Majina ya Magari ya TOYOTA Na maana yake

Kasomi

JF-Expert Member
Sep 3, 2014
6,643
2,000
MAJINA YAMAGARI YA TOYOTA NA MAANA ZAKE.
FB_IMG_16221485157990614.jpg

Kampuni ya Toyota ilianzishwa na mtu anayeitwa toyoda na si Toyota kama wengi wanavyofikiria . mwanzo ilikuwa ikijulikana kwa jina la katakana . kampuni ya Toyota ni ya mtu na famila yake .

katika ukuaji wa biashara , katakana co.ltd , ilibadilishwa . dhumuni kubwa lilikuwa kushindana katika soko la biashara ya magari nje ya nchi.

Kimaandishi kwa kijapani TOYODA , inatumia alfabeti 10 . TOYOTA inatumia alfabeti 8 . kwa mujibu wa wajapani namba 8 ni namba ya bahati , ikampendeza mr. toyoda kuita kampuni Toyota.

Katika logo ya TOYOTA kuna ubunifu , siri na maana kubwa . logo ya Toyota ambayo imechorwa kama zero na michoro ndani yake . kuna “T” iliyojificha , ikimaanisha herufi ya kwanza ya Toyota. Kuna maneno yote sita kwa alfabeti yaliyojificha yakimaanisha neno Toyota .

Maana halisi ya logo hiyo , iliyoanzishwa tangu mwaka 1990 katika muundo wa overlapping ellipses logo , inamaanisha muunganiko wa moyo wa mteja na moyo wa bidhaa za Toyota.

Majina mengi ya Toyota model , yalianzishwa na maana zake kwa sisi watu wa kiroho kila gari , muundaji alilinenea jambo na hayo lazima yataambatana na gari husika. Unaweza kuchagua kwa ubora na matumizi yako pia . kuna majina kama haya ya Toyota mfano.
TOYOTA RAV4 - ni kifupi cha maneno recreational active vehicles with 4wd . yaani ni magari ya mapumziko hasa Kama unaenda kupumzika sehemu za pembezoni mwa mji , zisizo na barabara bora ( outdoors recreation activities ). Waliziweka katika kundi la SUV cars ( sport utility vehicles).

TOYOTA HILUX – mkusanyiko wa maneno high na luxury . kiingereza

TOYOTA CARINA – ni mkusanyiko wa nyota kijapani.

TOYOTA HIACE – ikimaanisha TOYOACE na wakaweka HI (high) , ikiashiria kuwa imepita matoleo yote ya “ACE” ambayo yalikuwa magari kwa ajili ya kubeba wafanyakazi .

TOYOTA LAND CRUISER – neno la kijapani lilitolewa likimaanisha kwenda popote . neno la kizungu likauzika zaidi na kuita land cruiser.

TOYOTA SIENNA - jina hili lilitolewa kwa heshima ya mji wa sienna italia.

TOYOTA ALTEZA – kwa maana ya neno la kiitaliano likimaanisha heshima na urefu wa kitu.

TOYOTA VEROSSA – limepewa kutokana na neno la kiitaliano VERO( ukweli), na ROSSO ( nyekundu ).
TOYOTA KLUGER – imetokana na neno la kijerumani , kisifa (adjectives) , ikimaanisha “KLUG” , ikimaanisha busara au nzuri. Kuna kuger l na v . l =liberty na v= victory .

TOYOTA VANGUARD –ni neno lililomaanisha kwa wajapani , wale waliombele katika maendeleo . neno la kiingereza likauzika zaidi … na hili ndilo gari nilipendalo sana.

TOYOTA COASTER – ni neno au jina la meli inayobeba mizigo kutoka bandari moja kwenda nyingine .

TOYOTA NOAH - limetokana na neno la kijapani sauti nyororo, ya kuburudisha .

TOYOTA HARRIER – ni ndege anayewinda kama tai au mwewe .

TOYOTA PASSO – hatua ,steps

TOYOTA IST - Ni kifupisho cha mwisho kutokana na maneno ya mwisho kama stylist , artist nk . ambao ni watu wenye shauku na kitu Fulani .

TOYOTA DYNA – ni magari ambayo yalibuniwa na wafanyakazi wenyewe wa Toyota , wakamaanisha neno , DYNAMIC kwa kiingereza

FB_IMG_16221485157990614.jpg

Na Toyota zingine...
 

Mr Q

JF-Expert Member
Aug 16, 2012
10,890
2,000
Passo hatua au steps 😁😁😁 ndio maana tunasikika kwa ubugiaji mdogo wa mafuta
 

ibanezafrica

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
5,467
2,000
Ati hata
Crown, Prado, Brevis, Corolla, Corona,
Zote toyota naona mtoa mada ametupa hizo chache tu kwa faida ya wengi ambao tulikua gizani,hongera zake....hizo zingine basi tujiongeze na sie ktk tafasiri lakini mimi nimemuelewa vizuri
 

ibanezafrica

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
5,467
2,000
Land cruiser peke yake ndio gari ya maaana kwa toyota nzima
Na Toyota brand ndio gari namba moja kwa ubora hasa huku barani kwetu afrika ikiwa hutaki stress za kusumbuliwa na matengenezo ya mara kwa mara ,ni kama zamani ilivyokuaga simu ya Nokia

Ukitaka presha jiingize kwenye
Honda Crv
Land lover Discovery
Land lover freelander,
Benz
Duet....
 

Ugumu wangu

JF-Expert Member
May 6, 2021
1,616
2,000
Hapa ndio naomba mnitoe tongo tongo wakuu Kuna landcruicer V8 Ina speed 180 kph alafu ni ya mwaka 2019 alafu Kuna 260kph pia ya mwaka huo huo je tofauti hapa ikoje ?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom