..mgogoro wa Zitto na CDM ni wa muda mrefu sana.
..kuna wakati CDM waliunda kamati ya kujaribu kupata muafaka na Zitto ilimradi aendelee kuwepo CDM.
..mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo alikuwa ni mama mzazi wa Zitto Kabwe.
..sasa mpaka hapo utaona kwamba CDM walimpenda na kumthamini Zitto, tatizo ni kwamba yeye mwenyewe hapendeki na hathaminiki.
..Pamoja na hizi tuhuma za usaliti, Zitto Kabwe anaamini kwamba ana akili kuwazidi viongozi wote wa CDM. Kutokana na imani yake hiyo anaamini kwamba yeye ndiye anayepaswa kuwa Mwenyekiti na Kiongozi mkuu na siyo hao "vilaza."
JokaKuu, hizi ni siasa, uzushi, na propaganda za kisiasa ambazo zipo sikuzote na hazitakwisha.
Tutoke huko, tusonge mbele.Chadema wana safari yao na ACT na Zitto wana safari yao, ni safari mbili tofauti.Historia itakuja kuandika ni nani alikuwa sahihi kati yao, ni mapema sana sasa.
Ata uchaguzi wa rais ungefanyika mwaka 2008 Lowassa asingekuwa tishio kabisa, lakini vip leo?ndio siasa.Yawezekana kabisa msaliti wako wa leo akawa shujaa wako wa kesho.Vuta subira.Muda utaongea.