Majina saba yaipa kamati kuu ya CCM wakati mgumu

Hapo pamekaa sawa! Sioni hata mmoja ambaye amewahi kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania. CCM wakiamua kumchinja mtu wanatumia kauli kama vile sasa ni zamu ya wanawake; basi unakosa sifa na huwezi kujigeuza jinsia. Mzee Sitta analikumbuka hili. Sasa zamu hii ni kwamba wale waliowahi kuwa Mawaziri wakuu wanaishiaa Kamati Kuu! Naona Dr. John Pombe Magufuli akipenya na kuipeperusha bendera ya CCM. Ana mtaji wa wananchi. Siamini kama ana mtaji ndani ya Halmashauri kuu lakini tapenya kwa ile kauli ya Mwenyekiti kwamba wanataka mtu anayekubalika kwa wananchi; Magufuli anakubalika.

..utamuuza vipi Magufuli kwa haya makundi yanayom-support Lowassa?

..hivi mmefuatilia namba za wadhamini anaowapata Lowassa kulinganisha na wenzake?

..demokrasia gani hiyo ambapo chama kinamdhulumu mgombea anayependwa zaidi na wanachama wenzake?

cc Rev. Kishoka, Mkandara
 
Last edited by a moderator:

Hivi kuna principle ya kuangalia umati wa wadhamini? Kama wamelipwa kuja pale!! Nitashangaa kama ccm watakitumia hiki kama kigezo.Kuna ambao misafara yao ya kutafuta wadhamini ina waandishi wa vyombo vya habari!! Hivi hao waandishi posho zao zinalipwa na waajiri wao? Swali rahisi itakuwa kwa nini mwajiri A alipe posho kwa waandishi kwenye msafara wa mtia nia X ila asilipe posho au kupeleka waandishi wake kwa mtia nia Y. Na mtia nia X kila anapoenda umati wake unaonekana kwenye taarifa ya habari wakati mtia nia Y hajulikani kaenda wapi na kadhaminiwa na umati au mmoja mmoja. Kama CCM haiwezi kwenda zaidi ya hizo report za umati wa wadhamini, tunajua kitakachofuata ni mini.

Ukiangalia vizuri, kum 'regulate' Mengi ili asivitumie vyombo vyake vya habari Ku distort hali ya kisiasa ni rahisi sana ikiwa tuna mioyo safi na nia yetu ni kufanya regulation. Kuna makosa mengi sana ya kitaaluma yanafanywa na hizo media zake. Ila wenye mamlaka wanakaa kimya hadi unashangaa kwa nini wanafikia kutunga sharia ya media ambayo inaonekana kumtarget mengi wakati ni rahisi tu kumregulate kwa kutumia sheria zilizopo ila hawafanyi hivyo!!!
 
Last edited by a moderator:
ahahaha! wasoma kwa ladha basi nitaweka fanta ndani yake!...nimesema siandiki kwa kukushibisha wewe bali hutoa mawazo yangu juu ya hoja iliyopo. Talking of insight please nakushauri skim first you ain't an in depth reader. Besides you're not alone, most of you folks have lower comprehension, 'cause your minds are preoccupied with recognizing on which side I stand..Mnaandika na kusoma kwa ushabiki insight utaiona wapi?

Kwenu siku zote JF ni Uadui na ushindani, CCM vs CDM - Uisaam vs Ukristu yaani bado mna mila na desturi za mababu hambadiliki. Hii mada inahusu majina saba ya wagombea, wewe umeshuparia Mkandara kila napokukamata pabaya kwa hoja hukosi kujitetea ati unashindwa kufuatilia porojo ndefu, ilihali walonisoma wamenielewa! sipo hapa kukiridhisha wewe Ain't Casanova!

= umeshupalia

Ukiandika kwa ufupi unaeleweka, lakini yale makala yako amabayo mpaka yanajisahau kichwa kikowapi na miguu iko wapi, hayafai.

Ni ushauri wa bure tu, ukipenda uchukuwe usipopenda uwache.
 
..utamuuza vipi Magufuli kwa haya makundi yanayom-support Lowassa?

..hivi mmefuatilia namba za wadhamini anaowapata Lowassa kulinganisha na wenzake?

..demokrasia gani hiyo ambapo chama kinamdhulumu mgombea anayependwa zaidi na wanachama wenzake?

cc Rev. Kishoka, Mkandara
kupendwa ni mojawapo ya sifa ila siyo sifa pekee!
 
..utamuuza vipi Magufuli kwa haya makundi yanayom-support Lowassa?

..hivi mmefuatilia namba za wadhamini anaowapata Lowassa kulinganisha na wenzake?

..demokrasia gani hiyo ambapo chama kinamdhulumu mgombea anayependwa zaidi na wanachama wenzake?

cc Rev. Kishoka, Mkandara
Mkuu kuhusu wadhamini, unajua inachekesha sana maana kanuni yao inahitaji mgombea kupata wadhamini wanachama wasiopungua 45 au 50 kila mkoa au wilaya kitu kama hicho, kwa hiyo hata Ukipata wadhamini 5,000 haisaidii kitu maana sheria yao inataka tu uwe na wadhamini kiasi hicho.

Ni sawa na kuanzisha chama unatakiwa kuwa na idadi fulani ya wanachama waasisi kila mkoa haina maana unapokuwa na wanachama wengi ndio chama kitapata usajili tofauti...
 
= umeshupalia

Ukiandika kwa ufupi unaeleweka, lakini yale makala yako amabayo mpaka yanajisahau kichwa kikowapi na miguu iko wapi, hayafai.

Ni ushauri wa bure tu, ukipenda uchukuwe usipopenda uwache.
tatizo ni wewe unayetaka maneno machache ujue miguu iko wapi? mimi kazi yangu sii kukutandaza miguu bibie tafadhali..
 
Mkuu kuhusu wadhamini, unajua inachekesha sana maana kanuni yao inahitaji mgombea kupata wadhamini wanachama wasiopungua 45 au 50 kila mkoa au wilaya kitu kama hicho, kwa hiyo hata Ukipata wadhamini 5,000 haisaidii kitu maana sheria yao inataka tu uwe na wadhamini kiasi hicho.

Ni sawa na kuanzisha chama unatakiwa kuwa na idadi fulani ya wanachama waasisi kila mkoa haina maana unapokuwa na wanachama wengi ndio chama kitapata usajili tofauti...

Hili la wadhamini, na jinsi walivyo bize kukusanya maelfu wakati wanahitajika wadhamini 30 tu kila mkoa ni dalili kuu ya jinsi gani kiongozi HUSIKA ni BOYA na hafai kukabidhiwa nchi.

Yani hawa watu wamekuwa kama mata*h*ra kwa vitendo vyao visivyo-reflect cheo wanachotaka kupewa. For me it shows extremely poor showing in judgement.

nikitazama sarakasi, wanaocome out as president ready ni Mwandosya,magufuli, Pinda na Mahiga. hao waliobaki wana-act kama over excited teenage girls in the first trip to Disneyland. I would not want them near the State house.
 
Usisahau

*****************

Kupiga kura
Diamond Platnumz kategori 3 (tatu) - Best MALE, Best COLLABORATION na Best LIVE and Vanessa 1(moja) -- Best FEMALE

ingia kwa link hii chini

http://mama.mtv.com/voting/

Bonyeza bonyeza VOTE usichoke

******************
 
Usisahau

*****************

Kupiga kura
Diamond Platnumz kategori 3 (tatu) - Best MALE, Best COLLABORATION na Best LIVE and Vanessa 1(moja) -- Best FEMALE

ingia kwa link hii chini

MAMA 2015

Bonyeza bonyeza VOTE usichoke

******************

Vipi wewe?is this spamming au ndio vurugu tu?
 
tatizo ni wewe unayetaka maneno machache ujue miguu iko wapi? mimi kazi yangu sii kukutandaza miguu bibie tafadhali..

Sasa hayo matusi ambayo sikutegemea kutokea kwa mtu mzima na unaeheshimika humu JF kama wewe.

Nilikuwa nnajaribu tu kukupa ushauri wa bure alkini umeuchukulia vibaya.

