwae CCM
 
Unamjua david zimbihile wewe au umekariri wamanyema wa kariakoo ambao bila shaka miaka hiyo mji wa dar es salaam ulikuwa na waisla wengi wengi,kesho inshaaalah nakuletea majina ya wagalatia waliopigania uhuru toka huko bara
😄😃😀😆😁Mkuu Umechafukwa
Kesho Orodha Ya Wagalatia, Warumi, Hewani
 
pointt muhim inasahaulka kihistoria.da res zalam wakat ule white colar jobs ziliku zimeshikwa na waafrika wachache ambao hawakutaka kuriisk kaz zao .so kushuhudia .katika Tanu Kanzus and balakashiaz huwez kwepa mana wao ndio walikua majority of self employed
waliokua civil services kama kina Abdul Sykes walipata msukosuko kushirik siyasa

Sent from my TECNO CF7 using JamiiForums mobile app
 
Unamjua david zimbihile wewe au umekariri wamanyema wa kariakoo ambao bila shaka miaka hiyo mji wa dar es salaam ulikuwa na waisla wengi wengi,kesho inshaaalah nakuletea majina ya wagalatia waliopigania uhuru toka huko bara
Mdukuzi,
Hili la Wamanyema silo tunalojadili.

Wewe kwa kejeli, kebehi na dharau umeandika maneno haya: ''Hayo majina ni kamati ya ujenzi wa msikiti au.acha udini.''

Sasa unakuja na habari za Wamanyema.
Hutaki tena chembelecho, ''Kamati ya Msikiti.''

Hiyo picha hapo chini ni wanachama wa TANU Tawi la Ali Msham 1950s
tunapigania uhuru wa Tanganyika.

1645296920687.png

Waliosimama wa pili kushoto ni Ali Msham (Mwenyekiti wa Tawi la
Magomeni Mapipa) na wa nne ni Bi. Khadija biti Jaffar wa tano
Bi. Mtendwa
biti Iddi Sudi, wa sita biti Feruzi wa saba Mama Tindwa
waliokaa wa kwanza ni Mzee Mwinjuma Mwinyikambi na wa tatu ni
Bi. Titi Mohamed na pembeni ni mwanae na baada ya mwanae ni
Bi. Tatu biti Mzee.
 
Mdukuzi,
Hili la Wamanyema silo tunalojadili.

Wewe kwa kejeli, kebehi na dharau umeandika maneno haya: ''Hayo majina ni kamati ya ujenzi wa msikiti au.acha udini.''

Sasa unakuja na habari za Wamanyema.
Hutaki tena chembelecho, ''Kamati ya Msikiti.''

Hiyo picha hapo chini ni wanachama wa TANU Tawi la Ali Msham 1950s
tunapigania uhuru wa Tanganyika.

View attachment 2124306
Miaka hiyo mji mwisho magomeni wengi dini moja,weka na picha ya wapigania uhuru mkoa wa mbeya na iringa,uhuru haukupiganiwa kariakoo na gerezani pekee.huyo mzee haruna taratibu ni babu yangu aliyehamia dodoma,ntakuletea rafikize wa imani nyingine aliokuwa nao kwenye harakati,japo nae alikuwa mmanyema kama mimi ila sifagilii approach yako ya mukhtadha wa unachokiandika
 
What's wrong with Tandamti ?

Kabla hatujataka kubadilisha hilo Tandamti labda tujiulize kwanini liliitwa hivyo..., Binafsi jina fupi rahisi na linatamkwa kwa urahisi naona linafaa
 
Back
Top Bottom