Majina mengine ni soooo

Bujibuji Simba Nyamaume

Platinum Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
78,133
Reaction score
166,010
Jamani, baba mwenye nyumba wa ninapoishi, jumamosi alijaaliwa kupata mtoto wa kiume. Mtoto kapewa jina Graduation.
Nikauliza kwanini mtoto aitwe hivyo, kasema anataka mwanawe asome hadi awe Rais.
Kimoyomoyo nkasema, tumtakie kila la kheri, asije kuwa rais wa chama cha wapigadebe Manzese
 
Buji kwani we hujui ma graduate ndio wanaokuwa marais?
Mbaya zaidi siku hizi chekechea wanagraduate
 
Jina kama Bujibuji... kwa roho safi kabisa sijawahi sikia na ingawa
naliona bado sijalizoea.... naomba niambie maana yake nini...
 

Kuna jamaa toka Kaskazini mwa mchi yetu nilisoma naye anaitwa GODLISTEN J. HEAVENSEND...Kama tungetumia kigezo cha Baba Graduation basi huyu mate wangu angekuwa ASKOFU🙂
 
jirani yangu mwanae anamwita MAIN ROAD...kisa mkewe alijifungulia njiani.
Padri kagoma kumbatiza mtoto na ilo jina.nyumbani bado wanamwita mainroad!
 
bujibuji vipi umesharudi kutoka huko kwetu, kama umerudi nakukaribisha sana.
 

babako huuyo makondee nini!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…