G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 12,463
- 39,883
Majina saba ya watia nia ya urais kwa tiketi ya CCM yameonekana kuipa wakati mgumu kamati kuu ya CCM itakayoanza kukaa kwa ajili ya mchujo mwishoni mwa mwezi huu, imefahamika.
Majina hayo yameanza kujadiliwa miongoni mwa wana kamati hiyo kuu ambayo ni Dr. Salim Ahamed Salim (anayetarajiwa kuchukua fomu jumatano), Makongoro Nyerere, Prof. Mark Mwandosya, Mizengo Pinda, January Makamba, Benard Membe na John Magufuli
Hata hivyo jina la Benard Membe linatarajiwa kutoa upinzani mdogo kwa wana kamati kwani ameelezwa kutumia mitandao ya watu kukigawa chama.
Kamati kuu ya CCM imatarajiwa kupitisha majina matano tu hivyo kuhitajika kuwaondoa majina mawili.
Wana-CC kadhaa wamenukuliwa kuwa hata rais Kikwete haoni haja ya kumuunga mkono Membe ili kukwepa kunyooshewa kidole siku za usoni hivyo kuipa kamati hiyo kuu urahisi wa kukata jina la Membe kwa kigezo cha makundi.
Hata hivyo Membe ameanza kampeni za chini kwa chini kugombea ubunge wa jimbo la Lindi mjini baada ya kuahidiwa cheo kikubwa na mmoja wa wanaopigiwa chapuo kufika mbali kwenye vikao vya mchujo baada ya kuonyesha nia ya kumuunga mkono.