Mwanzi1
JF-Expert Member
- Sep 19, 2016
- 6,000
- 4,586
….lakini Chadema ni nini kwa CUF? Sio jambo la ajabu au la kujificha kwamba CUF ya Maalim Seif ina uhusiano wa karibu na Chadema. Uhusiano huu ni uhusiano wa mkubwa na mdogo, nikimaanisha Chadema ni chama kikubwa kwa CUF ni chama kidogo. Chadema ina wanachama wengi zaidi ya CUF, ina madiwani wengi, wabunge wengi, meya wengi hata majimbo mengi.
Nikichukulia mfano wa wanyama walio kwenye mbuga zetu hapa Tanzania, utaona simba akimwona swala yeye kwake inakuwa ni neema, kwamba leo nita lala vyema, huu mnofu ni size yangu. Simba atapiga kila aina ya hesabu ili asipitwe na baraka ile. Lakini sasa, tukipinduwa sarafu upande wa pili, swala akimwona simba huwa anaona nini? Kwa haraka haraka ninaamani swala anaona hatari au kifo au vyote viwili, kazi iliyobaki kwa swala ni kutimuwa mbio mbazo hajawai kutimuwa maishani mwake.
Chadema ina mengi ya kuneemeka ikijiweka karibu na CUF, kwanza Chadema kinapata uwakilishi mkubwa kwenye maeneo ambayo ni ngome ya CUF bila hata kunyanyuwa mguu. Pili Chadema inajiweka tayari kupata wanachama wengi kama ikitokea CUF kusambaratika maana wanachama wa CUF watakuwa wameshajenga mausiano na wenzao wa Chadema. Ni rahisi kumshinda adui ukiwa ndani ya ngome kuliko nje ya ngome.
Mwaka 2010 uchaguzi mkuu nchini Uingereza ulishindwa kupata mshindi kwasababu hakuna chama kilipata kura zaidi ya asilimia hamsini. Kwa sheria ya nchi hiyo, mshindi watatu anaweza kukubalia na mshindi wa kwanza au wapili ili waunganishe kura zao pamoja namba ya wabunge wao ili kuunda serikali ya mseto. Chama cha Liberal democrat (ambacho kilichukuwa nafasi ya tatu) kikakubalina na chama cha Conservative (ambacho kilikuwa mshindi wa kwanza) waunde serikali ya mseto iliyodumu kwa muhula mmoja (2010-15). Ukumbuke conservative ni chama kikubwa na liberal democrat ni chama kidogo. Lakini uchakuzi wa mwaka 2015 wakagombea kama vyama tofauti matokeo yake Conservative wakapata ushindi mkubwa na kujiongezea majimbo mengi zaidi. Liberal democrat walianguka vibaya sana tokea wabunge 50 mpaka 10 mpaka nafani yao ya chama cha tatu ikachukuliwa na chama kingine.
Sasa CUF kama swala, wamejipanga vipi ndani ya himaya ya simba Chadema? CUF wanauwezo wa kutimuwa mbio za kufa mtu iwapo simba Chadema akiamuwa kulianzisha vanga? Huu ndio mvutamo kati ya Maalim Seif na Prof. Lipumba. Maalim yeye anataka kumsogele simba karibu na sharubu zake wakati Prof. Lipumba anahimiza tuanze mbio kabla janga halijatufikia.