Tuwashauri wapinzani: Mambo yanayopunguza sifa kwa wapinzani ni haya hapa

Tabby

JF-Expert Member
Jan 8, 2008
10,652
2,000
Naomba tuwasaidie VYAMA VYA UPINZANI ili kama wakipenda kujirekebisha, wafanye hivyo kwa misingi ya kuongeza nguvu za hoja badala ya malumbano.

1). Waelewe kwamba Tanzania inawatu wengi wajinga. Na kutumia ujinga wa watu ili kupata nafasi za uongozi kamia wanavyofanya ccm ni uharifu. Ni human abuse. Hivyo tunategemea WAPINZANI wakazie kwenye mahitaji muhimu ya ustawi wa Tanzania na watu wake. Kwa kiwango cha kuelezea waweke nguvu kwa yale maendeleo ambayo waTanzania watayaona na kugusa maisha ya kila siku, lakini ki mkakati wajwe na sera za maendeleo yaliyojuu ya ufahamu wa watanzania wengi ambao ni wajinga katika nyanja zote muhimu.

CCM imekuwa ikitumia ujinga wa Watanzania na dniyo sababu tunaona wanapewa ubwabwa, wengine wanakwenda kukuna nazi majumbani mwa wapiga kura, wengine wanapewa tshirts and kanga, wengine wanaambiwa wakichagua upinzani hawatapata maendeleo as if fedha za maendeleo ni za ccm!. Huu ni uharifu wa kibinadamu.

WAPINZANI pamoja na kuaddress mahitaji halisi ya Watanzania kwa sasa, semeni mtafanya nini ili kufanya sustainable trasformation ya maendeleo ya taifa na kwa kiwango kipi katika miaka 10 kwenye maeneo yote muhimu, kama upatiakanji na matumizi ya Technologia sahihi katika maeneo youte muhimu; Social zikiwemo elimu, afya, michezo na mahusiano nk., Uchumi kwa misingi ya kuongeza tija katika zalishaji mbalimbali za kilimo, viwandani, masoko ya ndani na nje, ufugaji, nk,, kuongeza pato la taifa na maboresho ya maisha ya watu binafsi kwa ujumla,;

Mtangamano wa kisiasa ambao utatanzua madhara ya political marginalization na imbalances ambazo zimeleta madhara makubwa katika sehemu mbalimbali duniani ya mida mifupi na mirefu;, Mazingira ambayo ni changamoto ya kimataifa na ambayo pia tayari tuemona athari zake sehemu mbalimbali katika taifa ya kusababisha migogoro ambayo imeshapelekea upotevu wa mali na m aisha ya binadamu; na Sheria kwa maana ya kupata sheria ambazo zinawiana na maisha ya watu katika mazingira ya sasa na yajayo kwa mitazamo ya uhusiano wa kimataifa na utandawazi. Mfano, sheria zetu zizingekuwa kama zlivyo, isingekuwa rahisi watu kuwa na ujasiri wa kuliingiza taifa katika mikataba ya kifisadi, mauzo ya nchi kwa wachina, kugeuza nchi kuwa yakifalme, kubambikizwa makosa kwa utashi wa mtu ama kundi la watu wachache, n.k.

2) Awamu ya Tano, inayoongozwa na Rais Magufuli imefanya mambo mengi sana kwaa muda mfupi. Kitendo cha kukandia kila juhudi aliyoifanya mkisema hata waliotangulia walifanya, inaudhi watu kwa kuwa ni dhahiri hayo mnayoyasema yalifanyika miaka zaidi ya hamsini. Mnasahau kwamba hata pamoja na uwepo wake laikin hayakuwa yakifanya kazi kama bado yali exist. Mfano Bwawa na Mtera, - Mgao wa umeme kila siku na kufanya uzalishahi na maisha kuwa magumu.

Ujenzi wa Reli - Mnajua kabisa walijenga wakoloni na hazikuwa zikifanya kazi kwa miaka mingi tu.
Elimu - Ninyi wenyewe mnajua ni kwa mamna gani elimu ilishuka na kukosa thamani watu wanaswwga tu bila kufaulu ili kutunza jina la mtawala.
na mengien Mengi.
Rais Magufuli amefanya kazi kubwa ya kufufua miundombinu iliyouliwa na kubadhirishwa na Watangulizi wake, na pia mnajua aliikuta nchi iko katika hali gani baada ya awamu iliyopita. Mnaposhindwa kusema kweli kwamba kafanya mema mengi ndani ya miaka 5 ambayo ni zaidi ya yaliyofanyika kwa miaka 50 iliyopita, mnamkose Mungu na bila Mungu msijidanganye kwamba mtapata kitu. Mwogopeni Mungu semeni Ukweli!.

3). Si wana CCM wala wapinzani wasioelewa kwamba Ccm inatembelea jina la Magufuli na wagombea wake wengi wanafurahia mfumo wa kubebwa na mabao ya mikono. Mnanafasi kubwa ya kushinda majimbo meangi kwa kuwa rais hana Wabunge. Amewatumbua hadi akaanza kurudia tena. Hawana viwango ila tu anafanya afanye nini. Mwenye ufahamu ameelewa ninachomaanisha.

4). Mnaposema mtarejesha mahusiano ya kimataifa yaliyoharibiwa bila kuonyesha kwamba mnatambua mahusiano mengine yalikuwa ni kwa hasara ya taifa, mnawapa watu mashaka kama mtasimamia maslahi ya nchi ama maslahi ya mataifa mengine.

Mnatambua mahusiano na CHINA ni ya kifisadi sana. Na ninyi mmekuwa mkilalamika miaka yote, Leo Rasi amethibiti na wasio nia njema wameanza kuachia nchi yetu, badala ya kusimama katika misingia yenye maslahi kwa nchi, mnaanza kulalamika as if mnafurahia uharibifu uliofanywa na mafisadi wenyeji kwa kushirikiana na wagen.

Mbembe jama anasema alikwend Dubai akapimwa Corona, kwa kuwa anatoka dar Esa laam eti ni kosa la Rais, huu ni ujinga. Wangapi mlipimwa mlikutwa na Corona? Nchi gani ambayo ime control Corona kama Tanzania katika hao mnaodai kuwamiss? Kwa nini hamna uwezo wa kutambua vita vya uchumi vina hla na mikakati kama vita vingine vyovyote? Mnapomlaum Rais hata katika mambo aliyofanya vizuri, huku mnasifia majirani ambao wamnapigika mnaashiria nini? Kwa hili kama hamtaonyesha cleaar Mindset ya kutetea nchi na maslahi ya taifa, na kwamba ninyi mnataka mpate nchi muanzishe ushoga na kuwafurahisha matajifa nyonyaji, acheni kupiga kampeni kwa kuwa hamtapata kura.

5). Lipo suala la Ushoga linazungumziwa kila siku kwamba Tundu Lisu amekubaliana na mataifa yanayoangamia (yaliyoendelea), kuweka uhuru wa sex za jinsia moja ama kufumbia macho waut wa namna hiyo kwa kuliita "Personal Privacy". Huu ni ushetani na usaliti mkubwa kwa misingi na mirathi yetu Watanzania. Kama ndivyo ilivyo na kwamba hamwezi kusimamia values za taifa kwa mataifa kwamba sisi hapa kwetu, hatutafungamanishwa na matakwa ya watu wengine ambayo yako nje ya misingi ya uwepo wa taif letu, ", hamfai kuongoza nchi.

SIMAMENI MLITOLEE HILI UFAFANUZI KINAGA UBAGA KWAMBA HAMKUBALIANI NA USHOGA, MTASIMAMIA MAHUSIANO NA NCHI ZINGINE LAKINI BILNA KUUZA UTU NA NEMBO ZA TAIFA LETU!. Naa kwamba mtahakikisha mahusiano yoyote yanoyoanzishwa, kuendelezwa ama kuboreshwa yatakuwa katika MFUMO HORIZONTAL mo na si mfum overtical wa kukubaliana na kila litokalo huko eti wasaidizi wetu.

6). "... I'm happy to hear from you. Here it has been tough with the virus. Africa is the futur. The whole world news it but the Africans themselves."

Huu mstari nimeuchukua kwenye mawasiliano ya Mke wangu na rafiki yake Mzungu mmja yuko Ubeligjiji. Ikiwa Wanzugu wanajua hili, ninyi mnajitambuaje? Bado mnalilia kupata misaas kutoka ulaya? Uhuru gani na wakiwango gani mtalisaidia taifa?

Acheni kupgia debe sera za utegemezi. Simameni na maendeleo endelevu ya Tanzania na uhusiano unaojenga maendeleo ya Watanzania na Africa. Huu muda Africa yenye akili inachakata namna gani ya kujitegemea bila kutegemea misaada. Ninyi mnataka kufanay nini katia kufanikisha uhuru wa Tanzania na Africa? Mtafanya nini specifically ili kutumia na kuedeneleza raslimali zetu katika kufanikisha uhuru halisi wa Mtanzania?

Acheni propaganda na kutulazimisha ku submit kwa nchi zingine kiasi cya kuuza utu wetu na kuingia kwenye ushoga ama kufuata kile wanasema hata kama hakina maana. Mnang'ang'a nia lockdown. Nchi gani imepona na CORONA kwa mfano kw kufanya lock down?

7). Mliwaongoza watu vizuri kuona matatizo ya kikwete aliyekuw a meaua nchi, ufisadi, rushwa nk. Leo hii mnapogeuka na kuanza kumsifia, inaonekana ham maanish imambo mnayoyoasema kama vile ccm tu wanavyoaghai watu.

Mnapashwa kuwa consistent. Ongeeni matatizo ya CCM namna ilivyoua taifa na hadi leo Rais anavyopata shida kufanya kazi na hawa watu ambao wamekuw amzigo kwake katika kila jambo.

8). Sijaelewa ni kwa nini katiba hamuiongelei na uhabiribu uliofanywa na awamu ya nne katika mchakato wa katiba.

CCM IMECHOKWA SANA, LAKINI ILI MKUBALIKE ONYESHENI UELEWA NA UTAYARI WA KULIUNGANISHA TAIFA NA KULISIMAMIA KATIKA MAENEO YOTE KWA MITAZAMO YA SASA NA YA MUDA MREFU.

Mwenye maoni mengine ongezeeni nami nipumzike.
 

akajasembamba

JF-Expert Member
Dec 24, 2010
277
250
Nitarudi mkuu
"WAPINZANI" Wapinzani wa chama chenu siyo wapinzani wa watanzania, wapinzani wa Yanga ni Simba, sasa timu pinzani ni ipi. Hivi ni vyama mbadala au vyama vya mageuzi hiyo lugha ya wapinzani mnataka watu wawaone maadui, wakati vyama vya siasa ni sawa na makampuni ya biashara au mfano makampuni ya simu, sisi tunachotaka ni huduma bora iwe voda au tigo au airtel au halotel, siyo kuitana "wapinzani" wapinzani na wa kwenu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom