Majiji 5 kwa Uzuri Tanzania

Kasomi

JF-Expert Member
Sep 3, 2014
11,036
20,337
Hii hapa ni orodha ya Miji mizuri Tanzania.
1-Dar es Salaam (Mzizima)
Eneo la mkoa ni jiji la Dar es Salaam ambalo ndilo kitovu cha shughuli za biashara (na za utawala, kwa kiasi fulani) nchini Tanzania, na ni kati ya majiji yanayokua haraka zaidi duniani.

Ni km² 1,800 pamoja na visiwa vidogo 8 na eneo la bahari kati ya pwani na visiwa hivi. Eneo la nchi kavu pekee ni km² 1,393.

Kuna wilaya tano: Kinondoni (wakazi 1,775,049), Ilala (wakazi 1,220,611) na Temeke (wakazi 1,368,881) ambazo zimeongezewa Kigamboni na Ubungo. Kila moja inaangaliwa kama mji. Takwimu hizi ni za mwaka 2012, kwa ujumla idadi ya wakazi ilikuwa 4,364,541.

Wakazi asili wa eneo la mkoa walikuwa Wazaramo pamoja na makabila madogo kama vile Wandengereko na Wakwere. Kutokana na kukua na kupanuka kwa jiji kuna makabila yote ya Tanzania.

2-Mwanza (Rocky city)
Jiji la Mwanza ni mji nchini Tanzania ambao ni makao makuu ya Mkoa wa Mwanza. Mji upo kando la ziwa Viktoria Nyanza Kulingana na sensa ya mwaka 2002 idadi ya wakazi wake ilihesabiwa kuwa 378,327 (ukijumlisha wakazi wa Wilaya ya Nyamagana na sehemu za Wilaya ya Ilemela).


3-Arusha (A city)
Arusha ni jiji la kaskazini mwa Tanzania na makao makuu ya Mkoa wa Arusha. Kiutawala eneo la jiji la Arusha ni sawa na eneo la Wilaya ya Arusha Mjini. Katika sensa ya mwaka 2012, idadi ya wakazi wa wilaya hiyo ilihesabiwa kuwa 416,442

4-Dodoma (Idodomya)
Ilitangazwa kuwa mji mkuu wa Tanzania mwaka 1973, lakini mnamo tarehe 26 Aprili 2018 katika maadhimisho ya miaka 54 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar, rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa awamu ya tano John Magufuli aliupandisha hadhi na kutangaza rasmi kuwa Dodoma ni Jiji. Serikali ya awamu ya tano ilihamia rasmi jijini Dodoma mwaka 2016.

Jiji hili pia ni makao makuu ya Mkoa wa Dodoma na eneo lake linahesabiwa kama Wilaya ya Dodoma .

Eneo la mji liko mita 1135 juu ya usawa wa bahari UB. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, mji wa Dodoma ulikuwa na wakazi wapatao 410,956 waishio humo.

5-Mbeya (Green city)
Mbeya ni mji wa nne kwa ukubwa nchini Tanzania. Idadi ya wakazi imehesabiwa kuwa 385,279 katika sensa ya mwaka 2012. Wengine 300,000 hivi wanaishi katika mazingira karibu na Mbeya mjini.

Kiasili Mbeya ilikuwa eneo la Wasafwa. Siku hizi sehemu kubwa ya wakazi wanaweza kuwa mchanganyiko wa Wasafwa pamoja na makabila ya Wanyakyusa kutoka wilaya za Rungwe na Kyela, Wanyiha kutoka Mbozi, Wandali kutoka Ileje na Wakinga kutoka Makete.




Tazama zaidi video ya mandhari ya majiji hayo.

 
Uzuri?Katika yepi?Majengo maziri,watu wazuri,maisha maziri,hali ya hewa nzuri,uchumi mzuri "unaoshikika" ,rasilimali nzuri au kipi hasa unajikita?Au ndiyo Wanyaturu wanavyosema ..."the beauty is in the eyes"...?
Kuanzia madhari japo nimejikita katika majiji
 
Back
Top Bottom