Majimbo haya njia nyeupe kwa CHADEMA

Chadema wana uwezo wa kutetea majimbo yao nimesafiri kuja mwz na nimefanya ka research kangu kadogo kwa maboda boda, bar, guest, vijiweni na sehemu ninapofanyia kazi naona wengi zaidi ya asilimia 70 wanaonyesha imani kwa chadema, hasa huku ilemela niliko..kwingine sijafika lakini ntaingia nyamagana kabla sijaondoka
 
mbona husemi ya chadema kama vile ilemela nyamagana meatu musoma mjini ukelewe arusha iringa mbeya mjini hawa wote wamefanya nini kama siyo maandamano kila siku?

Majimbo yote yapo fit wananchi wanasema eti walikuwa wamechelewa kupata maendeleo kwa miaka yote 40+ kitu walichofanya CDM nikujipanga na kutumia vizuri pesa ya walipa kodi.
 
Vipi Mnyika kaleta maji Ubungo? Vipi Halima Mdee kajenga barabara Msasani mandazi road? Vipi Wenje kaishawajengea machinga jengo lao (Machinga Complex).
Watajengaje kama fedha zote za serikali zipo mikonini mwa magamba na magamba hayo hayako tayari kutoa hizo fedha kwenye majimbo yanayoongozwa na upinzani? Angalia kama Arusha, mmekazana kujenga barabara za lami kwa sababu Lema amesimamishwa lengo ikiwa ni kuwahonga wananchi wa Arusha kwa kusema mmefanya maendeleo bila Lema kuhusika. Ingekuwa halmashauri ya jiji la Arusha imeshikwa na upinzani mngezuia fedha za maendeleo. Mnawakwamisha wenzenu kwa kuwanyima fedha halafu mnataka muwakosoe eti wameshindwa kuleta maendeleo. Kwani huko mnakoleta maendeleo ninyi mnatoa fedha zenu kutoka mifukoni mwenu? Na isitoshe katika miradi yote ya maendeleo mnayofanya lazima muibe. Shame on you Magamba.
 
ndio maana mnyika alifanya ziara ya kuzindua visima vya maji ubungo, halima barabara zake zipo katika mpango wa bajeti ya mwaka huu. vp kikwete kamaliza kujenga machinga complex 2 kwa kila manispaa?

Kikwete vipi haya:
Bwawa la samaki umasaini,
Meli mpya ya kwenda bukoba
Uwanja wa ndege mkubwa Bukoba,
Mwenye kuzikumba ahadi za msanii JK aongeze.....
 
kila jimbo linaweza kuchukuliwa na yeyote swala la msingi ni kujipanga tu.
 
Hili jimbo lipo wazi kwa CDM 2015 ni Jimbo la Arusha (zamani ni Arumeru Magharibi) hapa Ole Medeye hana lake kamwe!
 
Mbona majimbo yaliyowazi ni mengi mno it is just a matter of time. Jimbo la Magu,Busega,Kwimba na Sumve yako wazi ni ya kujichukulia asubuhi! Dr Limbu kajisahau anafikiri jimbo kapewa liwe la kwake,huyu mzee hajitambui na kajikatia tamaa kwanza anajua staili iliyotumika kumpa ubunge! Dr kamani nae aliingia kwa matarajio ya kupata uwaziri alivyoukosa nae kbmua kula bata coz alitumia pesa lukuki kupata jimbo hilo! Kwimba ndo kwishnei, bana kuba hata hajui matatizo ya jimboni kwake! Huyu ni janga la kitaifa,alinunua ubunge ili aweze kufanya biashara zake za mafuta! Vyama vya upinzani majimbo hayo yako wazi kabisa.
 
mbona husemi ya chadema kama vile ilemela nyamagana meatu musoma mjini ukelewe arusha iringa mbeya mjini hawa wote wamefanya nini kama siyo maandamano kila siku?

Ukombozi wa nchi kutoka kwenye meno ya mkoloni mweusi (CCM) anaewanyonya wananchi kwa njia ya EPA, RICHMOND, MEREMETA, DOWANS, DEEP GREEN, WIZI WA TWIGA, PEMBE ZA NDOVU n.k hayaji kwa kila mtu kukaa ndani. Ukombozi wa Misri, Libya na Libya haukuja kwa watu kukaa ndani bali ni kwa maandamano.
 
Wanasiasa kwa ujumla kuanzia wanaotuongoza(rais Kikwete na serikali yake) pamoja na upinzani walitoa ahadi za uongo au nyingine hazitekelezeki...ni jukumu la wananchi wajue kuchuja mpunga na mchele.
 
Sema majimbo hayo 2015 yanatakiwa kuwa chini ya chama tawala. By then CDM itakuwa chama tawala.
 
Vipi Mnyika kaleta maji Ubungo? Vipi Halima Mdee kajenga barabara Msasani mandazi road? Vipi Wenje kaishawajengea machinga jengo lao (Machinga Complex).


Maji Ubungo kwa asilimia 60 tayari maeneo yaliyokusudiwa ndani ya mwaka huu wa fedha, kwa Mdee Makongo juu barabara ishachongwa kwa kiwango cha kokoto na imeunganishwa na eneo la Goba jimbo la Mnyika,
 
Makongo juu hivi Mdee amepeleka maji na barabara?du bora Ritha Mlaki,

Makongo juu barabara ishachongwa kwa kiwango cha kokoto na juzi maji yametoka makongo juu mwisho wa daladala kwa mara ya kwanza,sijui ni nguvu zake ama kwa utraratibu mwingine,
 
Hata hapa irnga mjin ha2na mbunge bora monika mbega wa ccm badala ya msigwa
Acha uzushi kabisa.
Pastor Msigwa ni mtu wa watu yupo na wananchi kwa karibu sana, anajitahidi kushirikiana na wananchi bega bega katika maendeleo.

Hivi wewe unamjua vizuri Monica Mbega? Yule mama hatutaki tena hata kumsikia.
Wakati akiwa mbunge alikuwa pia ni mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, akawa anaishi Moshi tu, Iringa hafiki na wala bungeni Dodoma haendi.

*Kumbuka kuwa Iringa ndio mkoa ambao mauaji ya kupangwa na CCM dhidi ya Mwangosi yalitokea, hivyo CCM inachukiwa karibu na kila mtu, hakuna jimbo hata moja mpaka sasa CCM wanauhakika nalo.
 
mbona husemi ya chadema kama vile ilemela nyamagana meatu musoma mjini ukelewe arusha iringa mbeya mjini hawa wote wamefanya nini kama siyo maandamano kila siku?
Mkuu njoo ujionee mwenyewe na wala sio kusimuliwa tu.
Wabunge wa Chadema ni majembe ya ukweli, Chadema wanatenda kwanza kisha ndio wanaongea sio kama CCM kazi yao kuropoka ujinga tu. CCM haiwezi tena kurudisha hata jimbo moja katika hayo.
 
Manyoni mashariki kwa Chiligati kule elimu ya Uraia tu inahitajika! Nasikia yeye kasema hagombei anamrithisha mtu wake wa karibu kitu ninachokiona ni kushindwa vibaya
Mkuu kwa tetesi tu ni kwamba jimbo la Manyoni ni mali ya CHADEMA wakati wowote kuanzia 2013, mikakati karibu yote ya kulichukua imeshakamilika kinachosubiriwa ni kazi kuanza tu.
 
Kule songea ndo usiseme,jimbo lipo wazi kabisa.Nchimbi yupo busy na uwaziri,yaani kwa wakazi wa songea hawajui kama kuna mbunge.
 
Back
Top Bottom