Amma shule ulisomea ujinga amma huo ujinga unao ndani ya damu, uiinga wa jadi uliourithi genetically na ndiyo maana unapofahamishwa mema huyaoni.

Pole sana.
 
Mkuu kuhusu wadhamini, unajua inachekesha sana maana kanuni yao inahitaji mgombea kupata wadhamini wanachama wasiopungua 45 au 50 kila mkoa au wilaya kitu kama hicho, kwa hiyo hata Ukipata wadhamini 5,000 haisaidii kitu maana sheria yao inataka tu uwe na wadhamini kiasi hicho.

Ni sawa na kuanzisha chama unatakiwa kuwa na idadi fulani ya wanachama waasisi kila mkoa haina maana unapokuwa na wanachama wengi ndio chama kitapata usajili tofauti...

..that is one way of looking at it.

..tatizo lako umeangalia mambo kikanuni na kisheria.

..kwasababu hili ni zoezi la KISIASA basi inabidi uliangalie suala hili kwa mtizamo wa kisiasa.

..sasa kisiasa Lowassa anaonyesha kwamba anaungwa mkono na wanachama wengi zaidi wa CCM.

..simuungi mkono Lowassa, lakini nadhani huu umati unaojitokeza kumuunga mkono ni BIMA na KINGA yake dhidi ya viongozi wenzake wasiompenda.

cc Kimbunga, christine ibrahim, ocampo four
 
Last edited by a moderator:
Hivi kuna principle ya kuangalia umati wa wadhamini? Kama wamelipwa kuja pale!! Nitashangaa kama ccm watakitumia hiki kama kigezo.Kuna ambao misafara yao ya kutafuta wadhamini ina waandishi wa vyombo vya habari!! Hivi hao waandishi posho zao zinalipwa na waajiri wao? Swali rahisi itakuwa kwa nini mwajiri A alipe posho kwa waandishi kwenye msafara wa mtia nia X ila asilipe posho au kupeleka waandishi wake kwa mtia nia Y. Na mtia nia X kila anapoenda umati wake unaonekana kwenye taarifa ya habari wakati mtia nia Y hajulikani kaenda wapi na kadhaminiwa na umati au mmoja mmoja. Kama CCM haiwezi kwenda zaidi ya hizo report za umati wa wadhamini, tunajua kitakachofuata ni mini.

Ukiangalia vizuri, kum 'regulate' Mengi ili asivitumie vyombo vyake vya habari Ku distort hali ya kisiasa ni rahisi sana ikiwa tuna mioyo safi na nia yetu ni kufanya regulation. Kuna makosa mengi sana ya kitaaluma yanafanywa na hizo media zake. Ila wenye mamlaka wanakaa kimya hadi unashangaa kwa nini wanafikia kutunga sharia ya media ambayo inaonekana kumtarget mengi wakati ni rahisi tu kumregulate kwa kutumia sheria zilizopo ila hawafanyi hivyo!!!

..wewe inaelekea unamchukia Lowassa.

..hata mimi simpendi Lowassa, lakini lazima tukubali kwamba jamaa ana mtandao mkubwa unaomuunga mkono.

..hakuna mtu amepigwa vita ndani na nje ya CCM, lakini yote hayo hayajamvunja nguvu.

..kwa upande mwingine, kinachoendelea kinaweza kuwa kielelezo cha maoni ya wana-CCM kuhusu ufisadi na mafisadi.
 
Napokuona senior kama , wewe unashabikia mtandao uliotunyima rais bora 2005 , na Leo unaushabikia kwa staili ile ile ya 2005 , ya kununua kwa kutumia rushwa, na siasa chafu, kununua media sizani kama unatenda haki ,

Fikiri kwa maslahi ya taifa na si maslahi ya mafisadi na huo mtandao
 
..ninachoeleza mimi ni hali halisi iliyopo ktk CCM.

..kama wana-ccm wangekuwa wanakerwa na ufisadi basi wasingemuunga mkono Lowassa kwa kiwango wanachofanya sasa hivi.

..nadhani hukunielewa tu. sishabikii mtandao, na sijawahi kushabikia mtandao.
 
Back
Top Bottom